Exclusive: Ripoti ya Uchunguzi wa Vifo Tarime - Marehemu walipigwa mgongoni wakikimbia

Dah! Inatia huruma sana watu wanadai haki zao wanapigwa risasi na kuuawa bila sababu. Ni aibu kwa JK kutembea kifua mbele akidai anatoka tanzania. Shame on JK R.I.P. Wapiganaji. Asante Nyakarungu kwa taarifa.
 
Damu iliyomwagiga iwe msingi wa ukombozi na haki,hakika kila aliyeshiriki kuua raia,kumwaga damu isiyo na hatia,atalipwa sawa sawa na matendo yake
saa ya ukombozi ni sasa...
 
'Walipigwa kwa nyuma wakiwa wanakimbia' hiyo ni conclusion ya uchungu sana. Kwamba wananchi wametimuliwa kwenye mali yo na wanapigwa risasi wakiwa tayari wame-give up. Kuna siku watasimama. Poleni sana wafiwa. Damu yenu sio bure. Ukombozi unakuja
 
HABARI ZENU WANAJAMII!!!!!!!!!?

Nafahamu nyote mwajua tukio la Tarime, la wananchi kuuwawa na jeshi la polisi huko migodini Nyamongo Wilayani Tarime,tarehe juma lililopita.

Wafiwa wallitaka kujua undani wa mauaji ya ndugu zao, ili waweze kufuata njia za kisheria za kudai haki yao ya kisheria.

Ililazimika uchunguzi wa kitaalam ufanyike ili ukweli ujulikane...
Uchunguzi huu ulifanywa jana na mtaalam wa uchunguzi wa aina hii (Post Motum) ya kitaalam, Dr Makata kutoka wizara ya afya kitengo cha dharura matukio tata.
Kwa upande wa wafiwa waliwakilishwa na Grayson Nyakarungu, aliyepewa imani na chama pia kuhakikisha ukweli ndio unaletwa hadharani.
Pia jeshi la polisi na Hospitali ya wilaya ya Tarime walikuwa na wawakilishi wao.
Tuliifanyia miili mnne kati ya mitano, ya watu walio uwawa, kwani mwili mmoja ulishazikwa kwa kuibiwa na polisi.

IFUATAYO NI TAARIFA HALISI TULIYOTOKA NAYO BAADA YA UCHUNGUZI WA WETU, KWA KULINDA NA KUHESHIMU UADILIFU WA TAALUMA YETU YA KIAFYA.

KIAPO NILICHOAPA HUKO CHUONI (MEDICAL ETHICS)
1. Kile kinachoonekana katika vipimo/uchunguzi, ndicho kinachotakiwa kuwekwa wazi kwa muhusika.
2. Sitakeuka wala kughiribu utu wa mtu kwa sababu zozote zile.

Hizo ni chache tu kati ya Medical Ethics nyingi, ambazo niliapa kuzilinda na kuzisimamia.

POST MOTUM ROOM
Tulianza kazi hii saa 10:25 A.M hadi saa 16:57 P.M baada ya wafiwa kuitambua miili ya ndugu zao.

1. Mwili wa Emmanueli Magige
P.M No 1-5-11
T.G.H
Entrance site: Left illiac cleft (upande wa kushoto wa juu ya nyonga)
Wound size: 0.5 cm diameter the wound was round.
Exit site: Lumber region back (juu ya kiuno kidogo karibu na uti wa mgongo)
Wound size: 2.5 cm diameter

Positive findings;-
-Blood vessels/Nerves and sorounding muscles were destroyed.
-The clavicle bone was destroyed and blood clots was seen, ( mfupa mkuu wa kiuno na nyonga uliharibiwa na damu nyingi ilivuja na imeonekana imeganda humo)

But beneath the exit site, there was a cut wound, 2.5 cm diameter.
Lakini kulikuwa na alama ya jeraha kubwa linaloonyesha alama ya kuwa kitu chenye ncha kali kilichoma, na hii ilileta hisia tofauti, polisi walihisi kuwa aliangukia jiwe au kijiti kilichomchoma, kwa hili tulibishana na tukaamua hakuna jibu la nini kilichoma, ila mimi nilihisi na kusimamia kuwa alichomwa na singe ya bunduki, na ndipo niliomba nguo zake zitafutwe ili tuzichunguze na tubaini ukweli, hata hivyo hazikupatikana.

2. Mwili wa Chacha Ngoka
P.M No. 2-5-11
T.G.H

Entrance site: Right side of the body back 16 cm from illiac (usawa wa bega chini na juu ya kiuno, nyuma ya mwili.
Wound size: 0.3 cm diameter
Exit site: In 5th intercoastal muscle right side, 2cm from the nipple.
Wound size: 5cm diameter

Positive findings
Major blood vessels were destroyed
Midle and right lobe of liver were destroyed led to rasaration
In the Trachea, blood clot was seen.

3. Mwili wa Chawali Boke.
P.M No. 3-5-11.
T.G. H
Entrance site: Occipital bone 8cm from the Pinna, (Kisogoni sm 8 kutoka sikio la kushoto)
Wound size: 0.2 cm diameter
Exit site: In parietal bone ( kwenye paji la uso pembeni kidogo)
Wound size: 5cm diameter
Positive findings;-
The brain and inner part of the head was destucted, blood clotts was seen, this was due to blood aspiration.

4. Mwili wa Mwikwabe Marwa Mwita
P.M No. 4-5-11
T.G.H
Entrance site: Left illiac cleft (upande wa kushoto juu ya nyonga)
Wound size: 3.5 cm diameter
Exit site: It was not pass through, it remained intact.
Wound size: None

Positive findings;-
There was worse destruction of;-
-Femoral artery
-Femoral vein
-Sorrounding muscles
- Fructure of illiac bone ( mfupa wa nyonga na uzazi)
- Piece of lead was seen lying deeply inpsoas muscle, sorrounded by bone fragments

Msimamo wangu kimaadili na na kibinadamu;-
1. Polisi walikusudia kuua na sio kudhibiti watu waliowaita wavamizi, kwani kwa mjibu wa force law, hawakutakiwa kupiga risasi sehemu yoyote tofauti na miguuni.
2. Polisi waliwapiga risasi watu waliokuwa wakikimbia kutoka eneo hilo, kwani risasi zote zimepenya kwa upande wa nyuma wa mwili na zikatokea upande wa mbele wa mwili.
HIVYO wananchi hawa hawakupambana na polisi, bali walipigwa risasi wakiwa wanakimbia, ndio sababu ya risasi zote kuingia sehemu za nyuma za miili yao.
Mungu watazame waja wako na uwalinde na yote aliyoyaandaa SHETANI.

MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI AMINA, NITAKUWA SHAHIDI MWEMA NA MSEMA UKWEI KWA KUUENZI UTU.

Hakuna mtu anaeshangilia mwenzie kufa lakini watu watajadili kifo chake,umesema unahisi kuwa alichomwa na singe na wakati huohuo unasema hakuna aliyepambana na polisi na kwamba walipigwa wakiwa mbali wanakimbia je hiyo singe unayoihisi ilifyatuka kama risasi? halafu haujawaeleza wana JF hilo tundu la "singe" lilikuwa upande gani wa mwili? na je mbona haujaonesha wasiwasi wako juu ya daktari aliyefanya hiyo post motum?kwani yeye ndio final say wa hiyo post motum na hakuona hiyo "singe" uliyoiona wewe.Palipo kweli ongea kweli na pale ambapo hapana ukweli usiongee.
 
Speaker,
kinachofuata nimetoa taarifa kwa vyombo vya habari na baada ya mwanasheria kuipitia, kitakachofuata ni kesi na mimi nitakuwa SHAHIDI.

safi sana,sina shaka kwamba sio tarime peke yake wanapo
teseka watu wanao kaa karibu na migodini,..
naamini na migodi mingine ni hivi hivi,ila nawaombeni hili mlikomalie
ili uwe mwanzo wa wanchi wanao ishi karibu na migodi kuishi kama binadamu
 
......Ni aibu kama imefikia mahali POLISI wamefikia mahali wanauwa rais ambao tayari .....walikuwa wanakimbia....,mabomu ya machozi tayari yalitosha kuwakimbiza wananchi ...,
Walikuwa na option ya kutumia risasi za mpira kama ilikuwa lazima hawakutumia......walikuwa na option ya kuwapiga risasi miguuni ...wao wakawapiga za kisogo na nyonga....
Walikuwa na fursa ya kuwaacha wazikwe kwa heshima ...wao wakachukua maiti zao usiku na kwenda kuzitelekeza barabarani..........................................................................
Alafu mtawalaumu CHADEMA wananchi wakiwachuki? nCHI ikichafuka mtawalaumu CHADEMA?
Ni wazi kuwa adui wa serikali ya kikwete amejificha ndani ya wasaidizi wake waaminifu...au kama ni maagizo yake basi ..ajilaumu yeye mwenyewe......
 
HABARI ZENU WANAJAMII!!!!!!!!!?

Nafahamu nyote mwajua tukio la Tarime, la wananchi kuuwawa na jeshi la polisi huko migodini Nyamongo Wilayani Tarime,tarehe juma lililopita.

Wafiwa wallitaka kujua undani wa mauaji ya ndugu zao, ili waweze kufuata njia za kisheria za kudai haki yao ya kisheria.

Ililazimika uchunguzi wa kitaalam ufanyike ili ukweli ujulikane...
Uchunguzi huu ulifanywa jana na mtaalam wa uchunguzi wa aina hii (Post Motum) ya kitaalam, Dr Makata kutoka wizara ya afya kitengo cha dharura matukio tata.
Kwa upande wa wafiwa waliwakilishwa na Grayson Nyakarungu, aliyepewa imani na chama pia kuhakikisha ukweli ndio unaletwa hadharani.
Pia jeshi la polisi na Hospitali ya wilaya ya Tarime walikuwa na wawakilishi wao.
Tuliifanyia miili mnne kati ya mitano, ya watu walio uwawa, kwani mwili mmoja ulishazikwa kwa kuibiwa na polisi.

IFUATAYO NI TAARIFA HALISI TULIYOTOKA NAYO BAADA YA UCHUNGUZI WA WETU, KWA KULINDA NA KUHESHIMU UADILIFU WA TAALUMA YETU YA KIAFYA.

KIAPO NILICHOAPA HUKO CHUONI (MEDICAL ETHICS)
1. Kile kinachoonekana katika vipimo/uchunguzi, ndicho kinachotakiwa kuwekwa wazi kwa muhusika.
2. Sitakeuka wala kughiribu utu wa mtu kwa sababu zozote zile.

Hizo ni chache tu kati ya Medical Ethics nyingi, ambazo niliapa kuzilinda na kuzisimamia.

POST MOTUM ROOM
Tulianza kazi hii saa 10:25 A.M hadi saa 16:57 P.M baada ya wafiwa kuitambua miili ya ndugu zao.

1. Mwili wa Emmanueli Magige
P.M No 1-5-11
T.G.H
Entrance site: Left illiac cleft (upande wa kushoto wa juu ya nyonga)
Wound size: 0.5 cm diameter the wound was round.
Exit site: Lumber region back (juu ya kiuno kidogo karibu na uti wa mgongo)
Wound size: 2.5 cm diameter

Positive findings;-
-Blood vessels/Nerves and sorounding muscles were destroyed.
-The clavicle bone was destroyed and blood clots was seen, ( mfupa mkuu wa kiuno na nyonga uliharibiwa na damu nyingi ilivuja na imeonekana imeganda humo)

But beneath the exit site, there was a cut wound, 2.5 cm diameter.
Lakini kulikuwa na alama ya jeraha kubwa linaloonyesha alama ya kuwa kitu chenye ncha kali kilichoma, na hii ilileta hisia tofauti, polisi walihisi kuwa aliangukia jiwe au kijiti kilichomchoma, kwa hili tulibishana na tukaamua hakuna jibu la nini kilichoma, ila mimi nilihisi na kusimamia kuwa alichomwa na singe ya bunduki, na ndipo niliomba nguo zake zitafutwe ili tuzichunguze na tubaini ukweli, hata hivyo hazikupatikana.

2. Mwili wa Chacha Ngoka
P.M No. 2-5-11
T.G.H

Entrance site: Right side of the body back 16 cm from illiac (usawa wa bega chini na juu ya kiuno, nyuma ya mwili.
Wound size: 0.3 cm diameter
Exit site: In 5th intercoastal muscle right side, 2cm from the nipple.
Wound size: 5cm diameter

Positive findings
Major blood vessels were destroyed
Midle and right lobe of liver were destroyed led to rasaration
In the Trachea, blood clot was seen.

3. Mwili wa Chawali Boke.
P.M No. 3-5-11.
T.G. H
Entrance site: Occipital bone 8cm from the Pinna, (Kisogoni sm 8 kutoka sikio la kushoto)
Wound size: 0.2 cm diameter
Exit site: In parietal bone ( kwenye paji la uso pembeni kidogo)
Wound size: 5cm diameter
Positive findings;-
The brain and inner part of the head was destucted, blood clotts was seen, this was due to blood aspiration.

4. Mwili wa Mwikwabe Marwa Mwita
P.M No. 4-5-11
T.G.H
Entrance site: Left illiac cleft (upande wa kushoto juu ya nyonga)
Wound size: 3.5 cm diameter
Exit site: It was not pass through, it remained intact.
Wound size: None

Positive findings;-
There was worse destruction of;-
-Femoral artery
-Femoral vein
-Sorrounding muscles
- Fructure of illiac bone ( mfupa wa nyonga na uzazi)
- Piece of lead was seen lying deeply inpsoas muscle, sorrounded by bone fragments

Msimamo wangu kimaadili na na kibinadamu;-
1. Polisi walikusudia kuua na sio kudhibiti watu waliowaita wavamizi, kwani kwa mjibu wa force law, hawakutakiwa kupiga risasi sehemu yoyote tofauti na miguuni.
2. Polisi waliwapiga risasi watu waliokuwa wakikimbia kutoka eneo hilo, kwani risasi zote zimepenya kwa upande wa nyuma wa mwili na zikatokea upande wa mbele wa mwili.
HIVYO wananchi hawa hawakupambana na polisi, bali walipigwa risasi wakiwa wanakimbia, ndio sababu ya risasi zote kuingia sehemu za nyuma za miili yao.
Mungu watazame waja wako na uwalinde na yote aliyoyaandaa SHETANI.

MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI AMINA, NITAKUWA SHAHIDI MWEMA NA MSEMA UKWEI KWA KUUENZI UTU.
Mkuu ubarikiwe sana,nilikwisha sema safari hii lazima serikali ipate somo la kihistoria.
 
Hakuna mtu anaeshangilia mwenzie kufa lakini watu watajadili kifo chake,umesema unahisi kuwa alichomwa na singe na wakati huohuo unasema hakuna aliyepambana na polisi na kwamba walipigwa wakiwa mbali wanakimbia je hiyo singe unayoihisi ilifyatuka kama risasi? halafu haujawaeleza wana JF hilo tundu la "singe" lilikuwa upande gani wa mwili? na je mbona haujaonesha wasiwasi wako juu ya daktari aliyefanya hiyo post motum?kwani yeye ndio final say wa hiyo post motum na hakuona hiyo "singe" uliyoiona wewe.Palipo kweli ongea kweli na pale ambapo hapana ukweli usiongee.

Wewe umerudi lini? Subiri mahakama na wewe nenda kateteee wauaji
 
KWA KUWA MAMBO HAYA YAMEKUWEPO KWA SIKU NYINGI NI VIZURI SASA WASIWASINGIZIE CDM KUWA WAMECHOCHEA WANCHI KUINGIA MGODINI(kama kweli waliingia) MAANA MATUKIO YA AINA HII YAMEKUWEPO NA YANAENDELEA WALA HAYAJAISHA
 
Hakuna mtu anaeshangilia mwenzie kufa lakini watu watajadili kifo chake,umesema unahisi kuwa alichomwa na singe na wakati huohuo unasema hakuna aliyepambana na polisi na kwamba walipigwa wakiwa mbali wanakimbia je hiyo singe unayoihisi ilifyatuka kama risasi? halafu haujawaeleza wana JF hilo tundu la "singe" lilikuwa upande gani wa mwili? na je mbona haujaonesha wasiwasi wako juu ya daktari aliyefanya hiyo post motum?kwani yeye ndio final say wa hiyo post motum na hakuona hiyo "singe" uliyoiona wewe.Palipo kweli ongea kweli na pale ambapo hapana ukweli usiongee.

ziada,

singe inashikwa mkononi, mtu anapopigwa risasi anaanguka, polisi mwenye singe/njaa/hana mshahara/ametukanwa na anaambiwa aue, akifanikiwa kuachia risasi, kwa roho ngumu yake hatashindwa kumfuata aliyeanguka na kumchoma singe....
Nilochoandika ndiyo taarifa, ambayo hata yeye mtaalamu anaikubali na alisema mengine ni ya watalaamu wa sheria na hatukuwa tunabishana pale.
kuhusu alama ya amabayo sio ya risasi...hujasoma vizuri au tumia dictionary ya medical utaelewa nimeandika " beneath the exit site...." a cut wound
 
kama serikali imeshindwa kulitawala jimbo la Tarime basi waliachie uhuru liwe nchi huru na si kuleta mahafa ya jamii ya tarime.
 
Hii ni sawa na 'cold blood murder' watu wanakimbia unawapiga risasi migongoni na ndiyo maana wengine wamepigwa risasi za juu ya nyonga au begani. POLISI hawa hawana tofauti na wale POLISI wa utawala wa Makaburu waliofanya mauji ya vijana wa Sharperville kule Soweto Afrika ya Kusini wakati wa vugugu la kudai ukombozi na haki ya kweli.

Hii haikubaliki hata kidogo na pia serikali ya CCM ndiyo inabeba lawama zote kwa kupuuza 'utu wa watu' wanaopigania kupata haki ya kiuchumi toka maeneo yao ya asili ambayo imeporwa kwa mikataba feki ya kigandamizi kati ya utawala wa CCM na wawekezaji toka nje.
 
Good job, haya ndo hawakutaka yajulikane sasa yamejulikana tena kwa umma. Tuone ubabe wao katika hii kesi sasa.
Serikali inayotenda maovu na kutaka kuyaficha uvunguni tena kwa gharama yoyote haitufai na haina faida yoyote kwa watu wake.

Kwa swala hili na lile la Arusha ni fedheha kubwa kwa serikali iliyochaguliwa na inategemea tena 2015 kurudi kuomba kura. Sidhani kama kuna mtanzania aliyetayari kupigia kura magamba haya tena!

Huwa ninasema kila wakati mtu anayekutendea mabaya siku zote isipokuwa tu wakati wa uchaguzi basi hakufai kuwa kiongozi wako.

Serikali hii ukweli haina nia nzuri mtanzania wa kawaida vitu tunavyopata kutokana na serikali yeti ni kama ambavyo mbwa koko hutupiwa mabaki ya mifupa na ugali. Katika keki ya taifa kama asilimia 80 hugawana wenyewe wachahce na walalahoi ambaao ni wengi ndo hugawana ile 20 perc.
 
Lakini mm nashindwa kuelewa kwa nn wa2 mnalifanya tukio la Tarime kua la kisiasa?
Na kwa nn mnafanya au mnaforce polisi kua chombo cha siasa?
kwa maan mm ninavyo jua chombo chochote cha usalama kina Protocol zake ambazo hua zinafatwa.na ndio hua zinaongoza hivyo vyombo na kwa bahati mbaya au nzuri wakivunja zile protocol zao vipo vyombo ambavyo vipo wazi muda wote kusikiliza malalamiko ya mtu ambavyo ni kama mahakama.
Nawaomba tusihusishe tukio la Tarime na mambo ya siasa tafadhar.

Asanten
 
Asante Nyakarungu
RIP wapiganaji,hii ni damu nyingine inamwagwa migodini,hatujasahau,bulyanhulu na kwingine,damu hii haikumwagika bure,lkn hatuwezi kukubali hali hii iendelee,tutapigana mpaka haki ipatikane!
 
Back
Top Bottom