Exclusive: Njoolay mrahishie Kikwete kazi; jiuzulu mwenyewe!

halafu kuna mpuuzi alidai kuna "usalama wa taifa"..
nani huyo?
ki ukweli hawa jamaa wapo ila sasa ufinyu wamishahara yao umelifanya taifa liwe la kihuni.

tatizo lao kubwa ni matabaka yaliyo ndani ya sekta hi lakini pia udugu ni mwingi mno.
 
Katika mikoa niliyowahi kutembelea hakuna mkoa ulio na mafisadi kama rukwa. Huu mkoa umesahaulika kabisa. Haufikiki kirahisi,hivyo kuna watu wanaendeleza ufisadi wakijua hawatafikiwa.

Serikali inatakiwa kuuangalia upya huu mkoa,ufisadi uko kila mahali,ukianzai kwenye barabara,afya,elimu, kilimo na kila kitu.​
 
Uongozi wa nchi yetu umejificha nyuma ya kisingizio cha kufuata sheria; kwamba watenda maovu hawawezi kuchukuliwa hatua mpaka uchunguzi ufanyike kuthibitisha kwamba kuna kosa limetendeka na kama itadhihirika kosa limetendeka wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria ili hatimaye wawe proven guilty , bla, bla, bla …...

Mlolongo huu ni danganya toto kwa sababu wananchi tunajua na viongozi nao wanajua kwamba hakuna sheria yoyote itakayochukua mkondo wake effectively kwa sababu ya corruption iliyokithiri. Hili linajulikana lakini tunalifumbia macho kwa kujidanganya ama kudanganywa kwamba nchi yetu inafuata utawala wa Sheria.

Inabidi tufike mahali tujiulize, Malawi wamefanikiwaje kuweza kuwa na utaratibu unaowajibisha wahalifu wa aina hiyo papo hapo without delay? Sisi je tunashindwa nini kuwa kama wao?

Njolay anatingisha kiberiti tu! Angelikuwa mkweli angeliomba kujiuzulu ili atangazwe kwamba amefanya hivyo na si yeye kuanza kutamka kwenye vyombo vya habari kwamba atajiuzulu.
 
Oooooooooh dear Me Pinda!

Hivi Pinda ulisemaje vile kuhusiana na Wauaji wa Walemavu wa Ngozi vile? C'mon, You have to show the way this TIME!

Kazi bado ni kubwa: ongo ya buku mbili unasaini vocha hewa?
 
Hongera Njoolay. Nampongeza Njoolay kuwa kiongozi aliyechukuwa hatua haraka baada ya kupata habari za ufisadi wa mbolea na kuunda kamati ya uchunguzi. Ni hatua ambayo Kiongozi yoyote makini ndivyo anavyotakiwa kufanya mara tu baada ya kupata taarifa. Uzuri yeye amepata taarifa akazifanyia kazi haraka na majibu ya uchunguzi yameanza kufanyiwa kazi. Ningefurahi zaidi kama kamati ingemaliza kazi yake kwa kufanya uchunguzi kwa wote waliohusika pamoja na wafanyabiashara waliohusika. Ninaamini kabisa kutakuwepo mpaka na wafanyabiashara papa hasa wanaoingiza mbolea nchini na hawa huwa wanaitwa untouchable. Uchunguzi huo ufanyike mpaka ijulikane mbolea hiyo iliishia wapi. Ukishafahamu kila kitu ndiyo tu unaweza kuzuia upotevu kama huo usitokee tena. Heko Njoolay!!! Kama ungejiuzulu ingekuwa vizuri kwa wale waliochini yako maana wote watasema ni wewe...si unakumbuka Richmond na EL na Mawaziri? Wao wamejiuzulu na watendaji wa chini ambao ndiyo wamefanya madudu bado wapo kazini kwanza kwa kusafishwa na kufutiwa kashfa na tume zao za nidhamu nalo Bunge juzi limebariki. Swali PM na Mawaziri wao ndiyo walikuwa wanaandika na kutoa hiyo mikataba? Wale washauri na wahusika wakuu wako wapi? Tunahitaji kusafisha kwenye mizizi kama tunataka tumalize au kupunguza ufisadi na kutowajibika kwa watendaji wa serikali. Ukikata matawi bado mti wa ufisadi utandelea kumea, inakiwa kung'oa na mizizi yake na hii inatakiwa hawa watendaji walioko chini wote wawajibishwe ili wajue kuwa wanafanyakazi kwa ajili ya wananchi na hawawezi kujificha chini ya kivuli cha wakubwa!!!!!
 
To my opinion wote hapa bongo ni wezi!! Kama ni kuchukua hatua ni bora kufukuza na kupeleka mahamani kuanzia ward excutives to R.C. Hili mnalosema kujiuzulu doesnt hold water. Wengi kwenye madaraka sasa hivi walishaiba na wamejiandaa kuwajibishwa .Mali zao zipo kwa majina ya watu wengine.
 
Nani atamuwajibisha nani nchi hii ni lazy affair hatuna utamaduni wa kujiuzulu mpaka ufukuzwe. Sasa ni lazima watu wa Rukwa wamuulize Pinda amewasimamisha kazi watendaji wa Bagamoyo kwa tuhuma anangoja nini kwa Njolay na wanzake ? Ujenzi hafifu chini ya kiwango barabara za lami Sumbawanga mjini Njolay hausiki ? Viongozi wanamaliza nchi ni lazima sasa Watanzania tuchukue hatua kuiwajibisha CCM na Serekali yake inatosha
 
Kama kujiuzulu basi wangeanza mapema sana utamaduni huo kwa viogozi wa JK ulikwisha kipindi cha EL maana yeye ndiye atleast alisema kwa hasira na yakatokea hivyo na kwa sasa sijui kama utamaduani huo
 
nani huyo?
ki ukweli hawa jamaa wapo ila sasa ufinyu wamishahara yao umelifanya taifa liwe la kihuni.

tatizo lao kubwa ni matabaka yaliyo ndani ya sekta hi lakini pia udugu ni mwingi mno.

Mimi nakataa mishahara sio tatizo ila tatizo ni priority zao ambazo ni kupambana na upinzani, Alafu si kuna PCCB? Kazi yao nini hawa jamaa? si tunambiwa wanaofisi kila wilaya? Lakini sishangai kama mkuu wa mkoa naye yumo ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa unategemea nani ataongea hapo? KILIMO KWANZA Oyee!!!:D:D:D
 
"Uongozi wa Mkoa wa Rukwa unaiomba radhi sana serikali kwa kashfa hii iliyotokea mkoani na tutakuwa tayari kuwajibika kisiasa kama hapana budi," imesema sehemu ya taarifa ya Njoolay aliyoitoa kwa waandishi wa habari.

Taarifa ya tume hiyo ya watu tisa iliyofanya uchunguzi kwa takribani mwezi mmoja, imebainisha kuwa waliohusika na ufisadi huo ni watendaji 43 wa vijiji, mawakala 23, watumishi wanne wa kilimo ambao wote watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kwa mujibu wa Njoolay,wenye nyadhifa za kisiasa waliobainika kuhusika na kashfa hiyo wakiwemo madiwani na wakuu wa wilaya watafikishwa kwenye vyama vyao vya kisiasa ili washughulikiwe huko.(say whaaaaaaat!)



Tunashukuru kwa kuombaradhi
Ila kwa nini wengine mahakani na wengine kwenye chama? Ina maana kama ni mwenyekiti au diwani apelekwi mahamani ila kwenye vikao vya chama? kwani wameiba hela za chama? ACHENI UTANI BWANA!! Pinda yu wapi jamani? KILIMO KWANZA? Huu mkoa ndio kati ya mikoa .... inayotegemewa kulilisha taifa yenyewe inatambulika kama big ...., Sasa itakuweje mwakani? Si njaa tu?
 
Hivi ni lini Bunge litamuhoji Rais ili atoe maelezo ya kina kwa taifa kuhusu uozo wa kutisha uliopo nchini mwetu kwa sasa na unaoendelea kutokea kila kukicha???!!!
 
Kapu zima limeoza na sijui mnategemea unafuu upi!
nchi yetu imefikia mahala ambapo hakuna tena nafasi ya kutolea mfano..
Nchi imeoza jamani ufisadi kwa kwenda mbele. Sioni sababu ya mtu huyu mmoja kujiuzulu hali sioni kiongozi bora ktk sekta zote za na mashirika yake.
Wenzetu wanasema show me a beautful lady, I will show you who damped her!
 
sitashangaa kama hata jiuzulu, nitashangaa akiondolewa madarakani, sitashangaa kama akihamishwa kituo cha kazi as punishment, au akiteuliwa kuwa waziri kama akiamua kugombea ubunge. Bila shaka atajiuliza kwanini yeye awajibike wakati wezi ni wengine, na kwaninini walio wezi wanaojulikana wazi wanaachwa? as simple as that.
 
nani huyo?
ki ukweli hawa jamaa wapo ila sasa ufinyu wamishahara yao umelifanya taifa liwe la kihuni.

tatizo lao kubwa ni matabaka yaliyo ndani ya sekta hi lakini pia udugu ni mwingi mno.

Si kweli kuwa ni mishahara, hawa jamaa wanakula pesa nyingi mno na nyingi hazikatwi hata kodi ya mapato na haziwi audited.
 
Halafu hawa ndio watendaji wa serikali mnaotaka washiriki kuiondoa serikali ya ccm madarakani! Hamjui utamu wa mfupa wa goti nyie.

Labda ndio juhudi zenyewe za kushamirisha kilimo kwanza!
 
Back
Top Bottom