Exclusive: Njoolay mrahishie Kikwete kazi; jiuzulu mwenyewe!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
NImesikia juzi ati Mkuu wa Mkoa wa Rukwa amesema kuwa yuko tayari kujiuzulu endapo uongozi ulio juu yake utaamua afanye hivyo kufuatia wizi wa vocha za mbolea zenye thamani ya Tsh bilioni 6 kuibwa. Habari hii imeandikwa kwenye Habari Leo vile vile:

MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Daniel ole Njoolay, yupo tayari kujiuzulu endapo mamlaka za uteuzi (a.k.a Rais) zitamtaka awajibike kutokana na kashfa ya ufisadi wa fedha za ruzuku ya pembejeo za kilimo inayowakabili viongozi mkoani humo.

Njoolay amewaeleza waandishi wa habari kuwa, yupo tayari kujiuzulu ikiwa hana budi kufanya hivyo.

Ametoa msimamo huo baada ya kupokea taarifa ya tume aliyoiunda kuchunguza kashfa ya matumizi mabaya fedha za ruzuku ya pembejeo za kilimo kupitia mfumo wa vocha.

Inadaiwa kuwa,viongozi mkoani humo wametumia visivyo Sh bilioni 6.8,za ruzuku.

“Uongozi wa Mkoa wa Rukwa unaiomba radhi sana serikali kwa kashfa hii iliyotokea mkoani na tutakuwa tayari kuwajibika kisiasa kama hapana budi,” imesema sehemu ya taarifa ya Njoolay aliyoitoa kwa waandishi wa habari.

Taarifa ya tume hiyo ya watu tisa iliyofanya uchunguzi kwa takribani mwezi mmoja, imebainisha kuwa waliohusika na ufisadi huo ni watendaji 43 wa vijiji, mawakala 23, watumishi wanne wa kilimo ambao wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa Njoolay,wenye nyadhifa za kisiasa waliobainika kuhusika na kashfa hiyo wakiwemo madiwani na wakuu wa wilaya watafikishwa kwenye vyama vyao vya kisiasa ili washughulikiwe huko.(say whaaaaaaat!)

Taarifa ya Njoolay imeeleza kuwa, uchunguzi wa tume umebaini mambo mengine kadhaa ikiwa ni pamoja na mkoa, wilaya na vijiji kutokuwa makini kusimamia na kufuatilia kwa karibu usambazaji wa ruzuku ya pembejeo ya kilimo kwa wakulima.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,'wajanja' walitumia mwanya huo wa Serikali kutofuatilia kwa makini kuiibia Serikali mabilioni hayo ya fedha.

Kazi ya kufanya hesabu haijakamilika,lakini kiasi kilichokuwa kimechukuliwa benki ni Sh bilioni 6.8 na kilichobaki ni Sh bilioni 1.6 tu.

Kati ya hizo kiasi kilichotumika vizuri, asilimia 25 zimetumika Sumbawanga, asilimia 30 Nkasi na asilimia 80 wilayani Mpanda. (kutoka kwenye asilimia 100??)

Waliohusika kuiba fedha hizo za Serikali walitumia mbinu kadhaa ikiwa ni pamoja na kughushi sahihi za wakulima, kuandikisha wakulima hewa, wafu, watoto,na vichaa.

Mbinu zingine ni pamoja na kuwahonga wakulima fedha kidogo kati ya Sh 2,000 na 7,000 ili watie saini vocha bila kupata mbolea na pia kuwapatia wakulima idadi ndogo ya mbolea kuliko kiasi halisi walichosainishwa.

Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa imeagiza hatua kadhaa zichukuliwe zikiwemo za kuipongeza Wilaya ya Mpanda kwa kusimamia kwa ufanisi suala hili na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa Serikali waliolegalega kufuatilia kwa ukaribu zoezi hili.

Hatua nyingine ni pamoja na mawakala wote na watendaji walioibia Serikali wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na tume iendelee na uchunguzi kuwabaini wengine, kuna uwezekano idadi ya watuhumiwa ikaongezeka.

Tume ya kuchunguza uozo huo uliokuwa ukipigiwa kelele na wakulima wengi waliolalamika kukosa pembejeo za kilimo msimu huu, iliundwa Januari 11, mwaka huu na mkuu wa mkoa huyo.
Nimeamua kujitolea kuelezea hili vizuri zaidi baada ya "ka nzi" kupita mitaa ya Rukwa (thanks ka-nzi.. you are becoming a pin in ccm's you know what!). Ifuatayo ni ripoti ya katoto ka "nzi"

Mkoa wote kwa ujumla umekumbwa na kashfa ya wizi wa mbolea ya ruzuku. Lakini wizi huo umekuwa mkubwa zaidi katika wilaya ya Sumbawanga Vijijini kutokana na sababu kuu mbili. Kwanza, wilaya hii inapakana na nchi jirani za Zambia na DRC ambako mbolea hii imekuwa ikivushwa kimagendo. Pili, ndiyo wilaya iliyopokea mbolea ya ruzuku nyingi zaidi kutokana na sababu kwamba ndiyo inayozalisha mahindi kwa wingi katika mkoa huu napengine kitaifa.

Mbolea hii imeibwa kwa njia kuu zifuatazo

Kwanza mawakala kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa juu kabisa wa wilaya wamejaza majina ya uongo na ya watu waliokufa kwenye vocha za mbolea. Vile vile walichukua vitambulisho vya wapiga kura ambao ni masikini wasio hata na mashamba na kujaza majina ya hao watu kwenye vocha. Wale wachache waliopata mbolea kidogo waliwekewa sharti la kuandikisha kiasi kikubwa cha mbolea wanayohitaji ambapo walipewa chini ya robo ya mbolea hiyo, na inayobaki inakuwa mali yao.

Mbinu nyingine waliyoitumia ni kutoa taarifa zauongo kwamba kijiji Fulani hakihitaji mbolea, then vocha zote wanazihamisha na kujaza majina wanayojua wao. Vile vile utaratibu wa kuwapata mawakala ulikiukwa katika kata nyingi za Wilaya ya Sumbwanga Vijijini ambapo waliteuliwa tu badala ya kuchaguliwa na wajumbe wa kata. Hivyo mawakala wengi waliwekwa kwa maelekezo ya viongozi wa juu wa serikali ya wilaya.

Baada ya taratibu zote hizo, hawa mawakala wametumia hizo vocha kuchukua fedha benki, tena mbolea hiyo imeuzwa Zambia na DRC kwa wastani wa Tsh 40,000 kwa mfuko wa Kg 50 Urea na Tsh 60, 000 mbolea ya chumvi chumvi. Mipaka waliyo itumia ni Mozi, Mtula, Mpanga, Kasha, Bandari ya Kasanga, Kalembe-Kanamwene nk. Katika kata za mipakani kama vile Matai, Mwimbi, Ulumi, Mambwe Kenya na Kalembe hakuna kijiji hata kimoja ambacho wakulima zaidi 20 waliopata mbolea. Ukiacha makao makuu ya Kata hizo, katika vijiji vingine wastani wa walio pata mbolea ni 0-5 tu kwa wakazi wote. Hii siyo uongo mtu yeyote anaweza kutembelea kata hizo kama mfano tu na kuthibitisha wizi huu.

Kufuatia agizo la Waziri Mkuu Mh. Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ndg. Njolai ameunda tume inayoendelea na kazi ya kufanya uchungizi. Tatizo tume hii ni kwamba inawajumbe ambao wanatuhumiwa na wananchi katika kashfa hii. Vile vile tume hii haikagui mashamba ili kubaini kama kweli walioandikwa kwenye vocha wapo na jje mashamba yao yamewekewa mbolea. Mbaya zaidi haitembelei vijiji badala yake inaenda tu katika makao makuu ya kata ambazo kidogo zina unafuu. Kwa kufanya tu mikutano ya hadhara na kuwahoji baadhi ya wananchi sidhani kama wote wahusika watachukuliwa hatua.

Ajabu ni kweamba ukienda kununua mbolea unaambiwa mbolea ya ruzuku ipo lakini vocha zimeisha. Tunashindwa kuelewa iweje mbolea ziwepo vocha ziwepo wakati kila mfuko wa mbolea uliletwa na vocha zake?

Itawagharimu sana wananchi kwa maana wengi walipanda mahindi karibu karibu badala ya kuachanisha kama walivyozoea maana walijua mbolea watapata. Nafikiri watu wa Sumbawanga hawajawahi kuona ufisadi kama huu. Mbolea imekuwa ikivushwa mchana kweupe bila hatua yoyote. Wananchi wanafikiri huenda serikali haiko serious na sera/ kauli mbiu ya kilimo kwanza au pengine haijui kwa nii imeamua kutoa mbolea ya ruzuku.

Ndugu, Mhariri hali huku ni mbaya. Kupata uhakika zaidi unaweza kutembelea huku ili ujionee mwenyewe. Ukienda Laela, Matai na Ulumi utaoneshwa maduka ya mbolea na majina ya wamiliki utambiwa ya wale walioteuliwa na Mh. Rais. Kwa huvi sasa nafikiri ndilo suala kubwa linaloongelewa na wananchi. Nafikiri huenda likawa na impact katika uchaguzi mkuu ujao maana sijawahi kuona wananchi wa Mkoa wa Rukwa wakawa na hasira namna hii. Wamekuwa provoked sana katika hili.
 
Haya sijui PM atasema nini, na sera zake za kilomo kwanza. Mbolea zenyewe zinaibiwa nje ya mlango wake. Kawafukuza watu majuzi huko dar kwa uzembe, labda mi nadhani mwanakijiji ungemuuliza Mh.Pinda kwamba jamaa yuko tayari kuwajibishwa kwa uzembe wake.

Tukimuona anayo kazi hadi wiki ijayo huyu jamaa PM atakua ni msanii tu vile vile. Asilete mambo ya double standard fire the 'bozzo' who is responsible.
 
Kikwete hana la Kufanya juu ya hili kuna ambaye hamjui Mr Prezident katika kufanya maamuzi ..
 
tumewatajia hadi mambo mengine ambayo walidhani hayajulikani; natumaini Pinda huko Singida ataamua kuchukua uamuzi wa kumshauri Rais kuchukua uamuzi unaostahili..
 
kwa kuwa mkuu wa mkoa huo haivani na presidaa wetu basi huenda maamuzi flan yakafanyika.

karibu kila mkoa mbolea hii imeibiwa sana tu labda huko kwa njolay kumezid!
 
kwa presidaa huyu hilo mzee MM haliwezekani, labda atamhamishia Njoolay Dar aje kula kuku
 
Sijui nianzeje kwenye hili nalo... huo ni mkoa mmoja tu watu wanalamba bil. 6, kesho tukiambiwa hela ya kilimo kwanza imeisha then tunaanza kupiga kelele

hali iko hivyo kwa vitu vingi tu na mbole peke yake, mikoa yetu yote iliyo na borders iko porous na sielewi kwanini wanaweka viongozi dhaifu

Kuna wakati nilipost kuhusu our governance structure is not functional basing the quality of people we have onboard na geography yetu

decentralization may not be the best idea kwa baadhi ya vitu simply because we are very lenient to criminals
 
JK hawezi kuwawajibisha wasaidizi wake on the spot, labda kama kelele za kumtaka afanye hivyo zikiendelea....yeye yuko bariidi pale mjengoni.
 
tumewatajia hadi mambo mengine ambayo walidhani hayajulikani; natumaini Pinda huko Singida ataamua kuchukua uamuzi wa kumshauri Rais kuchukua uamuzi unaostahili..

Yo know what mkuu, haya maswala ya ruzuku ya Mbolea yapo pia Malawi. Na infact mbolea inayouzwa mfuko wa 50kg in Tz around 100,000 TZS, kwa Malawi ni kama 6000TZS. Lakini You will never ever find hiyo mbolea ya Malawi in Tz. Ila sisi tulipoanza tu mambo ya Ruzuku kabla ya Malawi anywayz, mbolea ilikuwa inavushwa usiku na mchana and was one of the hot cake biz by then.

SO WHY? It is all about consequences, Mr Bingu is very serious on the matter and he mean it. Ukikamatwa na mbolea mfukop mmoja unauvusha ni 1yr jail sentence bila kona kona. The same kwa mifuko 100 ni miaka 100 jela. Gari, mkokoteni, pikpiki itakayokamatwa kwa ajili ya kuvusha is seized right away by the govt.

Sisi tumekaa kifisadi fisadi as such hakuna agizo wala utaratibu unaoweza kuendeshwa bila ufisadi..Na hili pendekezo la wahalifu wapelekwe kwenye vyama vyao wakashiughulikiwe huko , Is TZ serious?????????
 
Ni habari ya kusikitisha sana,ubinafsi na tamaa za maisha bado ni ugonjwa kwa viongozi wetu.....sasa sijui KILIMO KWANZA ndio kina shika kasi ya kwenda nyuma au ni changamoto kama wasemavyo.........!
 
tumewatajia hadi mambo mengine ambayo walidhani hayajulikani; natumaini Pinda huko Singida ataamua kuchukua uamuzi wa kumshauri Rais kuchukua uamuzi unaostahili..
Kauli ya Njolay ni ya kujikosha kisiasa na mtego kwa Raisi..Anatambua uhusiano wake na Mkuu ukoje na angependa kuondoka kwa style ya kuachiana maswali hasa kwa umma..Ni nadra viongozi wakuu hasa hawa wa kisiasa wanapokosea hutoa kauli kama hizooo..naona TUNASONGA Mbele taratibuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu....

Nategemea PM amwite huyoo Njolay wajadili kwa maelekezo ya Raisi na hatimayee achiee ngazi..Itatusaidiaa kwa Maeneo mengine ambayo viongozii wamezoeaa kukosea na kubaki madarakanii..
 
lakini hawa watu wanataka tuwafanyie kazi zote kweli? tumewaambia kuhusu kuuzwa mbezi Beach wanakubali kuwa kumefanyika makosa.. lakini wanataka kuunda timu kuchunguza; zimeibwa voucha huko wanafanya nini? wanaunda tume kuchunguza; wamejenga majumba ya bilioni mbili na nusu hivi badala ya kuchukua hatua wanaunda tume!!
 
lakini hawa watu wanataka tuwafanyie kazi zote kweli? tumewaambia kuhusu kuuzwa mbezi Beach wanakubali kuwa kumefanyika makosa.. lakini wanataka kuunda timu kuchunguza; zimeibwa voucha huko wanafanya nini? wanaunda tume kuchunguza; wamejenga majumba ya bilioni mbili na nusu hivi badala ya kuchukua hatua wanaunda tume!!

Njoolay na mafisadi wenzake hawatakiwi kujiuzulu bali washitakiwe na warudishe pesa zote walizoiba na kufungwa.

MM si mbolea tu:
-Mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami sumbawanga mjini kama ilivyo katika mji wa panda nao umekufa (inasemekana Njoolay na mafisadi wenzake wamekula pesa)
-Hata Nusu ya Uwanja wa saba saba sumbawanga Njoolay amemuuzia mmiliki wa kampuni ya Tawaqal.

NI BAHATI MBAYA KWA WATANZANIA NA BAHATI NZURI KWA MAFISADI KWAMBA HATUNA RAIS ANAYEJUA WAJIBU WAKE
 
lakini hawa watu wanataka tuwafanyie kazi zote kweli? tumewaambia kuhusu kuuzwa mbezi Beach wanakubali kuwa kumefanyika makosa.. lakini wanataka kuunda timu kuchunguza; zimeibwa voucha huko wanafanya nini? wanaunda tume kuchunguza; wamejenga majumba ya bilioni mbili na nusu hivi badala ya kuchukua hatua wanaunda tume!!
MWanakijiji, your role no informal/formal... whether you like it or not, upo hapa for a reason, na kamwe usisikitike ni namna mambo yalivyo

endelea kuwa kiungo muhimu ila pia recruit system yako ya vi-nzi mara dufu kwani UWT wanaonekana kujua yanayoendelea lakini wanakuwa mute
 
lakini hawa watu wanataka tuwafanyie kazi zote kweli? tumewaambia kuhusu kuuzwa mbezi Beach wanakubali kuwa kumefanyika makosa.. lakini wanataka kuunda timu kuchunguza; zimeibwa voucha huko wanafanya nini? wanaunda tume kuchunguza; wamejenga majumba ya bilioni mbili na nusu hivi badala ya kuchukua hatua wanaunda tume!!

Mkuu,

Hiyo ndio namna pekee Wanayoona kazi zinafanyika ambazo Watanzania wengi bado wana wanaona...IGP naye aliunda Tume kuchunguza kifungu cha Sheria kuhusu raia kumiliki pingu. Can you imagine...??!!

Hawa viongozi wetu hawana fikra mbadala za kusukuma maendeleo wao wanafuata taratibu walizozikuta tu..kama Robots.
 
Hao maafisa watakuwa ni watu wenye akili nzuri sana. Wanajifunza kwa urahisi sana.

Nasema hivyo kwa kuamini kwamba wameona jinsi nchi inavyoendeshwa na kujifunza nini kitatokea kama wakiamua kuiba. Wanfahamu. Hakuna kitakachotokea.

Nani achukuwe hatua?
 
Kwani yeye hawezi kuamu mpaka uongozi wa juu utake?kama anaona amekosea anapaswa kufanya hivyo kabla hata hajaambiwa kufanya hivyo.Viongozi wetu bwana wamezoea kushinikizwa tu..aargh!
 
Hili suala nililipata kijuu juu mwaka jana nikiwa Sumbawanga, sijaamini kwamba limeenda deep kiasi hiki. Kimsingi kwa stori nilizopata, huu 'Wizi Mtupu' wa mbolea ya ruzuku una mizizi mirefu sana, kiasi kwamba kama ni kuwajibisha watendaji basi huenda uongozi mzima wa mkoa wa Rukwa utawajibika.
Kuna bwana mmoja ambaye katajirika ghafla na mbolea hii ya wizi, yeye yuko kijiji cha Matai, ana guest houses kadhaa Matai na Sumbawanga mjini, ana malori kadhaa na mashamba makubwa ya mahindi ambapo kapata vitu vyote hivi 'within no time'. Kwa stori nilizopewa pale ni kwamba naye ni mfaidika wa mbolea hii ya wizi, kwa mgongo wa mkubwa fulani, kwamba mkubwa huyu anamtumia mfanyabiashara huyu kama 'Pen name'. Kijiji cha Matai kiko karibu kabisa na Kongo na Zambia, pamoja na bandari ya Kasanga.
Kuna kiungo cha stori hii natafuta ili tuunganishe, be back later.
 
Back
Top Bottom