Exclusive Interview with JamiiForums founder - Maxence Melo | Page 3 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive Interview with JamiiForums founder - Maxence Melo

Discussion in 'Great Thinkers' started by King'asti, Aug 18, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,220
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  Habari za wakati huu mabibi na mabwana, waungwana wote kwa ujumla, wale tulio kwenye mfungo, hongereni kwa hilo na natanguliza kheri na salamu za sikukuu ya Idi.

  Itakumbukwa kuwa Jumanne ya tarehe 14/08/2012 ilianzishwa hoja na Roulette na kukaribishwa maswali kwa ajili ya kumuhoji Maxence Melo juu ya JamiiForums kwa ujumla na safari hii ya miaka 6 toka kuanzishwa kwake (Link to Roulette's thread). Ikumbukwe kuwa JamiiForums imekuwa maarufu nchini Tanzania, kitu ambacho kinaipa changamoto za kutosha. ni namna gani changamoto hizi zinashughulikiwa kutuhakikishia, sio tu ustawi; bali na uwepo wa JF katika siku za usoni.


  maxence-melo-01.jpg
  Maxence M. Melo
  Tulipokea maswali mengi. Mengine yakiwa marudio (Link to the latest interview of Maxence Melo). Tumejitahidi kuyaweka kwenye mtiririko muafaka kwa ajili ya kuokoa muda na kutengeneza picha halisi. Maxence Melo yupo hapa kuyajibu. Kamata kahawa yako, ama kinywaji chako baridi and stay tuned.
   
 2. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #41
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,596
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kusma 'sikuelewa' lakini nilijitahidi kujibu kwa nilivyoelewa. Ni kwa kuwa tayari suala la uboreshaji wa UI ya JF nilikwisha kuligusia hapo awali.

  Naam,
  Wanachama hawahawa ndio walipendekeza 'Premium Membership' iwe na kikomo ili JF ipate namna ya kujiendesha. Halikuwa pendekezo la mtu mmoja, ni wengi waliafiki hili hivyo nasi kutokana na kuona umuhimu wa kulifanikisha hili tukaanzisha utaratibu huu.

  Kiwango cha chini kwa mwaka (siku 365) ni TZS 20,000/- kiasi ambacho naamini mtumiaji wa JF kama kweli anaona umuhimu wa JF kuendelea kuwa hewani hakimshindi.

  Tukiwa 'serious' na kudhamiria kuiboresha JF na ikatuhudumia tunavyotaka basi walau wanachama 25,000 kati ya wanachama takribani 90,000 wakachangia 20,000 maana yake JF itapata walau TZS 500,000,000/- kwa mwaka; fedha ambayo ikipatikana ni wazi JF itaboresha mengi, itaanzisha gazeti na zaidi mengi ya mapendekezo yatafanyiwa kazi.

  Ni mapema sana kupata kusema kama mafanikio yapo makubwa, lakini yapo. Ndio maana mnawaona wenye hizo badges za Premium Membership.

  Inasikitisha, watanzania ni wepesi kusema lakini kutenda ni wagumu sana. Ukiiangalia TZS 20,000 ukaigawa kwa miezi 12 unaweza kuona ni kiasi gani mtu anakuwa katusaidia katika kuhakikisha tunamhudumia vema zaidi (TZS 1,667/- au US$1 kwa mwezi); sidhani kiasi hiki kinatushinda, ila ndio hali halisi, tunaongea na kutaka makubwa lakini hatupo tayari kuwa sehemu ya mabadiliko tunatoyataka.

  Ni wazo zuri, manake huyu hawezi kupata $1 kwa mwezi?

  Ingekuwa hivyo, wadau kama Nyani Ngabu, Rutashubanyuma n.k wangepewa huzo badges bure kwakuwa wana mabandiko mengi, lakini sidhani kama kiuhalisia yeyote anayetumia JF hawezi kupata $1 (ya ziada kuichangia JF) kwa mwezi.

  Ndugu zangu, tunahitaji kuwezeshwa ili tuwahudumie vema. Nakosa hata lugha ya kutumia ili watu wanielewe, nawashukuru wote ambao wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanatuchangia kwa hali na mali ili tuweze kutoa huduma hii. Kwa niaba ya wenzangu, tunashukuru sana.
  Premium Members hawana hisa, ni wanachama waliojitolea kuhakikisha wanaichangia JF ili iendelee kuwepo hewani. Mfano ni watu kama Pasco, Ritz, Edwin Mtei, ndetichia, Elli, Nyunyu, Kashaijabutege, Zogwale, Mwalimu, Kimbunga n.k na wengine ni wanafunzi. Wanapata/watapata nini baadae kama ziada, nisingependa kuliongelea kwa sasa (natumaini hutohoji kwanini, lol)
   
  Last edited: Jan 4, 2016
 3. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #42
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,248
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Bora tu ungezitaja ili ituvutie hata sie ambao tumevuliwa baada ya cheo chetu kuisha muda wake lol. Asante kwa majibu, swali linalofuata:-

  Swali # 14

  Imewahi gusiwa na baadhi ya members kwa wakati mbali mbali kuwa wangependa Jamii Forums ije iandae gathering kwa ajili ya members watakaopenda kukutana kwa pamoja hata bila kutoa ID zao wazitumiazo hapa JF. Unalipokea vipi hili? Imewahi tokea mkusanyiko kama huo?
   
 4. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #43
  Aug 23, 2012
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,596
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Waliowahi kuchangia ni wazi bado wataona umuhimu wa kuendelea kutuwezesha, hata hivyo safari hii tumepanga kuwanufaisha japo kidogo, sintoandika kivipi.
  Kuna mikusanyiko kadhaa imefanyika Dar na Arusha. Bado nasisitiza kuwa endapo wadau wanaamua kukutana, mtu anapoamua kui-disclose ID yake ya JF ni juu yake lakini ningeshauri watu kujiepusha kutaja IDs zao wala kujadili masuala ya siasa (labda pale inapolazimu).

  Hatujawa na mpango (kama JF) wa kuitisha mkutano lakini endapo wadau watatuhitaji kuwasaidia katika kuhakikisha hili linafanikiwa tutatoa ushirikiano. Wanaotaka kujua namna ya kufanikisha hili nashauri wawasiliane na PakaJimmy na Preta kwani wana uzoefu wa shughuli kama hizi.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...