Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.
Mh Lissu
Swali: Suala la kupita bila kupinwa limeonesha kuwachukiza watu wengi, endapo utakuwa rais wa Tanzania utalitatuaje?
 
Mh Tundu Lissu, kuna fufunu za mawakala wa upinzani kununuliwa ama wakikataa basi siku moja kabla ya siku ya uchaguzi au usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi wanakamatwa na askari police wanalala vituoni hivyo kushindwa kuwepo vituoni siku ya uchaguzi

Swali
Je, mmejipangaje na udhalimu wa aina hii au unaofanania na huu ?
 
Mheshimiwa TL, kwanza kabisa nikupongeze kwa kazi nzuri unayoifanya, unatuhamasisha sana na sisi vijana hakika tutafuata nyayo zako.

Kitu kikubwa kinachobana wapinzani ni katiba ambayo inam favor sana Rais.
Kwasababu yeye ndo anaechagua wasimamizi wa kura(NEC), je ikitokea umeshinda kiuhalali ila wakakuibia, utafanya nini mkuu?

Je, umejipanga kubadilisha katiba ya nchi iwapo ukishinda ili hizo nguzo tatu za serikali zifanye kazi bila kuingiliana?
 
In africa with power you can change everything,hivyo utakuwa amejibu maswali mengi ya wadau hapo juu?

Ni wazi Watanzania wengi pamoja na wana CCM wapo tayari kukupa Lissu kura lakini hawapo tayari kukaa kuzilinda hizo kura.

Mfano mzuri ni Km kwenye hii engua engua ya wagombea ambapo zaidi ya mabunge na madiwani 650 wameunguliwa na hamna wananchi wowote waliochukua action against it?

Swali, nyie kama viongozi wa CHADEMA mtatumia njia gani watu walinde hizo kura?
 
Mheshiwa mimi nashauri kwakuwa mwaka 2015 kwa mujibu wa tume CCM ilipata kura nyingi kanda ya ziwa. Nakuomba uweke nguvu sana maeneo hayo.

Pili, haya maeneo yote ambayo JPM hataweza kufika jitahidi ufike uyakamate kwani njia nyeupe kwenye maeneo hayo.

Halafu weka nguvu uchukue Morogoro, Zanzibar, Lindi na Mtwara , Mara,Pwani na Dar , Arusha, Singida, Kilimanjaro , Kigoma,Mbeya na Iringa.

Yale maeneo ambayo mlipoteza 2015 jitahidi ufike mwenyewe.

Hapo itabakia Tanga , Dodoma na Tabora ambazo naamini mtaziwekea mpango wake maalum.

Ningependa pia kuona video fupi za kusambaza social media uongee na wapiga kura zikiendana na count down ya kuelekea kwenye uchaguzi hadi siku moja kabla.

Mwisho naomba mtoe list ya wagombea ubunge wote wa CDM nchi nzima wapangwe kimkoa isambazwe kwenye mitandao ili wajulikane. Mkiweza iwe printed hard copy watu wapewe especially mikoani.

Mwisho naomba tujitahidi kuchangia kampeni ili Mheshimiwa afike maeneo mengi zaidi.

Ahsante.
 
Conglat Hon Lissu kwa kuwa Presdn candidate.

Naongeza uzito wa swali no 81 (1)

(a)Je, ktk serikali ya CHADEMA ukiwa Rais kuna mkakati wowote wa kuhakikisha kwamba watu wenye taaluma, (mafundi) kwa ujumla wao (wetu) wanafanya kazi zao kila siku kama wafanyakazi wengine wa serikali, huku wakiwa chini ya menejiment ya serikali na kuliingizia taifa kipato huku nao wakilipwa mishahara kila mwezi kama wafanyakazi wengine?

(b)Na kama hakuna mkakati, je huoni kama ni muhimu kufanya hivyo kwa kuwa hii ni sekta muhimu sana ktk nchi kwa kuwa mafundi wana kazi za kujenga mandhali ya nchi ktk sekta zote?


Asante.
 
Mheshimiwa Tundu Lissu mimi ninamaswali na nrrinaomba kupata majibu toka kwako;-

Ninaomba unichambulie vyema juu ya sera yako ya maendeleo ya watu.
Kwa upande wa :-

1.) Elimu;
Maendeleo ya watu au mwanafunzi ni katika muktadha upi hapa sababu ninachojua mimi ni kwamba ili mwanafunzi apate elimu bora na yenye tija kwanza nikatika ujenzi na uwezeshaji wa vifaa na miundombinu itakayomfanya mwanafunzi asome vizuri na apate elimu bora ambayo CCM ndicho wanachokifanya sasa.

2.) Afya
Sera ya maendeleo ya watu inakuwaje kuwaje kwa hapa bila miundombinu rafiki na upatikanaji wa huduma za kiafya.

N.k

-> Nimesikia kuna watu wanasema, maendeleo ya watu ni kuhakikisha serikali inawafanya wananchi wapate pesa Kisha wao ndio wataleta miundombinu au maendeleo ya vitu hii imekaaje kwa wewe kimtizamo wako Kama kiongozi..?

Asante 🙏🙏
 
Swali:- ni hatua gani zinafaa kuchukuliwa Kwa mujibu wa sheria za tume Kwa polisi aliemhakikishia Mbowe hatashinda ubunge kwa vyovyote vile???
 
Swali,
Wafanyakazi WA UMMA, walioondolewa kazini pasi na malipo eti kwa kuwa na vyeti feki, unampango wa kuwarudisha kazini au kuwalipastahiki zao?
 
Pole na hongera kwa kazi kubwa unayoendelea kuifanya. 1. Kama Taifa tuna uhitaji mkubwa wa katiba mpya, nini utafanya juu ya hili pindi tu utakapo shika dola mapema baada ya octoba 28?
 
Habari Mh Lissu? Pole kwa kampeni.

1. Naomba kujua umejipanga vipi kutatua tatizo la ajira nchini, tatizo linalohathiri vinana wengi sana.

2. Kutokana na uvunjifu wa sheria na haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi, je Serikali yako itakua tayari kufumua hili jeshi na kuliunda upya? Je utachukua hatua gani kwa viongozi wa hili jeshi endapo ukichaguliwa kuwa Rais?

3. Ni muda mrefu tumeona taasisi yetu nyeti (Usalama wa Taifa) ikijikita kwenye mambo ambayo hayasaidii taifa. Je unampango gani juu ya hii taasisi tunayoitegemea katika kusimamia nyanja zote za kimaisha?

4. Je, utatumia adhabu ya kunyonga mpaka kufa kwa viongozi wote mafisadi, walioidhinisha watu kutekwa, kuteswa na wengine kuuwawa?
 
Hellow Hon. Tundu A. Lissu

Mimi ni mmoja wa wanafunzi wa chuo Cha taifa Cha utalii, ingawa kwenye sector ya utalii ajira zipo Ila wengiwao wanaajiliwa makampuni binafsi, na tunaangalia dhahiri serikali inajali Sana sector za elimu, afya kwa upande wa ajira, me Ni shahidi mwaka Jana nikaenda field wenzangu niliomaliza nao waliochaguliwa.

Vyuo vya Ualimu wanapojiandaa kwenda field Kuna hela inaandaliwa na serikali Ili kuwapa wakajikimu na mahitaji Ila Cha kushangaza mimi na wenzang tuliochaguliwa hiki chuo bila ridhaa yetu hatukupew hela ya field inakuwa gharama kwa wazaz wet, je Ni haki??

Halafu, nifafanulie utafanyaje ili kila sector ipate haki kwa upande wa ajira serikalin? Pia kuhusu field, utaweza kutenga fungu Hasa kwa wanaochaguliwa vyuo baada ya matokeo ya form 4 bila ridhaa yao?

Swali langu laweza kuwa refu sana Ila ndo kura yako ukinijbu kwa ufasaha nkaridhika
 
Mheshimiwa Lissu vitendo vinavyofanywa na vyombo vya dola mfano kuvamia mikutano, kuharibu vyombo vya mziki ni hatua zipi mnazichukua kukomesha hayo kabla ya uchaguzi 28/10?
 
Swali langu: Mmejipangaje kulinda kura zisiibiwe? Iko wazi mchezo umeshatengenezwa upo wazi kwa wakurugenzi kuhakikisha CCM inatangazwa mshindi?

– tumechoka jamani maisha magumu sana tubadilishe serikali
 
Mheshimiwa Tundu Lissu, pole kwa changamoto unazopitia na hongera kwa kuwa na moyo wa kuendelea kupambana kwa ajili ya HAKI.


maswali yangu
1. Endapo ukishinda na kuwa rais wa tanzania, je utaunda mfumo gani huru ambao utasimamia swala la uhuru wa kuongea/au kutoa maoni na uhuru wa vyombo vya habari?kwa kipindi chote cha urais wako na hata baada ya muhula wako kumalizika.

2. Kwa mujibu wa katiba yetu,mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na wasimamizi wa chaguzi kwenye majimbo wanateuliwa na rais,hali hii inaweza kuleta mazingira ya upendeleo kwa chama tawala kipindi cha uchaguzi. Je, Utatumia mfumo gani ili kutengezeneza mazingira ya usawa wa kidemokrasia na uchaguzi huru na haki kwa vyama vyote wakati wa chaguzi.
 
Mh Lissu unaelewa fika wahafidhina wako wamejipanga kikamilifu kuiba kura zako, wewe na Chama mmejipanga vipi kudhibiti hili pamoja na kuhakikisha mawakala wenu hawanunuliwi? Pia ukithibitisha kura zako zimeibiwa ni hatua gani umepanga kuchukua?

Ahsante
 
Mhe.Lissu

Ni kwa namna gani tunaweza kutenganisha maendeleo ya WATU na Maendeleo ya VITU!? Kwanini tusiamini kuwa hivi vinategemeana!?
 
Mh Tundu Lissu nina maswali
a) Je, matokeo ya baada ya uchaguzi yakitoka na huja fanikiwa kupata urais utakubaliana na tume? Na kama hapana utachukua hatua gani?

b) Ukifanikiwa kupata urais unatuahidi nini vijana tuliokosa ajira hali ya kuwa tuna taaluma mbalimbali zinaishia mtaani bila kutumika ipasavyo
 
Ndg mheshimiwa,

a) naomba kuuliza ni miradi gan ya serikali utaiendeleza au kuistisha kwa faida ya wana jamii.

b) vipaumbele vyako katik taifa hili ni vipi haswa?
 
Status
Not open for further replies.
124 Reactions
Reply
Back
Top Bottom