Exclusive: 'PPFT (Politicised Police Force of Tanzania)

Julius Kaisari

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,176
671
Nilitamani kuandika heading yangu hivi " polisi (vyombo vya usalama) ya Tanzania ni sawa na mbwa mzee" .
Wakuu wanajamvi, nimekuwa nikitafakari huu mchezo mchafu , wa kisanii unaochezwa na vyombo vya usalama vya Tanzania,nashindwa kuelewa mwisho wake ni upi, kama siyo uvunjifu wa amani.
kwanini nasema hivi,; nadhani kuna ''maigizo'' tuliyokuwa tunayasikia kule Igunga,moja wapo likiwa lile la MAGAIDI,MAKOMANDOO, VIBAKA, WAHUNI n.k, kwa wamevamia nchi yetu wakitokea AFGHANSTAN,PALESTINA ,LIBYA,na ISRAEL kuja kusaidia chama fulani. Ukweli nadhani kila mwenye akili alitarajia kusikia BRIGEDI kadhaa zinaingia kazini kuinusuru nchi yetu na magaidi hao. Loooh, sarareeee, kumbe ni mchezo wa kuigiza na kuchota kura za hofu na ushindi wa Wanasiasa.
Hivi kweli tumefikia huko??? kwamba siku hizi mtu ukipita mtaani ukipiga PANDA (baragumu) kuwa tumevamiwa ,basi inakuwa poa tuu? Haki ya Mungu,!!!!
Hivi tuna JESHI LA WANANCHI? jeshi linalochezewa Sharubu na wanasiasa???
Ati tuna Jeshi la Polisi?? polisi jamii??? wanaolinda na kukumbatia wanasiasa wa Chama tawala???
Ati tuna Usalama wa taifa???? ptuuuuuuhhh!!!! UOZO mtupu.
Mwisho: kwa mtindo huu, tujiandae kwa mauaji ya haraiki yatayosababishwa na hivi vyombo feki vya usalama, pindi pale CCM itakapo ondolewa madarakani. Nina jiaminisha kuwa CCM haitokubali kushindwa. na itayatumia majeshi hayo kuilinda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom