Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.

kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
2,246
2,000
Sote tunajua tume ya uchaguzi imewekwa mfukoni na CCM. Swali:
(A) Umejiaanda vipi kukabiliana na hujuma za uchakachuaji wa kura zako?

(B) Ikithibitika dhahiri kama hujuma zimefanyika ktk kupiga kura na kutangaza matokeo. je; ni hatua zipi umejiandaa kuhakikisha haki yako inapatikana? (Maana matokeo hayahojiwi mahakani)
 

RWANDES

JF-Expert Member
Jun 12, 2019
493
1,000
Mheshimiwa tundu lisu swali langu la

1) Kilio cha wafanyakazi kutopandishwa mishahara na madaraja yao utakishughulikia vipi?

2) Je, miradi ambayo atakuwa ameiacha raisi magufuli utaiendeleza au utaiacha kwa kuwa we siyo mumini was mawndeleo ya vitu?

3) Ikumbukwe kuwa serikali iliingia mkataba madini na kampuni ya uchimbaji madini ya barrick gold mine ya kupata 50%kwa 50% kwa faida itakayokuwa inapatikana hadi sasa tuna kampuni ya TWIGA GOLD MINE LTD! Je mkataba huu utauvunja au utaendeleza?

3) Serikali ya CCM imekuwa ikisomesha watoto wetu elimu bure kuanzia chekechea hadi kidato cha nne je sera hii utaifuta na kuwa na mlengo wako katika kuendesha serikali?
 

GIRITA

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
2,776
2,000
Ndugu mgombea mambo vipi?
Pole na harakati za kampeni.

Iwapo utachaguliwa kuwa raisi utarudisha shughuli za kubadilisha fedha za kigeni mikononi mwa wananchi waliotaifishwa na serikali ya sasa na kuyapa uhalali mabenki kufanya shughuli hiyo?

Je, Utatumia njia gani kukomesha utakatishaji Wa fedha nchini?

Umeandaa mkakati gani Wa kuwainua wafanya biashara wadogo wadogo katika mustakabali Wa kuboresha maisha ya mtanzania Wa kawaida tukienda sambamba na maendeleo ya watu na sio vitu?

Je mtashirikiana bega kwa bega na chama ACT wazalendo katika kuunda serikali iwapo utashinda kiti cha urais?
Maana wameonesha kuwaunga mkono wazi wazi.

Na vipi kuhusu muungano akishinda maalim self Zanzibar na wewe ukashinda bara utavunjika?
 

KEUZ

New Member
Dec 29, 2014
2
45
Mheshimiwa.

1. Mnaona mna mikakati yoyote ya kuweza kudhibiti hujuma za kuanzia upigaji kura na matokeo ya kila ngazi ? Kama ipo inaweza kuelezeka ? Maana tunaona hujuma ni nyingi sana

2. USHAURI

Kwa siku zilizobaki, hakikisheni wagombea wenu wanalindwa na umati mkubwa wa watu jasiri sana, itasaidia.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,609
2,000
Ushauri iwapo utakuwa rais wa nchi hii, fungua mahusiano na nchi za Scandinavia yaani Sweden, Denmark, Norway na Finland.

Nchi hizi zina technoligia nzuri na sio nchi wanyonyaji, bali wenyewe hutaka kufanya kazi na nchi zenye uwazi na utawala bora. Wakati nakua nilikuta mashirika ya DANIDA, NORAD, FINIDA nk yakifanya ushirikiano wenye tija.

Nina hakika nchi hizi zitaweka nguvu zao kwenye kilimo cha kisasa, sekta ya afya, elimu ya ufundi na ujasiriamali, itayopekea kufungua viwanda vidogovidogo ili kukabiliana na hili tatizo sugu la ajira.

Nyerere alifaidika sana na mataifa haya ya Nordic, maana mikopo na misaada yao haina masharti magumu, na mingi ya misaada yao inalenga zaidi kwenye maendeleo ya watu. Sumu ya wazungu hawa ni utawala wa kihuni usiojali uwazi na kujali demokrasia.

Nina uhakika kwa kushirikiana na nchi hizi uchumi watu utaamka kwa kasi ya ajabu.
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,357
2,000
Mh Lissu, Sera kuu iliyoko kwenye Ilani ya CHADEMA, 2020, chama kilichokupa dhamana ya kuwa mgombea Urais ni Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu.

Kwenye hiyo Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2020 (Uk. 2), mmenukuu falsafa ya Baba wa Taifa ya Ibara ya 28 ya Mwongozo wa TANU wa mwaka 1971, kwamba; Kwa watu ambao walikuwa watumwa, au ambao walikuwa wakionewa, wakinyonywa, na kunyanyaswa kwa sababu ya Ukoloni, Ukabaila au Ubepari, “Maendeleo” maana yake ni “Ukombozi”.

Kitendo
chochote kinachowapa uwezo zaidi wakuamua mambo yao wenyewe, ni kitendo cha maendeleo, japo kama hakiwaongezei afya wala shibe. Kitendo chochote kinachowapunguzia uwezo wao wa kuamua mambo yao wenyewe na kutawala maisha yao
wenyewe, si kitendo cha maendeleo,ni kitendo cha kuwarudisha nyuma, japo kama kitendo chenyewe kinawaongezea afya na shibe kidogo.


SWALI:
Ni nini tafsiri sahihi na yenye uhalisi, nyakati hizi za Utandawazi, Soko uria, ili kuwaondoa maadui watatu (Umaskini, Maradhi na Ujinga) katika jamii?

SWALI:
Kwenye kampeni zako, na hata msimamo wa CHADEMA, Serikali ya CCM kwenye miaka 5 inayoisha, imeleta maendeleo mengi, ambayo mnadai ni "maendeleo ya vitu", je, mna Sera gani za kuondoa hao madui watatu katika jamii?

Ilani ya CHADEMA, imesheni mapendekezo ya mikakati mingi inayohusu "maendeleo ya vitu" kurasa za 56; 70; 72; 84 na 89.

SWALI:

Ni wakati gani wa kampeni utaongelea hayo, kwa msingi kwamba tayari kuna kiasi cha maendeleo ya vitu? Au mpango wa Serikali yako ni kuanza upya, na miradi iliyopo ikawekwa kando?

Utanisamehe kukuuliza maswali yafuatayo yanayogusa maisha yako binafsi:
1) Wewe ni muuamini wa dini? Kuna uthibitisho gani kuwa unaamini na kuishi kwa maandiko matakatifu?

2) Una jambo gani la kitaifa, lenye uzito mkubwa, umelifanya uweze kuaminika kukabidhiwa maisha ya Watanzania zaidi ya milioni 60?

3) Maisha yako yote umekuwa huheshimu mamlaka na kwa maneno na vitendo unadharau, je, ukipewa madaraka makubwa ya Urais, unauthibitishaje WaTanzania, hutokuwa dikteta mwenye dharau ya kiwango cha juu kisicho na mfano katika dunia hii?
 

Diba

JF-Expert Member
Jan 11, 2013
1,519
2,000
Umekuwa ukizungumzia haki za watumishi wa umma ikiwemo mishahara na kupandishwa vyeo/madaraja,mbona huzungumzii swala la uhamisho ambalo pia limebeba haki za watumishi, ikiwa toka 2018 uhamisho uliokuwepo kisheria umezuiliwa?

Serikali yako inampango gani kwenye swala hili la uhamisho?n.b asante sana kwa kusimama na watumishi wewe ndio mgombea pekee na chama chako mlioibeba ajenda ya watumishi kwa uzito wake tangu mwanzo wa kampeni.
 

Veto

Member
Apr 23, 2020
25
95
Mh.Lissu,raisi wetu ujae Pole na hekaheka za kampeni;

Swali:Una msimamo gani kuhusu ujenzi wa kiwanda au viwanda katika mkoa au kanda husika kutoka na malighafi yanayopatika mkoa husika?
mfano;Kanda ya ziwa-Pamba, kahawa
na samaki
Iringa-Mbao
Kigoma-Chumvi..
Simiyu,Shinyanga na Manyara-Ng'ombe
Singida-Alzeti n.k
 

rwamuli

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
879
1,000
Mh.. mimi nina maswali mawili,

i) Mawakala tume inadai kuwa hawatoruhusiwa kuingia na simu. Sasa kama itatokea fomu inaonesha umeshinda halaf hawataki kumpatia nakala umejipangaje?

ii) Tumeanza kuona kamatakamata imeanza je tumejiandaaje kuwasaidia hawa mawakala na wabunge wetu ambao wengi walikuwa wanawindwa kipindi cha kurejesha form. Wasije wakatekwa usiku kabla ya kupiga kura na baada?

iii) Ushauri wangu: kama inawezekana kwa kila wakala angalau akawa na kifaa cha siri cha kurekodia matukio yote yatakayo kuwa yanafanyika kituoni, kwa nchi nzima kama ushahidi. Wavae hata kweny shati.

Mungu azidi kukupigania kaka.
 

Lubengera

Senior Member
Jun 21, 2019
160
250
Hongereni Mgt ya Jamii forum kwa kufanikisha hili.

Mh. T.A L, Pole na hongera kwa hatua uliyofikia Hadi Sasa katika kampeni zako, na ni ukweli uliowazi, unaonekana kuungwa mkono na wafuasi wako kadri walivyoweza.

Je,

Hatua gani umeandaa kuchukua hasa kipindi cha uhesabuji wa kura pamoja na kutangaza matokeo? hi ni kwakuwa mpaka Sasa :-

1. Tume ya Taifa ya uchaguzi imeshatoa mashart ikiwemo kutoingia na simu katika chumba Cha kupigia Kura

2. Jeshi la Polisi TANZANIA limeshatoa maelekezo kuwa baada ya kupiga kura wananchi wote wanapaswa kutawanyika kutoka katika vituo vya upigaji Kura

3. Kuna uwezekano mkubwa sana siku ya upigaji Kura kusiwepo na internet na hivyo matokeo yakachelewa kufika na ikawa rahisi kufoji

4. Tume ambayo inamlaka ya kutangaza matokeo, imeonesha kulalia au kutosikia malalamiko ya Upande wa chama chako na hivyo upo uwezekano mdogo sana wa Tume kutangaza wewe endapo utashinda

5. Inaonekana kutakuwa na ugumu wa kupata nakala ya fomu ya matokeo, kwakuwa, tume inao uwezo wa eidha kuitoa au kutoitoa kulingana na Sheria husika na upatikanaji wake.

Nitashukuru endapo nitajibiwa maswali hayo.
 

chamilo nicolous

JF-Expert Member
Mar 10, 2016
1,487
2,000
1.Umekuwa ukilaani uwanja wa ndege kujengwa Chato na mbuga ya hifadhi kuwekwa Burigi. Je, ukiwa rais utaihamisha?

2. Unamnadi rais J J Magufuli kuwa ana ukabila, wewe wakati unampendekeza Dada yako nafasi ya ubunge viti maalumu na Mbowe akampitisha mtoto wa Mtei, sio ukabila na ubinafsi?

3. IMMMA ni kampuni inayotetea mikataba ya wazungu, Je uzalendo wako uko kwenye nini?
 

Haparahatu

Member
Jan 23, 2020
27
45
Mh Tundu Lissu naomba nitoe shukrani kwa kutupa nafasi hii ya kuuliza maswali. Mimi ni katika watu ambao wanakuunga mkono na ningependa utoe ufafanuzi katika maswahili yafuatayo:

1. Serikali ya awamu ya tano imeanzisha Miradi mikubwa sana kama SGR na Nyerere Hydropower Dam. Mikopo ambayo serikali imechukuwa katika miradi hii itagharimu pesa nyingi sana na pia itakuwa ni deni kubwa katika vizazi vijavyo. Kwa vile mfumo uliotumika ni kwamba serikali inagharimia kila kitu, Je ukiwa Rais unabadilisha mfumo wa mikopo (Public/Private partnership) au utaendela kama ilivyo sasa hivi.

2. Serikali ya awamu ya 5 imedorora sana kidiplomasia. Imekuwa ikijenga hoja kwa kuita nchi za nje kama wao ni mabeberu na pia kuwekwa katika travel ban na marekani. Balozi zetu za nje pia ziko hoi hata ukienda unakuta wana brochure za Tanzania za mwaka 1997 wakati sasa tuko 2020. Je una mikakati gani ya kuimarisha uhusiano wetu na nchi za nje.

Asante.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom