Uchaguzi 2020 EXCLUSIVE: Maswali kwa Mgombea Urais wa JMT, Tundu Lissu kutoka kwa Watanzania watumiao mitandao ya kijamii

Status
Not open for further replies.

baracuda

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
1,222
2,000
Vipi kuhusu fao la kujitoa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, unalizungumziaje? Na je, unakubaliana na mpango wa wanufaika kutakiwa kusubiri mpaka miaka 55 ndio wachukue?
 
  • Thanks
Reactions: JRK

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
4,611
2,000
Mhe. Lissu umekuwa ukionyesha mojawapo ya madhaifu ya serikali ya awamu ya 5 ni kuweka kipaumbele katika maendeleo ya vitu baadala ya watu, na umekuwa ukiongelea miradi mbali mbali ambayo imeshaanzwa kutekelezwa na serikali hiyo.

Je, kama ukipata Urais hiyo miradi utaifuta au kutakuwa na muendelezo wa miradi hiyo kutokana na gharama tulizokwisha ingia kama walipa kodi na nchi kiujumla ?
 

TWisheshagi

Member
May 2, 2020
14
100
Mheshimiwa, HONGERA kwa kampeni. Swali: Kwakuwa katiba yetu haitoi fursa ya moja kwa moja katika kukabidhi madaraka kwa Chama kingine tofauti na CCM!

UPI MTIZAMO WAKO JUU YA MGOGORO WA KIKATIBA UNAOWEZA KUJITOKEZA ENDAPO UTACHAGULIWA KUWA RAIS WA NCHI YETU?
 

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,182
2,000
Utakaposhinda uchaguzi, je utaendelea kuhudhuria mahakamani kisutu kwa zile kesi zako za kubambikiwa??

Bila kujali ni namna gani mahakimu watavyokuwa wanatetemeka wakati wa kuendesha kesi hizo.
 

mkulima gwakikolo

JF-Expert Member
Nov 22, 2014
1,192
2,000
Mhe. Lissu umekuwa ukionyesha mojawapo ya madhaifu ya serikali ya awamu ya 5 ni kuweka kipaumbele katika maendeleo ya vitu baadala ya watu, na umekuwa ukiongelea miradi mbali mbali ambayo imeshaanzwa kutekelezwa na serikali hiyo. Je kama ukipata Urais hiyo miradi utaifuta ? au kutakuwa na muendelezo wa miradi hiyo kutokana na gharama tulizokwisha ingia kama walipa kodi na nchi kiujumla ?
Kwenye miradi mingi kumefanyika siri kubwa. Na hili lazma lilieleweke wazi kuwa wananchi ambao ndy wenye pesa lazma serikali yetu ikaweke wazi mikataba hii na mikataba yenye maslahi Duni kwa Taifa itawekwa wazi ili chombo cha wananchi ambacho ni bunge kitathomin kitoe maamuzi sahihi kwa maslahi mapana ya Taifa Letu.
 

Peter Madukwa

JF-Expert Member
Sep 20, 2012
473
1,000
Nina maswali mawili

1. Ukifanikiwa kushinda kiti cha Urais; Je katika siku 100 za mwanzo wa uongozi wako utafanya mambo yapi?

2. Naomba kuelezwa kuhusu mfumo wa majimbo unaotarajia kuutumia na namna utakavyofanya kazi na kwa jinsi gani utaleta tija kulinganisha na huu wa sasa

Natanguliza shukrani na kila la heri ktk harakati za uchaguzi mkuu
 
Nov 26, 2014
48
95
1. Mh Lissu unaweza ukaelezea ni kwanini uchaguzi wa mwaka huu (2020) umeuita kama uchaguzi wa kufa na kupona ?

2. Moja kati ya nyimbo za kampeni zako unasema "Lissu tuvushe" kwa nadharia hiyo hiyo kwanini Lissu na sio Mtetezi wa Wanyonge John Pombe Magufuli?

3. Kauli ya "Lissu ni kibaraka wa mabeberu" kauli hii unaitafsiri vipi kwako kama mgombea wa CHADEMA na mgombea katika taifa lenye rasirimali nyingi kama Tanzania?

4. Kauli ya "CCM= Uchaguzi huu ni mwepesi mno kutokana na mgombea wetu alivyoweza kusimamia vyema rasirimali za taifa, kajenga tanzania ya viwanda , katengeneza ajira kedekede, kajenga uwajibikaji ndani ya serikali" kauli ya CHADEMA= Uchaguzi huu ni mwepesi mno kutokana na sera zetu za uhuru, haki na maemdeleo ya watu.....kauli hizi mbili tofauti zina maana gani kwako kama mgombea dhidi ya mpinzani wako wa CCM?
 

the great boy

Member
Jun 10, 2013
9
45
Swali kwa Mh Tundu Lissu

Kuna wafanyakazi kipindi cha East Africa Community iliovunjikaga 1977 hadi leo wazee wa watu hawajalipwa staiki zao na wengine tayari walitangulia mbele za haki.

Je, tukikupa dhamana kama Rais Utatatuaje hili tatizo kwa kuwalipa Fedha zao walizozulumiwa na CCM japo kesi ipo Mahakama ya Afrika ya Haki za Bimadamu
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom