Exclusive: Yajue maeneo yanayoongoza kwa kuvunjwa Nazi za Kafara jijini Dar es Salaam usiku mnene

Njia panda ya Ikulu na Hazina

Hilo eneo wamesema wamejitahidi sana kuvizia kuona kitu kama hicho kwa miaka hii miwili mitatu hawajaona japo wamekiri kwamba kati ya mwaka 2005 hadi 2015 vitendo hivyo vilikuwa vikifanyika japo si kwa sana na kwa vificho na mahesabu makali mno.
 
Wewe ndio mjinga ambae umeshindwa kuusoma uzi na kuuelewa

Mkuu wala usipate nae shida kwani siku hizi nimeshapa dawa ya Watu wanaowashwawashwa na Mimi kama hao humu JF ambapo mara moja ili kuepusha shari nyingi na kunilazimisha niwatukane / niwachambe sasa ninaweka tu katika ignore list yangu ambayo namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba mpaka sasa si haba nina msururu / mnyororo wa Watu ambao nimewaiginoa humu na najua sasa wanajutia kitendo chao cha kuwashwawashwa na Mimi.
 
Kwa Zanzibar kuna junction kama unaelekea CCM kutokea Michenzani na barabara ya kutoka magereza kwenda golf (Maisara) lazima ukute mafuta na vipande vya nazi. Kuna siku nilishangaa zoezi lilifanywa mchana nikishuhudia. Mtu kapakizwa kwenye bodaboda alivyofika pale kaipigiza na chombo kuondoka kwa mwendo kasi.

Sasa Mkuu huko Kwenu Zanzibar huu mchezo si nasikia ni wa kawaida sana tu au?
 
Ndio ulimwengu ulivyo ubaya na wewe huenda pamoja. God created both evil and bad, dini tu zimetuchanfanya, wenzetu wanajua namna ya kucheza na wema na ubaya .
 
Acha tu hiyo kitu noma! Kuna siku msichana sista duu akashuka kwenye bajaji mchana kweupe akavunja nazi njia panda kisha haraka akarudi kwenye bajaji na kutimua. Kuna vijana wakaikimbilia ile nazi wakaanza kuitafuna.
 
Back
Top Bottom