Exclusive Report ya GENTAMYCINE juu ya kilichotokea majuzi nchini Zimbabwe

Naona mambo bado..
Eti ataongoza mkutano Mkuu wa ZANU-PF december wakati yeye kavuliwa uenyekiti sasa sijui atauongoza kama nani...
Si ajabu kesho wakamwondoa kwa nguvu
 
Wale ni wanachama tu wa ZANU PF walioko jeshini na watiifu kwa Mugabe , hakuna mapinduzi pale, jeshi lichukue madaraka halafu wahangaike kumtoa mwenyekiti wa chama kinawahusu nini mambo ya chama chake?
Hata Mugabe akiondoka sidhani kama kutakua na mabadiliko ya maana ya kiuchumi na kiutwala Zimbabwe maaana ni wale wale waliokua kwenye circle yake kwa hiyo miaka 37 yote.
 
Utafiti mzuri na kuna ukweli ndani yake. Kwa upana zaidi, nenda kacheki 'Gang of Four' ya China iliyomuhisisha mke wa Mao. Interestingly enough, Grace Mugabe naye alikuwa na group lake lililojulikana kama 'Generation 40' ambalo jeshi limewaita 'wahuni wanaomzunguka Raisi wanaosababisha matatizo ya kiuchumi na kijamii'.

Same script imechezwa na watu bado wameingia kingi.
 
Wewe jamaa huwa ni tapeli flani hivi unayejifanya kuwa mjuaji sana

Hakuna na hakukuwa na haja yoyote ya kusababisha panic yote hiyo kwa nchi kisa Grace Mugabe...eti mugabe ndiye alipanga

acha kudanganya watu hapa
kweli huyu gentamyciline siyo tapeli tu. Ni chizi huyu.
 
Sasa siyo siri tena kwamba Afrika nzima Simba wa Nyika amebaki mmoja tu nae ni Rais wa sasa wa Zimbabwe Mzee Robert Mugabe na huenda siku ambayo Mwenyezi Mungu ataamua kumchukua huyu Mzee basi bara zima la Afrika litakuwa limepoteza ' Lulu / Thamani ' ya kweli ya Kiongozi madhubuti.

Siku ya Jumanne wiki hii dunia nzima ilipatwa na mshtuko mkubwa hasa baada ya kutokea sintofahamu huko nchini Zimbabwe baada ya pale Rais wa nchi hiyo Mzee Mugabe alipozingirwa katika makazi yake ya Kifahari ( Palace ) jijini Harare huku Jeshi likichukua hatua za kuimarisha Ulinzi mkali nchini humo kwa msaada ya Magari ya Kijeshi.

Ufuatao ni mtiririko kama siyo mserereko mzima wa Ripoti Maalum ya GENTAMYCINE juu ya chote kilichotokea huko nchini Zimbabwe ambapo nitaelezea ilivyokuwa, ilivyo na mwisho wake wote utakuwaje ambapo mwishoni wote tutakubaliana kwamba Rais Mzee Mugabe kweli ni Mzee ila bado akili na mbinu zake ni za hali ya juu.

ILIKUWAJE?

Miezi ya hivi karibuni inaelezwa kwamba Rais Robert Mugabe kwa Siri kabisa aliwaita Watu wake wa karibu aliyekuwa Makamu wake wa Rais Bwana Emerson Mnangagwa na Mkuu wa Majeshi wa Zimbabwe Jenerali Chiwenga na kuwaeleza mambo yake kadhaa ya Kifamilia ambayo yalikuwa yakimtatiza kwa muda mrefu.

Katika Kikao chake hicho na hawa Watu wake wa karibu Rais Mugabe alifunguka zaidi Kwao kwa kuwaambia kwamba mara kwa mara amekuwa katika mvutano na Mkewe Grace na kwamba tokea mwaka 2008 alipanga Kuachana na Urais wa Zimbabwe lakini Mkewe alikuwa hataki na akimshinikiza kuwa asitoke na mpaka hata kuutishia Uhai wake kitu ambacho kwakweli kilimkera sana Yeye ( Rais Mugabe )

Hivyo mara baada ya Rais Mugabe kufunguka hivyo kwa hawa Watu wake wa karibu huku akiwataka wamsaidie sana kwakuwa amevumilia karaha za Mkewe Grace kiasi kwamba hadi amejuta kuwa nae kwakuwa amemsababishia Uadui mkubwa dhidi yake kutoka kwa Wazimbabwe hasa kutokana na maisha ya Kifahari aliyokuwa akiishi Grace.

MUITIKIO WA MAKAMU WA RAIS NA MKUU WA MAJESHI CHIWENGA KWA RAIS MUGABE

Mara baada ya Rais Mugabe kuwaambia yote hayo hawa Watu wake wa karibu Makamu wa Rais Emerson Mnangagwa na Mkuu wa Majeshi Chiwenga na wao pia wakamuambia kwamba kwakuwa amewaambia ukweli wote juu ya kinachomsibu basi awape muda ili wawili hao wakae chini na waandae mkakati maalum ambao ungewahusisha Watu wa Idara za Kijasusi za Zimbabwe na Jeshi la nchini Zimbabwe.

HALI IKAWAJE?

Baada ya wawili hawa Makamu wa Rais na Mkuu wa Majeshi kumaliza kupanga mikakati yao walirudi kwa Rais Mugabe na kumpa mrejesho wao na mkakati kabambe waliouopanga ambao wao waliamini kwamba ungefanya Kazi kwani umeshirikisha Watu wengi na hadi baadhi ya Viongozi Waandamizi wa Chama chake cha ZANU-PF.

Walipomaliza kumpa mkakati wote Rais Mugabe ( ambao mkewe Grace katika mambo yote haya hakushirikishwa ) ndipo Rais Mugabe akaanza kuutekeleza ambapo aliunda Timu maalum ya kutengeneza fitna ndani ya Serikali yake na Chama chake cha ZANU-PF ili mradi tu akija kufanya maamuzi fulani basi yaendane sambamba na yale maelekezo yote aliyopewa na Makamu wake wa Urais na Mkuu wake wa Majeshi.

Pasipo Wazimbabwe wote kujua kwamba Rais Mugabe ni zaidi ya wamjuavyo na kwamba siku zote hata kama Ng'ombe akiwa Mzee ila hazeeki maini Mzee huyu alipohakikishiwa na Timu yake ya Fitna kuwa kila kitu sasa kipo tayari huku Makamu wa Urais na Mkuu wa Majeshi wakijua kila kitu Rais Mugabe alijifanya kumtafutia zengwe Makamu wake Urais kisha akamfuta Kazi na mara baada ya kumfuta Kazi hapo hapo tena akaitisha Mkutano maalum na Wanachama wa ZANU-PF na kumteua Mkewe kuwa Makamu wa Urais kuchukuwa nafasi ya Emerson Mnangagwa.

KILICHOFUATIA

Mara baada ya Rais Mugabe kuyafanya yote hayo kama ambavyo alielekezwa na akina Emerson na Chiwenga Rais Mugabe kwa Siri tena aliwatonya hawa hawa Watu wake kwamba Mkewe Grace ni mwoga sana na kwamba hapendi Umasikini na ni mfujaji mkubwa wa Mali za Wazimbawe na kwamba Yeye binafsi ameshamchoka na alichokuwa akikitaka ni Yeye na Grace kutenganishwa kwani kuna Msiri wake ndani ya Familia yake alishawahi kumwambia kwamba aliwahi kuambiwa na Grace mwenyewe kwamba hampendi Rais Mugabe ila yuko nae Kwanza ili kuhakikisha anapata Utajiri na muda ukifika ataachana nae na Yeye kuishi maisha yake na Wanae.

MPANGO MKUBWA ULIOPANGWA NA UKAFANIKIWA NI UPI?

Kila kitu kilipohakikishwa kwamba kipo tayari akina Makamu wa Rais Emerson na Mkuu wa Majeshi Jenerali Chiwenga walimwambia Rais Mugabe kwamba sasa atulie tuli kwani wanaenda kumaliza mzizi wa fitna ili lengo lake la kutaka Kupumzika Siasa na kuachana na Mkewe Grace.

Mara baada ya kuhakikishiwa kwamba yote haya yakifanyika hali ya Usalama wa Wanazimbabwe na nchi ya Zimbabwe utakuwa salama tu na hakuna jambo baya litakolotokea Rais Mugabe aliwaruhus wawili hawa kutekeleza sasa rasmi mkakati wao huku Yeye akijifanya kama hajui kinachoendelea.

Ndipo asubuhi ya Jumanne wiki hii ya tarehe 14 November, 2017 Wazimbabwe wengi wakiwa hawajui kinachoendelea Jeshi la Zimbabwe likaamua kujitokeza hadharani huku likiwa na Vifaa vyote vya Kivita na haraka haraka kushika / kudhibiti maeneo maalum na kwenda pia kumzingira Rais Mugabe katika ' Palace ' yake huku Mkewe Grace nae akiwemo.

MTEGO ALIOTEGWA GRACE MUGABE BILA YEYE KUUJUA NA AKAUKANYAGA NI HUU

Mara baada ya Jeshi la Zimbabwe kumzuia Rais Mugabe nyumbani Kwake katika Kasri lake ( Palace ) alipandikizwa Mwanamke mmoja ambaye inasemekana alikuwa ni mwana Usalama wa Taifa wa Zimbabwe ambapo alihakikisha anamtisha na kumshawishi Mkewe Rais Mugabe Grace kwamba atoroke kwani Mumewe anaenda Kuuwawa na Yeye atakamatwa, Kushtakiwa na Kufilisiwa Mali zake zote.

Grace Mugabe ( Mkewe Rais Mugabe ) baada ya Yeye kuambiwa haya yote pasipo kujua kwamba yote hayo anayoambiwa yalishapangwa mapema na hata Mumewe Rais Mugabe pamoja na Viongozi wengine Waandamizi hasa wa Usalama wanajua akakubaliana na ule ushauri wa yule Dada Jasusi na usiku akatoroka Jijini Harare kwa msaada wa yule Dada na kuelekea nchi jirani ya Namibia kusikilizia japo taarifa za ndani zaidi zinasema kwamba huenda Grace Mugabe akawa amekimbilia Botswana au Dubai au Malaysia ambako ndiko kuna Mali nyingi za Familia ya Mugabe na ambazo nyingi zina umiliki wake Yeye ( Grace )

MAFANIKIO YA MKAKATI WA SIRI

Mara baada ya kuhakikisha kwamba Grace Mugabe ameshatoroka Jijini Harare yule Dada Jasusi alirudisha mrejesho kwa Mabosi zake Makamu wa Rais Emerson, Mkuu wa Majeshi Jenerali Chiwenga na Wakuu wa Usalama ndipo lengo lao likatimia 100% ambapo ili kuwazuga Watu wengi na kuwahadaa Wazungu ambao muda wote wa hili tukio la Jumanne walikuwa wakifurahia Jeshi likajifanya kuchukua hatamu lakini kumbe chini kwa chini mikakati mingine ikipangwa huku Rais Mugabe nae akishirikishwa moja kwa moja.

MAKUBALIANO YA AWALI

Kutokana na hali yote ilivyokuwa na mkakati kufanikiwa kwa 100% Rais Mugabe aliwaambia akina Emerson na Chiwenga kwamba kiukweli Yeye sasa amechoka Kuongoza hivyo alichokuwa akitaka ni kwamba kwa siku hizi mbili tatu Jeshi la Zimbabwe chini ya Jenerali Chiwenga lishike hatamu lakini pia watafutwe Viongozi Waandamizi wa Kamati Kuu ya Chama cha ZANU-PF ili wataarifiwe kwamba Mzee Mugabe anataka Kupumzika hivyo ameamua kumuachia Uongozi Makamu wake yule yule ambaye mwanzo alimfukuza ( kimkakati zaidi )

Yafuatayo ni MAKUBALIANO MAALUM yaliyofanyika katika Vikao vya Jeshi tokea jana, juzi na jana na Rais Mugabe:

  1. Rais Mugabe akijiuzuru hatoshtakiwa
  2. Rais Mugabe akijiuzuru ataendelea Kulipwa Pensheni yake
  3. Rais Mugabe akijiuzuru Mali zake hazitoguswa wala kutaifishwa
  4. Rais Mugabe akijiuzuru atatangazwa kuwa Baba wa Taifa na kupewa Heshima hadi Mauti
  5. Rais Mugabe atakubali rasmi aliyekuwa Makamu wake Emerson Mnangagwa amrithi
  6. Rais Mugabe atawashawishi Wajumbe wote wa ZANU-PF wakubali kujiuzuru Kwake
  7. Rais Mugabe atahakikishiwa Ulinzi wake na Mali zake zote mpaka atakapokufa
KITENDO CHA KUONEKANA KATIKA MAHAFALI KINAASHIRIA NINI?

Kitendo cha Rais Mugabe kuonekana leo katika Mahafali katika Chuo Kikuu jijini Harare kilikuwa ni cha Kimkakati zaidi na hasa katika Kuimarisha Umoja, Amani na Utulivu kwa wana Zimbabwe na kuonesha kwamba Zimbabwe iko salama kitu ambacho hakijafurahiwa kabisa na nchi za Ulaya hasa Marekani na Uingereza ambao walishaanza kushangilia Kitendo kilichotokea na haraka sana wakamuibua ' Kibaraka ' wao wa muda mrefu aliyekuwa Kiongozi wa Upinzani Bwana Morgan Tshivangirai aanze ' chokochoko ' zake lakini akagundua kwamba nchi bado iko salama na asingefanikiwa.

HITIMISHO

Kinachofanyika sasa ni mazungumzo ya ndani kwa ndani katika Serikali ya Zimbabwe na Chama cha ZANU-PF na kama mambo yataenda kama yalivyopangwa basi kuna uwezekano mkubwa siku chache zijazo au wiki ijayo Rais Robert Mugabe akatangaza rasmi kuachia ngazi Urais wake na kumkabidhi rasmi Bwana Emerson Mnangagwa hivyo kupelekea kutimia kwa mikakati ya Kisiri iliyopangwa na ambayo kiukweli imepangika na inaelekea kufanikiwa na kuwa ni alama ya ushindi kwa Rais Mugabe.

OMBI

Niwaombeni wale wote ambao mtaichukuwa hii taarifa na kuitumia katika Vyombo vyenu vya Habari au mitandao yenu kwamba rukhsa kuitumia / kuichukuwa ila chonde chonde msiache kufanya ' acknowledgement ' kama heshima ya Kitaaluma inavyotaka kwa GENTAMYCINE na Mtandao wangu huu pendwa wa JamiiForums kwani nimechukuwa muda wangu mwingi mno kulifuatilia kwa ukaribu sana hili jambo hivyo haitopendeza mkaitumia taarifa hii kwa kusema ni ya Kwenu au mmeitafuta nyie na mkifanya hivyo mtakuwa mmenivunja mno moyo na hata kunikatisha tamaa kuendelea kusaka taarifa mbalimbali na kuzifanyia Reporting na Analysis humu Jamvini.

Nawasilisha.
Wewe si huwa ni chizi? au siku hizi umepona?
 
Uchambuzi mzuri mkuu, ila kuna taarifa nilisikia kwamba kabla Grace hajavuka boda kutoroka alikamatwa na wanajeshi wakamhoji kisha wakamuachia asepe, vp haukuipata hilo mbona hujaliongelea kwenye uchambuzi wako? Pia vipi kuhusu Jacob Zuma kuwasiliana na Mugabe wakati wanajeshi wake wamemuweka chini ya ulinzi? Pia kuna kikao kilifanyika na baadhi ya viongozi wa Afrika kulijadili hilo suala je una details zake zozote? Je unajua kama Mugabe aliwaambia wanajeshi wake wanamuharibia ratiba zake za kufanya shughuli za nchi ikiwa ni pamoja na ile ratiba yake ya aliyohudhuria chuoni harare? Huu uzi wako bado una mambo mengi umeyaacha pending
 
Back
Top Bottom