EXCLUSIVE: Katika hali isiyotarajiwa, Clouds yapiga rasmi wimbo wa Lady Jaydee baada ya miaka

Krikichino

JF-Expert Member
Oct 5, 2019
651
1,098
Habarini wakuu.

Leo mida ya saa nne kasoro katika kipindi cha Power Breakfast Kasoro Clouds imepiga rasmi wimbo wa Komando Jide Joto Hasira.

Kipindi hicho kilichoongozwa na Gardner Habash kilicheza wimbo huo mwishoni kabisa huku watu kama Adam Mchovu wakimtania Captain Habash kuwa amerudisha upya makazi kwa mpenziwe huyo wa muda mrefu Jide Jaydee.

Bila Shaka hicho kinaonesha wazi kuwa CMG na Jide Jaydee hawana tena bifu na mambo yapo shwari kabisa na ikibidi tutegemee mwanamama Jide muda si mrefu ikiwezekana aingie mjengoni kupiga na interview kabisa.

Swali ni je pia tutegemee the same reaction ya Clouds dhidi ya Wasafi? Au tuache waendelee na ishu zao.
 
Back
Top Bottom