Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,694
- 40,720
Basi katika kufuatilia mambo mbalimbali kuhusiana na uundwaji wa baraza na hasa kuelewa nini kinaendelea baada ya Ripoti ya Mwakyembe kuna mambo kadhaa ambayo naweza kuwahabarisha kwa uhakika zaidi.
a. Baraza la Mawaziri litakuwa dogo huku nafasi/watu karibu 21 wakiwa nje (halitazidi wizara 25).
b. Rais anatumia hekima ya ajabu katika panga pangua ya kuliunda upya, huku mwelekeo wake ukiwa ni "kurejesha imani ya wananchi kwa serikali yao). Kwa hiyo kinachoundwa ni kama "dream team". Lengo lake ni kuwa ndani ya muda uliobakia baraza hili lifanye more than expected. Wakati Mkapa aliunda "kikosi cha miamvuli" JK anakuja na SEALs (Sea, Air and Land). Yaani Makomandoo wa anga zote!
c. Suala la kushirikisha vyama vya upinzani vinafanya hali iwe ngumu. Chama kimoja kimekataza wabunge wake kuingia kwenye Baraza hilo kwa madai ya kutofautiana kisera na CCM. Chama hicho kinadai kuwa kwa vile serikali iliyoko madarakani inatekeleza sera na ilani ya CCM haiwezekani wabunge wake waingie serikalini kwenda kutekeleza sera na ilani hiyo.
Hata hivyo, chama kingine cha upinzani inaonekana kimekubali angalau Unaibu.
d. Timu ya Lowassa nayo bado imejipanga kujibu mashambulizi ya Kamati ya Mwakyembe. Hadi hivi sasa madai yanayoendelea kunong'onezwa pembeni ni kuwa siyo Msabaha tu aliyetolewa ngasubilo bali Lowassa wenyewe.
Kutoka ndani sana ya mafaili ya serikali kuna barua ambayo inaonesha kuwa EL alitaka kusitisha mkataba wa RDC na aliandika barua kwa mkuu wake kuonesha nia hiyo, hata hivyo alikataliwa na akaamua kuendelea nao. Uwepo wa barua hiyo kama ni kweli au la ni suala la mjadala.
Hata hivyo hilo linakumbusha "barua ya Meghji" ambaye baada ya kugundua tatizo kule EPA siyo tu aligeuka kinyume nyume bali pia aliamuru uchunguzi ufanyike ambao matokeo yake tunayakumbuka.
Hivyo, utetezi huu wa Lowassa unaweza kuwa vigumu kwa Lowassa kwamba baada ya kugundua tatizo la RDC ni hatua gani za kiuchunguzi alizochukua ili kuonesha kuwa kampuni hii haikuwa na ukweli wowote? Kama uchunguzi wake ungeonesha kuwa kampuni hii haikuwepo basi mkataba usingekuwepo na serikali isingepata adhabu yoyote ile!
Wachunguzi wengine wanamtonya wenu mtiifu, kuwa kama EL aligundua kuwa kuna tatizo na ushauri wake kwa mkuu haukufuata na hivyo utaliingiza taifa kwenye matatizo kwanini hakujiuzulu wakati ule? EL alikuwa na uwezo wa kujiuzulu baada ya kukataliwa mapendekezo yake kuhusu RDC (assuming yalikuwepo). Kitendo cha yeye kukubali na kuendelea kuna negate jitihada zote ambazo alizifanya kimya kimya.
e. Kuna dalili kuwa baadhi ya watu walioatajwa kwenye ripoti kuwa walizungumza "nje ya kiapo" kuwa walimuimplicate Waziri Mkuu wameanza kukana hata kukumbuka kuota maneno hayo. Balozi Kazaura ameandika barua leo jioni kwa Katibu wa Bunge akitaka ripoti ya Mwakyembe ifanyiwe masahihisho akikana categorically kuwa hakusema jambo lolote ndani au nje ya kiapo kumhusisha Lowasa na Richmond. Wengine nao wanatarajia kufanya hivyo.
f. Majina ya Baraza la Mawaziri bado yanaendelea kufanywa siri hadi yatakapotangazwa hewani, na kuna dalili endapo jina lolote linavuja basi jina hilo linatolewa. Hivyo, hata sisi wengine tulio na bahati ya kuwa nzi kwenye kuta zao tunashindwa kupenyeza lolote tusije kukesha tena!! So, hata tungetaka kuwanong'oneza hatuwezi!!
Wote tusubiri TVs!!