Exclusive Pictures: SeaFront- Imeuzwa nayo!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Well.. tunaelekea mwaka wa Uamuzi na wenye uwezo ndio wakati wao tena kuonesha nguvu yao; kwa mara nyingine tena utajiri na urithi wa watoto wetu umepigwa mnada na wenye uwezo tayari wameshagawiwa. Ninafahamu kuwa kuweka habari hizi hakuwezi kubadilisha fikra za watawala wetu lakini kwa masikitiko makubwa tunawataarifu kuwa eneo lililokuwa wazi la Masaki Beach kama wengi wanavyojua nayo imeshapimwa viwanja na wenye kugawiwa wanajulikana!!

Maskini nchi yangu! Siku si nyingi tutauza hadi kingo za pale Magogoni na kuwaachia watoto wetu matamanio tu ya urithi wao!

i1630_locating.jpg


Tunazungumzia hilo eneo upande wa kulia wa picha.

i1625_kiwanja.jpg


wameona hayo majengo yako mbali sana.. wanataka mengine karibu kabisa na Tsunami!!

i1624_eneolenyewe.jpg


Unaweza ukasema tunazusha tu na lengo letu ni kupandikiza chuki dhidi ya serikali ya CCM!

i1628_stones.jpg


Unaweza kupingana vipi na ushahidi huu?

i1629_stones2.jpg


Au huu hapa? Miaka 33 ya CCM haya ndiyo matunda yenyewe jamani? Nyerere angelia leo.

i1626_kiwanja2.jpg


Unafikiri kuna kitu wanasubiri? well.. wachekwe?

i1627_satellieimage.jpg


Hivi hakuna mtu anayeweza kusema hapana katika hii serikali au ndio wote wana bei!?

Well asante ka"nzi" kwa kazi nzuri.. I owe you more this time. Malizieni ile kazi.. hatuna muda mwingi.. !!

Hebu angalieni Wamarekani walivyotenga eneo la Belle Isle hapa nje ya jiji la Detroit for almost 100 years now.. na sisi wengine tunaenda na kufaidi!! Unachoona hicho kama kisiwa ni park ya wazi na daraja hilo refu linaunganisha detroit na kisiwa hicho.. upande ule mwingine kama unavyoona ni Canada. Kuna beach hapo, kuna viwanja vya soka, barabara ya magari na baskeli, mabwawa.., bustani za maua n.k..

picture.php
 
Coco-Beach inauzwa lini vile? Maana harakati za kuiuza zimefanyika muda mrefu!
 
Ni hapa opposite na mjengo mpya wa UBALOZI WA UNITED ARAB EMIRATES?....
 
Tunahifadhi machozi ya kujililia wenyewe muda muafaka utakapofika. Hii nchi rushwa inatumaliza.
 
Kwani sheria ya Mazingira si inasema mita 60 kutoka ukanda wa Bahari ndizo ambazo zinatakiwa kuwachwa free?

Ikiwa mita 60 zimewachwa basi sehemu baki inaweza kubadilishwa matumizi.

Au nimekosea?
 
Mzee picha hazipo.

Swali, je mbele ya safari haya yatawezaje kurekebishwa hata kama tukipata Serikali makini? Unless tunapata kiongozi atakayemua kuwa 'dictator' atakayeweka utawala wa sheria pembeni kwa makusudi ili aweze kurekebisha mambo yote ambayo yameleta madhara kwa nchi yetu. I would like to imagine Tanzania with a leadership that would annul all controversial contracts, title deeds etc etc na kuanza upya!
 
Picha zinaonekana tena vizuri tu.
Ila mh! Inasikitisha. Watanzania tu watwana ndani ya nchi yetu.
 
Nadhani watawala wetu wanataka wakiondoka madarakani na maliasili zote zimeisha. Watawala wana malengo ya muda mfupi na wala hawafikirii kabisa vizazi vijavyo....
 
Back
Top Bottom