Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
NImesikia juzi ati Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amesema kuwa yuko tayari kujiuzulu endapo uongozi ulio juu yake utaamua afanye hivyo kufuatia wizi wa vocha za mbolea zenye thamani ya Tsh bilioni 6 kuibwa. Habari hii imeandikwa kwenye Habari Leo vile vile:
Nimeamua kujitolea kuelezea hili vizuri zaidi baada ya "ka nzi" kupita mitaa ya Rukwa (thanks ka-nzi.. you are becoming a pin in ccm's you know what!). Ifuatayo ni ripoti ya katoto ka "nzi"MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay, yupo tayari kujiuzulu endapo mamlaka za uteuzi (a.k.a Rais) zitamtaka awajibike kutokana na kashfa ya ufisadi wa fedha za ruzuku ya pembejeo za kilimo inayowakabili viongozi mkoani humo.
Njoolay amewaeleza waandishi wa habari kuwa, yupo tayari kujiuzulu ikiwa hana budi kufanya hivyo.
Ametoa msimamo huo baada ya kupokea taarifa ya tume aliyoiunda kuchunguza kashfa ya matumizi mabaya fedha za ruzuku ya pembejeo za kilimo kupitia mfumo wa vocha.
Inadaiwa kuwa,viongozi mkoani humo wametumia visivyo Sh bilioni 6.8,za ruzuku.
Uongozi wa Mkoa wa Rukwa unaiomba radhi sana serikali kwa kashfa hii iliyotokea mkoani na tutakuwa tayari kuwajibika kisiasa kama hapana budi, imesema sehemu ya taarifa ya Njoolay aliyoitoa kwa waandishi wa habari.
Taarifa ya tume hiyo ya watu tisa iliyofanya uchunguzi kwa takribani mwezi mmoja, imebainisha kuwa waliohusika na ufisadi huo ni watendaji 43 wa vijiji, mawakala 23, watumishi wanne wa kilimo ambao wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Kwa mujibu wa Njoolay,wenye nyadhifa za kisiasa waliobainika kuhusika na kashfa hiyo wakiwemo madiwani na wakuu wa wilaya watafikishwa kwenye vyama vyao vya kisiasa ili washughulikiwe huko.(say whaaaaaaat!)
Taarifa ya Njoolay imeeleza kuwa, uchunguzi wa tume umebaini mambo mengine kadhaa ikiwa ni pamoja na mkoa, wilaya na vijiji kutokuwa makini kusimamia na kufuatilia kwa karibu usambazaji wa ruzuku ya pembejeo ya kilimo kwa wakulima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,'wajanja' walitumia mwanya huo wa Serikali kutofuatilia kwa makini kuiibia Serikali mabilioni hayo ya fedha.
Kazi ya kufanya hesabu haijakamilika,lakini kiasi kilichokuwa kimechukuliwa benki ni Sh bilioni 6.8 na kilichobaki ni Sh bilioni 1.6 tu.
Kati ya hizo kiasi kilichotumika vizuri, asilimia 25 zimetumika Sumbawanga, asilimia 30 Nkasi na asilimia 80 wilayani Mpanda. (kutoka kwenye asilimia 100??)
Waliohusika kuiba fedha hizo za Serikali walitumia mbinu kadhaa ikiwa ni pamoja na kughushi sahihi za wakulima, kuandikisha wakulima hewa, wafu, watoto,na vichaa.
Mbinu zingine ni pamoja na kuwahonga wakulima fedha kidogo kati ya Sh 2,000 na 7,000 ili watie saini vocha bila kupata mbolea na pia kuwapatia wakulima idadi ndogo ya mbolea kuliko kiasi halisi walichosainishwa.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa imeagiza hatua kadhaa zichukuliwe zikiwemo za kuipongeza Wilaya ya Mpanda kwa kusimamia kwa ufanisi suala hili na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Serikali waliolegalega kufuatilia kwa ukaribu zoezi hili.
Hatua nyingine ni pamoja na mawakala wote na watendaji walioibia Serikali wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na tume iendelee na uchunguzi kuwabaini wengine, kuna uwezekano idadi ya watuhumiwa ikaongezeka.
Tume ya kuchunguza uozo huo uliokuwa ukipigiwa kelele na wakulima wengi waliolalamika kukosa pembejeo za kilimo msimu huu, iliundwa Januari 11, mwaka huu na mkuu wa mkoa huyo.
Mkoa wote kwa ujumla umekumbwa na kashfa ya wizi wa mbolea ya ruzuku. Lakini wizi huo umekuwa mkubwa zaidi katika wilaya ya Sumbawanga Vijijini kutokana na sababu kuu mbili. Kwanza, wilaya hii inapakana na nchi jirani za Zambia na DRC ambako mbolea hii imekuwa ikivushwa kimagendo. Pili, ndiyo wilaya iliyopokea mbolea ya ruzuku nyingi zaidi kutokana na sababu kwamba ndiyo inayozalisha mahindi kwa wingi katika mkoa huu napengine kitaifa.
Mbolea hii imeibwa kwa njia kuu zifuatazo
Kwanza mawakala kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa juu kabisa wa wilaya wamejaza majina ya uongo na ya watu waliokufa kwenye vocha za mbolea. Vile vile walichukua vitambulisho vya wapiga kura ambao ni masikini wasio hata na mashamba na kujaza majina ya hao watu kwenye vocha. Wale wachache waliopata mbolea kidogo waliwekewa sharti la kuandikisha kiasi kikubwa cha mbolea wanayohitaji ambapo walipewa chini ya robo ya mbolea hiyo, na inayobaki inakuwa mali yao.
Mbinu nyingine waliyoitumia ni kutoa taarifa zauongo kwamba kijiji Fulani hakihitaji mbolea, then vocha zote wanazihamisha na kujaza majina wanayojua wao. Vile vile utaratibu wa kuwapata mawakala ulikiukwa katika kata nyingi za Wilaya ya Sumbwanga Vijijini ambapo waliteuliwa tu badala ya kuchaguliwa na wajumbe wa kata. Hivyo mawakala wengi waliwekwa kwa maelekezo ya viongozi wa juu wa serikali ya wilaya.
Baada ya taratibu zote hizo, hawa mawakala wametumia hizo vocha kuchukua fedha benki, tena mbolea hiyo imeuzwa Zambia na DRC kwa wastani wa Tsh 40,000 kwa mfuko wa Kg 50 Urea na Tsh 60, 000 mbolea ya chumvi chumvi. Mipaka waliyo itumia ni Mozi, Mtula, Mpanga, Kasha, Bandari ya Kasanga, Kalembe-Kanamwene nk. Katika kata za mipakani kama vile Matai, Mwimbi, Ulumi, Mambwe Kenya na Kalembe hakuna kijiji hata kimoja ambacho wakulima zaidi 20 waliopata mbolea. Ukiacha makao makuu ya Kata hizo, katika vijiji vingine wastani wa walio pata mbolea ni 0-5 tu kwa wakazi wote. Hii siyo uongo mtu yeyote anaweza kutembelea kata hizo kama mfano tu na kuthibitisha wizi huu.
Kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mh. Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ndg. Njolai ameunda tume inayoendelea na kazi ya kufanya uchungizi. Tatizo tume hii ni kwamba inawajumbe ambao wanatuhumiwa na wananchi katika kashfa hii. Vile vile tume hii haikagui mashamba ili kubaini kama kweli walioandikwa kwenye vocha wapo na jje mashamba yao yamewekewa mbolea. Mbaya zaidi haitembelei vijiji badala yake inaenda tu katika makao makuu ya kata ambazo kidogo zina unafuu. Kwa kufanya tu mikutano ya hadhara na kuwahoji baadhi ya wananchi sidhani kama wote wahusika watachukuliwa hatua.
Ajabu ni kweamba ukienda kununua mbolea unaambiwa mbolea ya ruzuku ipo lakini vocha zimeisha. Tunashindwa kuelewa iweje mbolea ziwepo vocha ziwepo wakati kila mfuko wa mbolea uliletwa na vocha zake?
Itawagharimu sana wananchi kwa maana wengi walipanda mahindi karibu karibu badala ya kuachanisha kama walivyozoea maana walijua mbolea watapata. Nafikiri watu wa Sumbawanga hawajawahi kuona ufisadi kama huu. Mbolea imekuwa ikivushwa mchana kweupe bila hatua yoyote. Wananchi wanafikiri huenda serikali haiko serious na sera/ kauli mbiu ya kilimo kwanza au pengine haijui kwa nii imeamua kutoa mbolea ya ruzuku.
Ndugu, Mhariri hali huku ni mbaya. Kupata uhakika zaidi unaweza kutembelea huku ili ujionee mwenyewe. Ukienda Laela, Matai na Ulumi utaoneshwa maduka ya mbolea na majina ya wamiliki utambiwa ya wale walioteuliwa na Mh. Rais. Kwa huvi sasa nafikiri ndilo suala kubwa linaloongelewa na wananchi. Nafikiri huenda likawa na impact katika uchaguzi mkuu ujao maana sijawahi kuona wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakawa na hasira namna hii. Wamekuwa provoked sana katika hili.