Executive Solutions ndiyo inahusishwa na sakata la Jairo? - Marealle akanusha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Executive Solutions ndiyo inahusishwa na sakata la Jairo? - Marealle akanusha!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jul 22, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kweli kampuni hii ndiyo inahusika na sakata la fedha za Jairo au watu wanahisi tu? Kama wao wenyewe wanajua kuwa wanatajwa sehemu sehemu ni vizuri kama watatoa kauli mapema (pre-empty) wale wanakusudia kuitaja. Hata hivyo, kama ni kweli kampuni ilikubali kweli jukumu la kushiriki kugawa hizi fedha kwa namna yoyote nje ya sheria basi inajiweka katika mwanga mbaya sana hasa kwa vile ni kampuni ambayo imekuwa ikitumiwa bila ya shaka kwenye PR nyingine mbalimbali za serikali kama kutangaza timu yetu ya riadha kule ujerumani miaka kama miwili iliyopita. Mapema mwaka huu kampuni hiyo inayoongozwa na Bw. Aggrey Marealle ilidhamini tuzo za waandishi wa habari zinazoendeshwa kila mwaka na MCT.

  Katika kutafuta ukweli, nimepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Mkurugenzi na Afisa Mtendaji Mkuu wa ES Bw. Aggrey Marealle muda mfupi uliopita ambaye kwa kauli nzito na kali amekanusha vikali kuhusika na suala la Jairo akidai kuwa kampuni yake haijawahi kuombwa, kupewa, wala kushiriki mkataba wowote unahusiana na Wizara ya Nishati na Madini, na kuwa hata kama wangeombwa wasingechukua jukumu hilo kwani wao kama kampuni ndogo ya PR ina mwelekeo wake wa shughuli zake na haihusiani na mambo ya bajeti.

  "Na mimi kama Watanzania wengine, nasubiri kwa hamu kusikia ripoti ya hao watu, lakini tetesi kama hizi zinalengo la kutuchafua tu, labda pia kutokana na ushindani wa kibiashara' alisema Bw. Marealle. Nilipomuuliza zaidi kuelezea kama kwa namna yoyote kampuni yake imeshirikishwa katika kugawa fedha hizo kwa wabunge, Bw. Marealle amesema kuwa "categorically" hawakuhusika na sakata hilo kabisa, hawakupewa zabuni wala mkataba wa kufanya jambo kama hilo toka wizara ya nishati.
   

  Attached Files:

 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji:

  Soma Maandiko haya:- (Kitabu Cha Joshua)

  "...But the time cometh when the things which they have hidden shall be revealed and made known, and the truth shall make free those which were bound.."


  Weekend Njema
   
 3. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #3
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  kwa dili kama hili huwa hakuna mikataba wala zabuni......nadhani wakati unaongea nae kama alikuwa na quivaling voice ujue anahusika...maana inaonekana kwa maneno yake haya anatoa povu jingi na kukanusha kutohusika kwa nguvu kweli.........

  lets wait and see...
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Mwanakijiji, niliposikia kuwa kuna kampuni ya PR iliyokuwa imepewa jukumu la kusimamia usambazaji wa bahasha za Jairo nilihisi 'Executive Solution'. Funny that Agrey anasema "kampuni ndogo" ! ndogo kwa kivipi? kugawa bahasha inahitaji kampuni ya ukubwa gani?

  Ni vizuri basi Agrey atoe kauli maana hadi dakika hii imani yangu ni kuwa Executive Solutions ndio watendaji wakuu kwenye hili! toeni statement ili tuondokane na mawazo potofu!
   
 5. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #5
  Jul 22, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  mie umeniacha kbsa? kuna tenda za kugawa fedha/posho? ama tenda ya kuentertain kundi fulani la wabunge? Tanzania yetu sivyo tuijuavyo?
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nimewawekea sehemu ya mahojiano yangu mafupi na Marealle kwenye posti ya kwanza.
   
 7. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #7
  Jul 22, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  Agrey huyu...lazima anahusika....categorically ina maana gani? mgawaji ni planner pia....ameratibu kila kitu from the beginning Agrey namfahamu bana....acha kumtetea MKJJ
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hahaha sasa mimi namtetea vipi tena; nimempa nafasi ya kusema. Maana kutwa nzima jana watu wanazungumza na kutaja jina lake na watu wengine bila ya shaka wametaja kampuni yake kwa uhakika kabisa ndio inahusika. Lakini sijui kama kuna mtu alichukua muda wa kumuuliza on the record. Well, nimempa nafasi ya kusema siyo mimi ninamtetea. I'll do the same thing kwa kampuni yoyote itakayotajwa au mtu yeyote. We can not let the politics of personal destruction to go on unchallenged.

  Kama kasema uongo, ukweli utamfichua; lakini kama kasema kweli, I hope you'll the courage to come back and say you were wrong, you really don't know him as you claim to do.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Fedha zile anagawa waziri mwenyewe kwa mkono wake kwa wabunge wenzake ili kutunza siri. Nyingi kati ya fedha hizi anabaki nazo waziri, naibu wake na Katibu Mkuu. Ngeleja sasa hivi ni tajiri kijana mzawa kwa sababu ya taasisi hizi zilizo chini ya wizara hii. Mliona Kapuya alivyocheza vizuri na akina NSSF. Muda mfupi tu waliokaa Chenge na Makongoro pale MIUNDOMBINU waliondoka hawajambo kabisa, wakapata na ujumbe wa NEC ya CCM na Chenge akaingia CC kwa kishindo kabisa.
   
 10. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #10
  Jul 22, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Nimekupata mkuu hivi ni part gani hawa ES wangeweza ku play katika hilo sakata kwa sababu napata shida kidogo kuona connectivity na hilo sakata. Mi najua baada ya fedha kuingia GST basi mtumishi wa Wizara angezichukua na kuanza kutoa mgao kwa wahusika kwa taratibu wanazozifahamu wao. Au kuna makampuni huwa yanapewa zabuni za kufanya hizo kazi za kusambaza hela mkuu?
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wildcard, unawasaidia kuhamisha magoli sasa Lol- tetesi ni kuwa kuna kampuni ya PR ndiyo imefanya hivyo - siyo Waziri! Well, kampuni iliyokuwa inatajwa ni hii na kama wamekuja kukanusha na kama ni kweli - basi kuna kampuni nyingine, Itajwe na yenyewe tuiweke on the record. Sasa mkianza kusema ni "waziri mwenyewe" nadhani hapa mtakumbana na ugumu mkubwa zaidi wa kuthibitisha. Njia pekee ya kujua nani alihusika ni kwa wabunge waliopewa fedha waseme walizipokea toka kwa nani... kama hayupo ambaye anaweza kujitokeza ni vigumu kweli kumhukumu Jairo... I can see this case crumbling like soaked biscuits..
   
 12. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #12
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Do you think wangeweka mkataba wa kugawa Rushwa?
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji,
  Ni kwa kuwa tu sheria ile ya rushwa ya wakati wa Mwalimu ilishatiwa ndimu. Fedha kwenye akaunti ile zilikotumwa na hizi taasisi hazipo. Kwa vyovyote kuna voucher na hundi viliandikwa pale chuo cha madini kuzichota fedha zile mara moja au kwa mikupuo kadhaa. Wapo watu waliosaini voucher na hundi hizi pale chuoni. Tuanze na hao. Tukilipeleka nje hili litatutatiza zaidi.
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Jul 22, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  i have faith in aggrey mareale.....

  still do....
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Jul 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,672
  Likes Received: 21,903
  Trophy Points: 280
  Executive Solution! la la la! basi kama ni kweli nchi hii imeporomoka shimoni kuliko wengi wetu tunavyofikiri. Suala hili lichukuliwe kwa uzito wa juu maana pengine ni ni tabia ya siku nyingi. Pia uchunguzi ufanywe kuona ni mbunge gani alikwisha pokea ili wananchi wawajue wanaokubali kurubuniwa ili kukandamiza haki zao ili wawaadhibu ipasavyo kwa kutumia sanduku la kura.
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Eti serikali inatuhumiwa halafu inamtuma CAG mtumishi mwingine mtiifu kwa serikali kwenda kuchunguza! Haya mambo Beatrice kayasemea Bungeni. Iundwe tume kama ile ya akina Mwakyembe kwenye Richmond angalau kutuzuga tu.
   
 17. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #17
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Bora kukanusha mapema kuliko kusubiri matokeo ya uchunguzi, inawezekana hata uchunguzi ukikamilika kampuni hii isitajwe lakini bado anapaswa kukanusha kupitia vyombo vya habari
   
 18. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #18
  Jul 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Executive solutions wametumika kama EMS ua sijawaelewa vizuri?
   
 19. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #19
  Jul 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Boss you have faith in Aggrey in what sense??

  That he's so clean to encroach ES into such a deal??
   
 20. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kama fedha ziliingia benki na kutoka kwenye akaunti iliyotajwa na Jairo kwenye barua yake basi yeye ndiye anapaswa kueleza nani walipokea mgao, hakuna haja ya kuanza kuwa na shaka juu ya hilo, ila kwa serikali yetu bado wanaweza kutufanya wajinga wa kufikiri na kupuuza uhalisia mwingine ili kulimaliza jambo hili kijanja janja lakini wajue mwisho ni wao kuzidi kupoteza imani kwa wananchi wake.
   
Loading...