Exclusive: Mkubwa Fella asema Yeye ndiyo humbebea Hirizi na Matunguri Diamond Stejini

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,844
2,000
Akizungumza kwa kujiamini kabisa na mikogo yote unayoijua Wewe Meneja mzoefu wa Wasanii maarufu na wakubwa nchini Tanzania na Diwani wa Kata ya Kilungule kupitia Chama cha Mapinduzi Said Fella ( Mkubwa Fella ) amesema kuwa Yeye Kazi yake kubwa kwa Diamond ni kumvutia tu mashabiki wengi Ukumbini kwa kutumia ndumba / ushirikina ambao amesema kuwa si tu amebobea bali ametukuka nao kabisa.

Maneno haya ameyatoa mubashara leo hii Siku ya Jumamosi tarehe 16 mwezi Septemba alipokuwa akifanya mahojiano na Watangazaji wa Kipindi cha Clouds tv 360 on Saturday akina Ceaser ( Siza ) na mwenzake Gibson.

Swali la Mtangazaji Siza kwa Mkubwa Fella lilikuwa kama lifuatavyo..." Tafadhali Mkubwa Fella hebu tuambie Wewe majukumu yako makuu hasa kwa Mwanamuziki Diamond Platinum ni yapi kwani Watazamaji na Watanzania kwa ujumla wangependa sana kujua ".

Majibu ya Mkubwa Fella yalikuwa yafuatayo... " Kicheko kikubwa kilianza na akasema unajua pale tupo Watu kama Watatu hivi Mimi Fella, Babu Tale na Meneja Salam na wote tuna majukumu yetu ila Mimi hasa jukumu langu ni kuhakikisha nabeba Silaha zangu za Kiutamaduni natembea nazo kila ambapo Diamond Platinum anaenda kufanya Show yake ili niweze kumvutia Mashabiki wengi na pia wazidi kumpenda. Kwa Sisi Waafrika hasa Watanzania haya mambo siyo mageni na yanafanyika mno tu ".

Hata hivyo katika hali isiyo ya kawaida na iliyoonyesha kwamba kweli Mkubwa Fella ni Mtoto wa Mjini hasa na pengine ndiyo maana anaishi kwa Masela na Wajanja Temeke alipotakiwa kutolea ufafanuzi hiyo kauli yake ya mwanzo kwa mshangao mkubwa sana pale pale aligeuza maelezo yake ya awali na kusema hivi namnukuu..." Hapana siyo kwamba labda namaanisha kuwa namfanyia Ushirikina / Ndumba Diamond Platinum ili ajaze Watu Ukumbini bali nilichomaanisha tu ni kwamba Mimi huwa nahakikisha kwamba kule kote ambako Diamond Platinum anaenda Kupafomu nakamata Marafiki zangu walioko huko na kisha nawajaza upepo / nawatia sana ndimu kwa kuwaambia wahamasishe Watu wa huko waje kuingia katika Shows za Mwanangu na ndiyo maana unaweza kuona kila Show ya Diamond Platinum huwa kunakuwa na Nyomi la Kufa Mtu ".

Mwisho nadhani leo Diwani wa CCM Kilungule na Meneja wa Wasanii Said Fell ( Mkubwa Fella ) amehitimsha rasmi ule mjadala wa kwamba Msanii Diamond Platinum ni mpenda ' Shiriki / uchawi ' kwani Yeye kama Meneja wake tena wa siku nyingi ' amekiri ' kuwa ndiyo humbebea matunguri na hirizi zote ili aweze kumjazia Watu / Mashabiki Ukumbini.

Akhsante sana Mkubwa Fella.

Nawasilisha.
 

Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,797
2,000
Huyo jamaa kulikua na tamasha leaders club lilikua organized na THT/clouds ..mvua na wingu zito likatanda mchana kweupe...RG akamuita akiwa yuko frustrated akamuuliza 'show itaharibika na mvua inashuka..we unafanya kazi gani hapa' jamaa (Fella) akaondoka chemba aliporudi wingu lilikatika na show ikapigwa..(Nilikuwepo) we jiulize MTU hata caption zake za insta kuandika hajui eti nae anatunga 'by-laws' za wakazi wa TMk..
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
43,844
2,000
Sawa, ila huyu Fela ana wasanii wengi sana anawasimamia au hizo tunguli zinafanya kazi kwa diamond peke yake? Nitamwita afanye hiyo kazi pia kwa Bestinaso akajaze ukumbi London.

Kwa mujibu wa ' Washirikina ' wanasema kuwa kawaida ' Uchawi / Ndumba ' huwa hauvuki / haivuki Bahari.
 

cocochanel

Platinum Member
Oct 6, 2007
25,367
2,000
Duh!!!
Hayo nini tena.. aiseeeeee

Ukipata kideo turushie... nitachungulia kwa channel yao youtube labda watarusha..duh!!!
 

Super Handsome

JF-Expert Member
Jul 16, 2013
3,797
2,000
Huyu mkubwa fella mkewe ndo yule mtumia maji ya betri?. Kqa uchawi wake ni kiboko haswaaa.

Diamond aache kujipaisha kuwa anamtegemea Mungu kumbe tunguli za mkubwa fela na fuvu la binadam
Dada ana chekesha bila kujijua..in short ni serious comedian!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom