JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,012
Salaam,
Ndg. Tundu Lissu ni mwanachama wa JamiiForums tangu 2010 akitumia jina halisi.
Kwa sasa, Lissu ni mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA; hivyo akiwa kama mwanachama mkongwe wa JamiiForums na mtumiaji mkubwa mitandao mingine ya kijamii, ameamua kutenga muda wa saa 2 kujibu maswali mbalimbali ya wadau kupitia hapa jukwaani.
Mada hii ni maalum kwa ajili ya kuweka maswali ambayo atayajibu kesho tarehe 15 Oktoba, 2020 kuanzia saa 2 hadi 4 asubuhi. Ameahidi pia kupokea ushauri wa wadau.
Tunakaribisha maswali yenye kulenga kujenga Tanzania yetu bila kumkashifu wala kumvunjia heshima yeyote (be objective). Maswali yanaweza kujikita katika nafasi yake kama mgombea urais au safari yake ya kisiasa kwa ujumla.
NOTE: Wagombea Urais wengine pia wako huru kutumia jukwaa hili kuufikia umma wa Watanzania na jitihada zinafanywa ili wafikiwe wote ikiwezekana.
ILANI: Maswali yamekusanywa ya kutosha, mgombea ametumiwa maswali hayo na atayajibu kadiri muda utakavyoruhusu.
Mjadala huu umefungwa