Exclusive: Mkubwa Fella asema Yeye ndiyo humbebea Hirizi na Matunguri Diamond Stejini

kifimbocheza_

JF-Expert Member
Jul 14, 2017
1,116
2,000
Acha uwongo na muogope Mungu wako hapo hapo ulipo Mkuu kabla ' hajakulaani '. Ali Kiba si ' Mshirikina ' na wala hata huo ' Ushirikina ' wenu Wewe, Mkubwa Fella na Ndugu yenu Diamond Platinum wala haujui. Halafu siku zote hata Sura za Watu huonyesha dhahiri matumizi ya ' Ushirikina '.

Hivi kwa Sura ya ' Uhendisamu boi ' ile ya Ali Kiba unadhani anahitaji kweli ' Ndumba ' ili kujaza Ukumbi anapokuwa anapafomu? Sasa angalia Sura ya Diamond Platinum nadhani ilivyo tu inajionyesha dhahiri kuwa anahitaji ' Ndumba ' ya Kufa Mtu ili ' Nyomi ' liwepo Ukumbini kwani hivi hivi anaweza akajikuta anaimba Yeye huku Mbuzi, Ng'ombe, Kuku na Bata wakimtizama badala ya Wanadamu.

Kwa post hii ya ' Kimakusudi ' na ' Kichokonozi ' najua sasa mtakuja rasmi na Mimi leo nina hamu sana ya ' Kuparurana ' nanyi na hivi Meneja wake / wenu Mkubwa Fella kathibitisha mwenyewe mubashara Clouds TV leo ' mtanikoma ' hakyanani Team Ndomo.

Na kitendo chake cha kwenda ' Kumshitaki ' mwana Dimpoz mwenzangu Ommy Central ndiyo kumenitibua na kunikasirisha kabisa juu ya huyo Mpuuzi wenu. Hivi mambo ya Chumbani tena ya Sirini Mwanaume uliyekamilika kweli kila siku asubuhi ' Mnara wako wa Babeli ' namaanisha Mkuyenge wako unasimama unaweza kumpeleka Polisi Mwanaume mwenzio kwa mambo ya Sirini / Faragha?

Amenichefua sana na nilikuwa namtafutia tu ' angle ' na hatimaye leo Mkubwa Fella amenianzishia. Namshukuru sana.

Team Ndomo mpo wapi?
Popoma kwny ubora wako......ww mbona sura lako bovu kama tako la kaoge na mtaani tumekuvumilia tu....kumbe na ww mshirikina eeeh mnajuana na washirikina wenzio......tutakuhamisha mtaa soon kumbe tunaishi na lichawi mtaani kwetu..!!!
 

brizy kisamo

Member
Feb 28, 2017
8
45
Naona wabeba ' matunguri ' na ' hirizi ' wa Ndomo Diamond Platinum sasa mmeamka na mmekuja. Naomba waamshe kabisa na Team Ndomo wenzio ili mje kwa wingi kwani ifikapo Saa 5 kamili muda mchache kutoka sasa nita log out ila mnamo Saa 8 kamili mchana huu hadi Saa 9 kamili alasiri ya leo nitarudi na nitakuwepo tena humu Jamvini JF ili kuja kuwajibuni vizuri. Naomba muyatumie vizuri haya masaa matatu ambayo nitakuwa sipo online muweze kujibu ' Hoja ' na nikija niweze kuzikabili vizuri.

Sasa ni rasmi GENTAMYCINE ni Team Kiba na Team Dimpoz. Diamond Platinum bye bye.
kuwa team dai au kiba ni ww na maslahii yako ......mm sina timu kikubw ni kwmba domo anatusua kwaiy unajihangaisha kubishn ujinga...alaf njia ya mafanikio ina mambo mengiii hukum hutok kwa Mungu...na km umeumia xn dai ofisi yake ipo pale kijitonyma unawez kwend kumwambia aache hzo mambo.......maan misulii inakutoka kchz kwa upuuziii
 

kifimbocheza_

JF-Expert Member
Jul 14, 2017
1,116
2,000
Naona wabeba ' matunguri ' na ' hirizi ' wa Ndomo Diamond Platinum sasa mmeamka na mmekuja. Naomba waamshe kabisa na Team Ndomo wenzio ili mje kwa wingi kwani ifikapo Saa 5 kamili muda mchache kutoka sasa nita log out ila mnamo Saa 8 kamili mchana huu hadi Saa 9 kamili alasiri ya leo nitarudi na nitakuwepo tena humu Jamvini JF ili kuja kuwajibuni vizuri. Naomba muyatumie vizuri haya masaa matatu ambayo nitakuwa sipo online muweze kujibu ' Hoja ' na nikija niweze kuzikabili vizuri.

Sasa ni rasmi GENTAMYCINE ni Team Kiba na Team Dimpoz. Diamond Platinum bye bye.
 

fasiliteta

JF-Expert Member
Jul 2, 2014
2,114
2,000
Ila huo ' Ushirikina ' wa Mkubwa Fella na anayemmaneji ' Ndomo hadi anawavutia Mashabiki maelfu Ukumbini bado sijaufikia kwani wenzangu watakuwa wapo zile levels ' zisizojulikana ' za Ushirikina / Ndumba hapa Ulimwenguni.
Wabongo BANAAA,,oooohhh pambana ufanikiwe hayo ndo maushauri mnatoagaUkishafanikiwa Mara ooohh ndumba Mara sijui nn


Ujinga mtupu na imani za kishirikina zimetujaaa zaid ya washiriki WENYEWE wa USHIRIKINAWewe Jamaa hapo ulipo ushawahi si wengi tu wamekuloga ndo mana hufanikiwi
PAMBANA NA HALI YAKO
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
54,744
2,000
Huyo jamaa kulikua na tamasha leaders club lilikua organized na THT/clouds ..mvua na wingu zito likatanda mchana kweupe...RG akamuita akiwa yuko frustrated akamuuliza 'show itaharibika na mvua inashuka..we unafanya kazi gani hapa' jamaa (Fella) akaondoka chemba aliporudi wingu lilikatika na show ikapigwa..(Nilikuwepo) we jiulize MTU hata caption zake za insta kuandika hajui eti nae anatunga 'by-laws' za wakazi wa TMk..
I like you u know
 

kipanta

JF-Expert Member
Sep 2, 2014
735
1,000
Wabongo kwa unafiki na uongo hamjambo...haya na wewe nenda karoge upate pesa na uanze kujaza hayo mashow kama utaeza...acha unafiki wa kuchafua watu...ukiona mtu anaamini uchawi basi nae ni mchawi tena alotukuka....
 

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
12,872
2,000
Akizungumza kwa kujiamini kabisa na mikogo yote unayoijua Wewe Meneja mzoefu wa Wasanii maarufu na wakubwa nchini Tanzania na Diwani wa Kata ya Kilungule kupitia Chama cha Mapinduzi Said Fella ( Mkubwa Fella ) amesema kuwa Yeye Kazi yake kubwa kwa Diamond ni kumvutia tu mashabiki wengi Ukumbini kwa kutumia ndumba / ushirikina ambao amesema kuwa si tu amebobea bali ametukuka nao kabisa.

Maneno haya ameyatoa mubashara leo hii Siku ya Jumamosi tarehe 16 mwezi Septemba alipokuwa akifanya mahojiano na Watangazaji wa Kipindi cha Clouds tv 360 on Saturday akina Ceaser ( Siza ) na mwenzake Gibson.

Swali la Mtangazaji Siza kwa Mkubwa Fella lilikuwa kama lifuatavyo..." Tafadhali Mkubwa Fella hebu tuambie Wewe majukumu yako makuu hasa kwa Mwanamuziki Diamond Platinum ni yapi kwani Watazamaji na Watanzania kwa ujumla wangependa sana kujua ".

Majibu ya Mkubwa Fella yalikuwa yafuatayo... " Kicheko kikubwa kilianza na akasema unajua pale tupo Watu kama Watatu hivi Mimi Fella, Babu Tale na Meneja Salam na wote tuna majukumu yetu ila Mimi hasa jukumu langu ni kuhakikisha nabeba Silaha zangu za Kiutamaduni natembea nazo kila ambapo Diamond Platinum anaenda kufanya Show yake ili niweze kumvutia Mashabiki wengi na pia wazidi kumpenda. Kwa Sisi Waafrika hasa Watanzania haya mambo siyo mageni na yanafanyika mno tu ".

Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida na iliyoonyesha kwamba kweli Mkubwa Fella ni Mtoto wa Mjini hasa na pengine ndiyo maana anaishi kwa Masela na Wajanja Temeke alipotakiwa kutolea ufafanuzi hiyo kauli yake ya mwanzo kwa mshangao mkubwa sana pale pale aligeuza maelezo yake ya awali na kusema hivi namnukuu..." Hapana siyo kwamba labda namaanisha kuwa namfanyia Ushirikina / Ndumba Diamond Platinum ili ajaze Watu Ukumbini bali nilichomaanisha tu ni kwamba Mimi huwa nahakikisha kwamba kule kote ambako Diamond Platinum anaenda Kupafomu nakamata Marafiki zangu walioko huko na kisha nawajaza upepo / nawatia sana ndimu kwa kuwaambia wahamasishe Watu wa huko waje kuingia katika Shows za Mwanangu na ndiyo maana unaweza kuona kila Show ya Diamond Platinum huwa kunakuwa na Nyomi la Kufa Mtu ".

Mwisho nadhani leo Diwani wa CCM Kilungule na Meneja wa Wasanii Said Fell ( Mkubwa Fella ) amehitimsha rasmi ule mjadala wa kwamba Msanii Diamond Platinum ni mpenda ' Shiriki / uchawi ' kwani Yeye kama Meneja wake tena wa siku nyingi ' amekiri ' kuwa ndiyo humbebea matunguri na hirizi zote ili aweze kumjazia Watu / Mashabiki Ukumbini.

Akhsante sana Mkubwa Fella.

Nawasilisha.
Muziki wa TZ unashikiliwa na Diamond ,Diamond akifa au akiacha kuimba TZ hatutapiga hatua yoyote ile ya kimuziki.

Hii ni sawa na marehemu kanumba alivyoondoka na tasnia ya filamu TZ ingawaje alipokuwa hai watu walimponda sana huku wakimshutumu mambo ya uchawi, free mason nk.
 

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,623
2,000
Hawakuzingatia ushauri wake wa ' Kishirikina ' na sasa ' Kwishnei '. Akiwapa Hirizi / Tunguri wazibebe wakiwa ' Stejini ' wao hawataki kaona ' wanamchelewesha ' na sasa kabaki tu kwa Mpenda ' Ushirikina ' mwenzie Diamond Platinum na sasa ' Ndumba ' zao zinaelewana sana kama Sumaku za South Pole na North Pole.
Mbona unatuchanganya sie ambae hatujasikia kupitia hiyo Clouds? Ulichosema ni hiki:
Mimi hasa jukumu langu ni kuhakikisha nabeba Silaha zangu za Kiutamaduni natembea nazo kila ambapo Diamond Platinum anaenda kufanya Show yake ili niweze kumvutia Mashabiki wengi na pia wazidi kumpenda.
Kwamba, yeye kazi yake ndo hiyo ya kubeba matunguri! Mara ghafla unageuka na kusema:
Akiwapa Hirizi / Tunguri wazibebe wakiwa ' Stejini ' wao hawataki kaona
Kwanini na hao asiwabebee basi?! Au kwanini asiwabebee akina Chege & Temba? Kwanini asiwabee Six Sisters?! Hayo yote ni makundi anayoongoza mwenyewe tofauti na kwa Diamond ambako alikaribishwa tu!

Na vipi kuhusu Pemba mbona hajaenda kama kazi yake ni kwenda kila Diamond anakofanya show?
 

Valentina

JF-Expert Member
Oct 12, 2013
22,343
2,000
Huyo jamaa kulikua na tamasha leaders club lilikua organized na THT/clouds ..mvua na wingu zito likatanda mchana kweupe...RG akamuita akiwa yuko frustrated akamuuliza 'show itaharibika na mvua inashuka..we unafanya kazi gani hapa' jamaa (Fella) akaondoka chemba aliporudi wingu lilikatika na show ikapigwa..(Nilikuwepo) we jiulize MTU hata caption zake za insta kuandika hajui eti nae anatunga 'by-laws' za wakazi wa TMk..
Kwahiyo kumbe anahusika na mambo haya mbadala sio
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom