Exclusive: Wizi nyumbani kwa Rais Mstaafu Mwinyi

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Wizi umetokea wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni kumi za kitanzania ndani ya nyumba ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Wafanyakazi wa ndani ya nyumba ambao ni wa Serikali walikamatwa pamoja na wengine watatu ambao ni wajenzi wa kampuni moja binafsi waliokuwa wakifanya matengenezo madogo nyumbani hapo.

Wafanyakazi wa ndani waliachiwa huru na wale wa nje huenda watafikishwa mahakamani karibuni. Fedha hizo inasemekana ni za mtoto wa Mwinyi ambaye inasemekana ni daktari. Fedha hizo alishtukia tu hazipo hajui zilipotea lini na kwa namna gani.

Familia za waliowekwa ndani zinahangaika kuwatoa ndugu zao ambao hawana kabisa historia ya wizi na mmoja wapo ameshuhudiwa akilia kama mtoto.

Jambao la ajabu ni kwamba sheria za kiusalama ni kwamba wakati wa matengenezo mafundi hawaruhusiwi kuingia vyumbani bila mlinzi.

Katika mchakato wa dhamana pale mahakama ya Kinondoni Hakimu amelamba 100,000 kutoka kwa familia hizo tatu za watu masikini, huku afisa mzungusha faili akichukua 30,000.

Uonevu mtupu!!
 
Wizi umetokea wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni kumi za kitanzania ndani ya nyumba ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.

Fedha hizo inasemekana ni za mtoto wa Mwinyi ambaye inasemekana ni daktari. Fedha hizo alishtukia tu hazipo hajui zilipotea lini na kwa namna gani.

Just a minute,... Someone needs to be serious, 10m cash na hujui zimepoteaje? siku hizi banking imekuwa rahisi kiasi kwamba sio lazima kuchimbia bulk cash na ukajisahau ulipoziweka.

Huyo kijana atakuwa tapeli anwazushia hao mafundi au kama si hivyo ana biashara za kichinichini.
 
Kuna mtu amesuggest kuwa huenda alitaka fedha kwa baba kwa hiyo akaamua kuchora haka ka plan ku draw sympathy, u never know.
 
Hakuma mtt mwenye akiki timamu atakayeelewa. Taarifa zinasema mafundi walikuwa wanaingia na walinzi, sasa inakuaje wahusishwe?? Familia ya mzee Mwinyi imeanza utapeli. Mwinyi is now loosing his good reputation.
 
Pesa zetu jamani wacha zirudi tena zikipatikana nyingine chukueni tu halali yenu walala hoi.
 
Ha ha ha ha ha zinarudi in the other way round, halafu milioni kumi unakaa nazo ndani zote ili iweje hizi ishu nyingine zimekaa kimagumashi kweli
 
Wizi umetokea wa kiasi cha zaidi ya shilingi milioni kumi za kitanzania ndani ya nyumba ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Wafanyakazi wa ndani ya nyumba ambao ni wa Serikali walikamatwa pamoja na wengine watatu ambao ni wajenzi wa kampuni moja binafsi waliokuwa wakifanya matengenezo madogo nyumbani hapo.

Wafanyakazi wa ndani waliachiwa huru na wale wa nje huenda watafikishwa mahakamani karibuni. Fedha hizo inasemekana ni za mtoto wa Mwinyi ambaye inasemekana ni daktari. Fedha hizo alishtukia tu hazipo hajui zilipotea lini na kwa namna gani.

Familia za waliowekwa ndani zinahangaika kuwatoa ndugu zao ambao hawana kabisa historia ya wizi na mmoja wapo ameshuhudiwa akilia kama mtoto.

Jambao la ajabu ni kwamba sheria za kiusalama ni kwamba wakati wa matengenezo mafundi hawaruhusiwi kuingia vyumbani bila mlinzi.

Katika mchakato wa dhamana pale mahakama ya Kinondoni Hakimu amelamba 100,000 kutoka kwa familia hizo tatu za watu masikini, huku afisa mzungusha faili akichukua 30,000.

Uonevu mtupu!!
Kama mahakama zetu zitatenda haki, dhamana ni haki ya mshitakiwa sio favour.
Mtoto wa Ruksa ambaye ni daktari ni mmoja na ana kwake. Kwa nini afiche pesa kwa baba?.
Kama ni kweli alipoziweka zilikuwa nyingi nadhani milioni 100 cash! kwa nini mtu ambaye sio mfanya biashara akae na amount kubwa hivyo ya cash?. Inawezekana kwa vile fedha zinabadilishwa ndipo amekwenda kuchukua ile milioni 100 akaibadilishe ndipo akagundua jamaa wamechomoa m.10.

Kwa vile hapo kwa mzee ni watu wa swala sana, kuyapeleka mambo hayo ya pesa ndogo hivyo polisi ndio nini?, sasa si yataibua maswali mengi kuliko majibu, wao si walitakiwa wawaulize tuu aliyechukua, wakikana wote, inapigwa Albadir biashara inakwisha!.

Sasa huyu daktari aitwe na kuieleza mahakama hizo pesa aliweka lini, watu wa takukuru na utawala bora wamuulize amepata wapi cash nying hiyo na kwa nini ikae ndani wakati pale nje kwake kuna Bank na ATM?!.

Poleni mafundi msio na hatia, tena mnabahati mko mahabusu tuu, mwenyenu Yusuph kule kwa kayapha, alisingiziwa kumbaka mke wa kayapha na kutupwa jela kifungo cha maisha, mpaka akipotafsiri ndoto ndio ikawa salama yake!.
 
a good piece of inductive reasoning
 
Tusishangae matumizi ya siku ya nyumbani kwa Raisi ni shilingi ngapi? Pesa ya jk haina hata thamani kama mlalahoi leo hii analazimika kutumia zaidi ya mwekundu wa msimbazi kutosheleza mahitaji ya chakula cha nyumbani sembuse kwa raisi. Mimi wala sishangai kukaa na tem m maana hela ya mkwere haina thamani tena
k
 
Aliletewa mgawo wake usiku wa manane...au labda ndio petty cash float yao

Umenikumbusha habari moja niliyoisikia miaka miwili mitatu hivi nyuma wakati EL bado ni PM. Katika mahesabu ya kufunga mwaka katika kampuni ya Caspian ya RA, mahasibu walikuta ziada ya Sh 400 milioni ambazo hawakujua zimeingia vipi katika vitabu vya mahesabu -- maana hazikuwa kutokana na mapato ya kampuni yanayoeleweka.

Wakamuuliza mmiliki, RA, kuhusu hela ile. Pale pale akampigia simu EL na kumuuliza: "Ulipeleka hela pale Sh 400 milioni kule Casspian?" EL akajibu "la hasha."

Baadaye siku iliyofuata EL akakumbuka vizuri kumbe ni hela zake akampigia simu RA: "Hizo hela zililetwa na yule mjamaa? (akamtaja jina) -- ni zangu ndiyo."

Akamwambia aende akazichukuwe kwani zinawachanganya mahasibu wake.
 
Umenikumbusha habari moja niliyoisikia miaka miwili mitatu hivi nyuma wakati EL bado ni PM. Katika mahesabu ya kufunga mwaka katika kampuni ya Caspian ya RA, mahasibu walikuta ziada ya Sh 400 milioni ambazo hawakujua zimeingia vipi katika vitabu vya mahesabu -- maana hazikuwa kutokana na mapato ya kampuni yanayoeleweka.

Wakamuuliza mmiliki, RA, kuhusu hela ile. Pale pale akampigia simu EL na kumuuliza: "Ulipeleka hela pale Sh 400 kule Casspian?" EL akajibu
"la hasha."

Baadaye siku iliyofuata EL akakumbuka vizuri kumbe ni hela zake akampigia simu RA: "Hizo hela zililetwa na yule mjamaa? (akamtaja jina) -- ni zangu ndiyo."

Akamwambia aende akazichukuwe kwani zinawachanganya mahasibu wake.

Haha haha hii ni kali
 
Mi najua yule ni mzee wa RUKSA, inawezekana hao mafundi wameingia ndani wakijua ni RUKSA, wakaingia mpk chumbani RUKSA, wakafungua drooo RUKSA, wakabeba pesa RUKSA. Kama ni walinzi au wafanyakazi pia ni RUKSA, no accusation at all, simple because ni RUKSA........I wonder wanapelekana mahakani!!!!!!!
 
Back
Top Bottom