Exclusive: Wachezaji Wawili Waandamizi wa Mtibwa Sugar FC na Dodoma Jiji FC wanithibitishia kuwa 100% Ligi Kuu ya Tanzania inanuka Rushwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,052
107,535
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunifanya GENTAMYCINE niwe najua Kujichanganya na kila aina ya Watu, Kukubalika na kujenga nao Urafiki hivyo kusaidia Kazi yangu ya 'Kufukunyuwa' Mambo kuwa rahisi.

Wadau wa Soka ( Mpira ) tukiwa tunasema kuwa kuna Rushwa Kubwa inayopelekea Timu Shiriki za Ligi Kuu Tanzania (VPL) Kupanga matokeo huwa tunamaanisha na wala hatutanii ila tunasikitika tu kuona Wahusika TAKUKURU (PCCB) wakiwa hawafanyi Kazi yao.

Leo GENTAMYCINE nimeweza kukutana na Wachezaji Waandamizi wa Timu Mbili zinazoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania (VPL) ya Mtibwa Sugar FC na Dodoma Jiji FC (sitowataja ili Kuwalinda kama nilivyowaahidi) ambapo walinieleza Kaka yao Mimi jinsi Rushwa ilivyokomaa katika Soka la Tanzania.

Bila Kunificha Mchezaji Mwandamizi wa Mtibwa Sugar FC na wa Dodoma Jiji FC wameniambia kuwa Mecbi Mbili Mtibwa Sugar FC ilizocheza na Kushinda zote iliwalazimu Kuhonga na wanaofanikisha hili ni Wachezaji wao Wastaafu ambao hupeleka Pesa kwa Timu Pinzani.

Mchezaji huyo aliniambia kuwa kwa miaka ya nyuma Mtibwa Sugar FC walikuwa ndiyo Wakihongwa na Timu Pinzani baada ya wao kuwa wameshajihakikishia kubaki Ligi Kuu ila kwa sasa baada ya wao kuwa na mwenendo ndiyo Wanahonga ili wabakie Ligi Kuu ya VPL.

Nae Mchezaji Mwandamizi (tena Tegemeo kabisa) wa Dodoma FC amenihakikishia kuwa kabla ya Mechi yao na Ihefu walishapewa Rushwa ili wakubali Kipigo walichokipata na kwamba angeshangaa kama wasingefungwa leo.

Sababu Kubwa ya Klabu ya Dodoma FC kuchukua Rushwa sasa ni kwamba wameshajihakikishia Kubakia katika Ligi Kuu ya Vodacom nchini Tanzania na hawatoacha Pesa zozote ambazo watapewa (watahongwa) na Timu Pinzani.

Kwa Nyakati tofauti kabisa Marafiki zangu hawa ambao ni Wachezaji Waandamizi wa Timu za Mtibwa Sugar FC na Dodoma Jiji FC walinitajia Timu Vinara ( kwa Kipindi Ligi ikielekea Ukingoni) kwa Utoaji na Upokeaji wa Rushwa katika VPL ni Ihefu FC , Mtibwa Sugar FC, Dodoma Jiji FC, Prisons FC, KMC FC, Kagera Sugar, Gwambina FC, Ruvu Shooting, Namungo FC na Mbeya City FC.

Sijaziongelea hapa Timu Mbili Kongwe nchini Simba SC na Yanga SC pamoja ya ile Tajiri kwa Mbagala Azam FC kwakuwa wameniambia hawa Wababe Wakubwa si tu wameshawapa Hongo (Rushwa) bali ndiyo wanaongoza Kuharibu Mpira wa Bongo ( Tanzania ) kwa Kupenda Michezo hii Michafu ya Kuhonga Wachezaji au Waamuzi ili washinde Mechi zao husika.

Haya PCCB nimewatafunia nyie mezeni.
 
Mkuu uko sahihi! Hasa kipindi hiki ligi ikielekea mwishoni, majuzi kati hapa ndugu zangu kule Tanga african sports walicheza Mbeya wakachukua mzigo kwa Kengold ili tu timu fulani isipande ligi kuu, tunayajua mzee coz hata tukisema tunaonekana wakuda.
 
Hivi klabu kongwe kama Yanga ilipata kulalamikiwa kushindwa kulipa mishahara wachezaji wake vipi hao Ihefu, Mbeya City, na Et al. Hali ikoje? Ndio maana wanashawishika kupokea laki laki maisha yaende.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nakuunga mkono 100% tatizo team zetu na wachezaji njaa tupu hawawez kuacha kuchukua laki mbilimbili
Timu za Tanzania (hasa za Ligi Kuu) zikiwezeshwa Kiuchumi kwa Serikali Kuyashawishi Makampuni yazifadhili hizi Timu huku ikiwapa nafuu ya Kodi (kama inavyofanyika Afrika Kusini, Misri na hata nchi nyingi za Ulaya) hili tatizo litaisha na Ligi kuwa Tamu, ya Ushindani na hata Bingwa halali atakuwa anapatikana kuliko ilivyo sasa.

Kuna mwaka nakumbuka Mbao FC ya Mwanza ilipokuja kucheza na Yanga SC hapa Dar es Salaam ilikuwa hoi Kifedha ambapo Yanga SC iliwapokea na Kuwakarimu kwa kila Kitu na Kesho walifungwa Magoli ya Kutosha tu kwa Mkapa.

Pia kuna mwaka nakumbuka Toto Afrika ya Mwanza ilipokuja kucheza na Simba SC hapa Dar es Salaam ilikuwa taabani Kiuchumi ambapo walikarimiwa na Simba SC tena kwa Kulazwa pale Lamada Ilala Boma na Kesho yake walifungwa Goli za kutosha tu kwa Mkapa.

Hivyo tena kuna mwaka nakumbuka Azam FC walikuwa wako mbioni kuchukua Ubingwa wa VPL ila walizidiwa alama chache na Yanga SC ambapo nao waliwakarimu Stand United FC (sasa imeshuka Daraja) kutoka Shinyanga ambapo Wachezaji wao hawakuishia tu Kuhongwa Pesa bali hata baada ya Mechi wote walinunuliwa Simu za Kisasa.

Ligi Kuu ya Tanzania inanuka tu Rushwa.
 
Nikipata mimi hiyo connection yaani hata nisikie walivyopanga matokeo nakuwa tajiri, Tatizo sipati connection.
 
Mkuu uko sahihi! Hasa kipindi hiki ligi ikielekea mwishoni..majuzi kati hapa ndugu zangu kule Tanga african sports walicheza mbeya wakachukua mzigo kwa Kengold ili tu timu fulani isipande ligi kuu..tunayajua mzee coz hata tukisema tunaonekana wakuda.
Tena kama kuna Ligi ambayo Rushwa iko wazi wazi (bila aibu wala Kificho) ni ya FDL ( Ligi Daraja la Kwanza ) na GENTAMYCINE sishangai kuona kuwa Timu Shiriki za Ligi hii ya FDL zenyewe huwa hazitaki kabisa Mechi zao kuwa ' Televised ' na Tv Station yoyoye ile kwakuwa zote huwa zinajua Dhambi ambazo huwa wanazitenda ambazo zikionekana zitaliaibisha Soka letu la Tanzania. Na kinachonisikitisha Upuuzi wote huu TFF ya Rais Wallace Karia wanaujua ila wanauchekea na sasa umeshaota Mzizi.

Huku (Huko) Hela za Mlungula (Rushwa) kuna muda hupewa Kamisaa wa Mechi azishike na ikifika Mapumziko akiona Timu inayotaka Kufungwa inakomaa (inadinda) Kutokufungwa Yeye huwafuata Vyumbani na kuwapa Somo huku akiwakabidhi Mshiko (Fedha) na Timu hiyo ikirejea Uwanjani itafungwa Magoli ya ajabu ajabu tupu huku Wachezaji wake wakijifanya Kulaumiana na hata Kupigana ili Kuwazuga Watazamaji.
 
Japo sina ushahidi lakini naamini kuna ukweli mkubwa sana
Hiki (Hicho) nilichoambiwa na hawa (hao) Wachezaji Waandamizi kabisa wa Mtibwa Sugar FC na Dodoma Jiji FC ni Ushahidi tosha na sijui unataka Ushahidi upi tena.
 
Nakumbuka niliwahi kucheza Chandimu mechi tu ya Maskani Friend Match ambayo hatugombanii chochote niliwahi kula Buku mbili kumuachia jamaa afunge goli ili Demu wake aliyekuwepo uwanjani amshangirie.

Hivyo Rushwa na Muafrika ni chanda na pete mpaka njaa ituondokee.
 
Nakumbuka niliwahi kucheza Chandimu mechi tu ya Maskani Friend Match ambayo hatugombanii chochote niliwahi kula Buku mbili kumuachia jamaa afunge goli ili Demu wake aliyekuwepo uwanjani amshangirie.
Hivyo Rushwa na Muafrika ni chanda na pete mpaka njaa ituondokee.
Oya Mkuu yaani nimecheka mpaka basi.
 
Hiki (Hicho) nilichoambiwa na hawa (hao) Wachezaji Waandamizi kabisa wa Mtibwa Sugar FC na Dodoma Jiji FC ni Ushahidi tosha na sijui unataka Ushahidi upi tena.
Mimi sitaki ushahidi ila naamini kuna ukweli mkubwa tu katika hili ila kusema ushahidi hizo ni mamlaka zichukuwe hatua na haya mambo yasiachwe tu ni hatari katika mipira yetu sasa shughuli kuthibitisha haya hatua kali zichukuliwe kushushwa daraja kabisa lakini ukiwashusha kesho wakubwa nao wakishutumiwa lazima uwashushe kusiwe na kigugumizi maana bongo tunajuwa rahisi kuwahukumu wadogo ikija wakubwa kama hatuoni. Mimi naamini team yoyote inapanga mchezo haifai kuwepo na pia naamini haya yapo sana tu kwetu.
 
Tatizo la ligi yetu kukosa wadhamini wa kutosha, hizi timu zinasumbuliwa na njaa kama zingekuwa vizuri haya yasingetokea.

Ndio maana ligi yetu inatawaliwa na timu tatu tu, kwa mtindo huu hatuwezi kuwa na ubora kwenye ligi, sijui kitu gani kinawashinda TFF kuitafutia wadhamini wa kutosha.
 
Tunaambiwa ligi yetu ina mvuto Afrika Mashariki kwa sababu ya timu tatu tu, nyingine hazijiwezi, ligi haiwezi kuwa na ushindani unaotakiwa kwa mtindo huu, hata hizo Yanga na Azam zimeshindwa kutoa ushindani wa kutosha kwa Simba SC.
 
Kwani unadhani PT na PCCB hawajui tu?
Wakati mwingine jitahidi kurekodi hayo mazungumzo yako na hao wachezaji, ili yatumike kama ushahidi. Ikiwezekana, fanya kama wafanyavyo wale waandishi wa habari za kiuchunguzi.

Ficha sura za wahusika, halafu unawarekodi. Kinyume na hapo, hakuna chombo chochote kitakacho fanyia kazi taarifa za kwenye vijiwe vya kahawa. Labda ziwe ni taarifa za hatari sana kwa usalama wa nchi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom