Exclusive interview na Violeth Mzindakaya


M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
Exclusive interview na Violeth Mzindakaya Mjumbe wa NEC.

v-pictures-1-751273.jpg


wadau blog yetu ilifanikiwa kukutana na mjumbe wa nec violeth mzindakaya nyumbani kwake na kufanya naye interview ana yapi ya kusema juu ya maisha yake na siasa kwa ujumla?fuatilia interview hii kwa makini uje alichokisema mwanadada violet a.k.a sister v

swali: Tupe historia fupi ya maisha yako?

Violeth:naitwa violeth mzindakaya nimezaliwa tarehe 29/9/1977, ni mtoto wa 7 kuzaliwa katika familia yetu. Nimesomea elimu ya msingi katika shule ya bungo primary morogoro mpaka darasa la 3 ambapo baba yangu kipindi hicho alikuwa ni mkuu wa mkoa wa kigoma. Baada ya hapo nikamalizia shule ya primary kiezya iliyopo mkoani kigoma kwa bahati nzuri nikafaulu nikachaguliwa kwenda shule ya sekondari weru weru lakini kutokana na ile hali ya baridi sikuweza kumaliza kule nikawa nimehamishiwa kilakala sekondari school baada ya hapo nikamalizia shule ya loleza high school baada ya hapo nikafanikiwa kuingia chuo cha tanzania school of journalism nikachukua mambo yangu ya uandishi wa habari na utangazaji certificate nikamliza mwaka 1999, nilipomaliza pale mwaka 2000 kuanzia mwaka 1999 zile kazi zangu za research za chuo nilikuwa naandikia gazeti la mwananchi kipindi hicho ilikuwa imeanzishwa halafu radio nikaenda uhuru kumuona abubakari liongo. Nakumbuka assignment yangu ya kwanza pale mwananchi ilikuwa ni kwenda kutafuta habari na kipindi hicho mobitel ambayo kwa sasa ni tigo walikuwa wanabadilisha mfumo wa analog kwenda kwenye digital nikaenda kwenye press conference maelezo nikauliza swali likaonekana ni zuri nikatengeneza story yangu ikawa kubwa na kusababisha kesho yake kutolewa kwenye front page na kipindi hicho story yako ikitoka front page unalipwa sh elfu tano. Nikaendele na kazi yangu, nikakutana na taji liundi wakati huo radio times ndio imeanza wakati na mimi bado nilikuwa na umri mdogo nikaendelea kujipa moyo watu wakanipenda baada ya kuanza kuhit jijini ikapelekea jina langu kuingizwa moja kwa moja kwenye mashindano ya tuzo za watangazaji bora wa radio ambazo ziliandaliwa na mnet kwa waandishi bora na watangazaji bora wa radio, nikashangaa katika wale watu wa tano na mimi jina langu likapendekezwa pamoja na marehemu amina chifupa na sarah dumba. Nawashukuru wazazi wangu walinipenda sana wamenipa elimu lakini pia ni binti ambaye maisha ambayo ya kwangu zaidi nimesimama mwenyewe sanasana.

Swali: Ni kitu gani ambacho kilikuvutia kuingia kwenye siasa?

Violeth:kilichonivutia mpaka nikaingia kwenye siasa ni yeye mwenyewe baba yangu, pia mapenzi yangu ya dhati ndani ya chama ambacho naamini kwangu mimi kimenilea kimenikuza mpaka nilipofikia hapa, na malezi ambayo nimekulia ni yaki siasa pili ilikuwa ndani yangu mimi mwenyewe kwamba naweza siku moja nikawa mtu fulani, jambo hili limeenda limekuwa mpaka limejenga mizizi ndani ya mwili wangu na hatimaye nimefikia hapa lakini pia naweza kusema ni wito ambao mwenyezi mungu pia nasema ameyapanga haya maisha kuna watoto wengi ambao wazazi wao hawako kwenye siasa lakini wao ni wanasiasa niseme tu hilo limenisaidiwa kuwa mwanasiasa mimi kama violeth na baba yangu anapata uraisi wa kunisaidia kulikoni ningesema nimuige pasipo mimi kuwa na uwezo ule ushawishi na ndoto ya mimi kuwa mwanasiasa ingenipa kazi sana ningemsumbua baba yangu lakini kwa sasa hivi simsumbui kwa sababu anajua kwamba violeth anajua anachokifanya.

sister-v-pic-3-722127.jpg


violeth mzindakaya akielekeza jambo wakati wa interview.

swali: Je utaweza kuwa mpiganaji katika siasa kama baba yako manake baba yako ni mkongwe katika siasa toka enzi za hayati mwl.nyerere?

Violeth:kwanza mpaka hapa ni mpiganaji kwa sababu nimejitahidi sana kumwangalia baba yangu nini anakifanya, mzee mzindakaya amefanya kazi na ana historia kubwa sana sina haja ya kuielezea kila mtu anatambua. Ni mkongwe ndani ya chama na ni mkongwe katika uongozi wake kisiasa naendelea kusema kwamba sitaki kumwangusha yale yote aliyoyatenda mema mimi nitachukua kama yalivyo na kuyaendeleza kama binti yake ambaye naamini kabis kwamba katika muda wake wote huu aliokaa kwenye siasa bado nina kazi ya ziada ya kuendeleza kuweza kumfanya awepo na upiganaji unaanzia chini kwenda juu. Nashukuru enzi za mwalimu nilikuwepo lakini nilikuwa bado mdogo sana nilipata bahati ya kwenda butiama wakati huo mzee alikuwa ni mkuu wa mkoa wa kigoma nilipokuwa kwenye media pale sasa ndipo nilipoanza kumfahamu baba wa taifa vizuri. Kadi yangu ya chama cha mapinduzi nimeipata mwaka 2000 nina miaka kumi sasa ndani ya ccm kuanzia vijana, na kadi zote za uwt na wazazi kwa hiyo upiganaji wangu mimi ndio umeanza rasmi na mzee mzindakaya kwenye halmashauri kuu ya mkoa akatangaza rasmi kwamba anastaafu kwa sasa akasema naoondoka. Kwa hiyo hilo ni jukumu la sisi vijana wake kuendelea kuwemo kwenye siasa. Mimi nitaendelea kulibeba jina lake na nitaendelea kuwa mwanasiasa ambaye kwa sasa hivi natumai ndio muda wangu muafaka kiumri na hata kwa nafasi ambayo nimeishika ni mdogo sana kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ni sio kitu kidogo ni kikao kikubwa sana cha chama chetu ambacho kinafanya maamuzi makubwa kabisa ya kitaifa kuchagua viongozi ambao ndio wanakuja kuwa wawakilishi wetu wabunge kwa hiyo si kazi ndogo kwa hiyo nitaendelea kwa kuyafanya yote aliyoyacha katika mustakabali ambao ni mzuri wa maadili na miiko ya viongozi wetu sisi hasa wa ccm.

Swali: Toka umeanza kusikika kama mtangazaji kuanzia times radio, radio uhuru, clouds fm na kurudi tena radio uhuru kwa nini uliamua kurudi radio uhuru?

Violeth: Baada ya kutoka times fm nikaona naingia kichama zaidi na ile radio si ya chama, nikaona kwamba napata tabu sana kufanya deliverance ile ninayoitaka ya chama changu kama kijana nikaenda radio uhuru sasa pale ndio mambo mwake kwa sababu ni radio ya chama nafanya kazi yangu vizuri nimekaa miaka mitano pale nilipokuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa. Clouds fm wakaniomba nikasema ok acha niende na clouds nikaone ushawishi gani ambao utaweza kuwashawishi vijana wenzangu angalau tutengeneze mazingira ya kupata vijana ambao watakaoweza kuja kuingia ndani ya chama chetu. Clouds fm kama youth radio station ambayo inasikilizwa na wanachama wote na watu wote ambao hata sio wanachama wa ccm sehemu kama ile ambayo mimi nikituma makombora yangu yatafika kwa watu wengi. Baada ya hapo secretariat ya ccm ikaniandikia barua ya kuniteuwa kwenda idara nyeti ya itikadi na uenezi. Ni heshima kubwa sana ambayo secretariat na halmashauri kuu ya taifa imenipa kwa hiyo niko pale sasa kwenye itikadi na uenezi radio uhuru ni sehemu ya idara yetu magazeti ya uhuru na mzalendo ni sehemu ya idara yetu kwa hiyo uenezi wetu sisi tutaueneza radio uhuru, magazeti ya uhuru na mzalendo na bado tutaeneza kwenye vyombo vingine ambavyo havimilikiwi na chama lakini kwa sababu ni idara ya uitikadi na uenenzi kwa namna moja ama nyingine lazima tutavitumia kwa hiyo mimi kurudi radio uhuru hapana ila kutokana na uenezi huo huo na nina talent ya utangazaji ikaonekana violeth apate nafasi kubwa sana yakupata vipindi vya kufanya vya itikadi nauenezi kwenye radio ya chama kwanza ndio maana kipindi cha uchaguzi wa wenye viti vya serikali za mitaa nilikuwa na kipindi cha safari 2009 kuelekea uchaguzi 2010 na sasa tunajifua kwa utekelezaji wa ilani 2010 kuelekea katika uchaguzi mkuu 2010 wa chama na kwa hiyo sauti yangu huto isiki tu radio uhuru utaiskia katika sehemu nyingi ambazo kunauenezi sababu tunahitaji kueneza sera za chama cha mapinduzi.

Swali: Marehemu amina chifupa wa mpakanjia alikuwa rafiki yako wa karibu na mlikuwa mkipeana mawazo ya kimaendelo, je uatweza kuyaendeleza yale aliyokuwa akiyafanya manake wewe ndio mwanadada pekee uliyebaki mpiganaji katika maswala ya siasa?

Violeth: Amina chifupa wa mpakanjia, mimi kama violeth ndio niliyekuwa mtu wa kwanza kwenda kumshawishi amina na kumkatia kadi yake ya chama cha mapinduzi,tulikuwa marafiki sana na tulianza kiutani tu nakumbuka niliwahi kumualika kwenye kipindi changu tukafanya mahojiano, basi watu wakamshawishi pia kwa nini asigombea unajua amina alikuwa na karisma ya kupendwa na watu ni mtu wa watu sio kwa unafiki mwisho wa siku namshukuru mungu kwamba ile brand ambayo tuliipanga mimi na amina imekuja imetoka nilimwambia amina agombe ubunge mimi nitagombea ujumbe wa halmashauri ya taifa akasema sawa nilivaa kibwebwe mimi nilicheza mpaka shoo amina chifupa awe mbunge kweli alishinda na alivyoshinda hakutusahau, yalitokea malumbano mengi tu ya kisiasa violet na amina hawapatani tena na unajua tena siasa zetu hizi lakini hilo kwetu halikuwa na nafasi. Kwa mara ya kwanza leo naongea na blog ya mo kati ya watu ambao natembea lakini ndani ya nafsi yangu amina anaishi ni mimi hata mzee chifupa leo akilisikia hili atashanga sana lakini kila ninayekuatana naye nafananishwa na amina sasa najuliza nimefanana naye nini utangazaji,tabia au uthubutu na ile hali ya kuwa mtu wa watu kwa hiyo mimi nasema kuyaenzi kuyafanya mambo ya amina na uhakika nayafanya na ndio maana kila ninapozunguka nikionekana tu huyu kama amina mpaka wakati ukafika nikasema jamani ngoja nipumzike nijifiche. Katika watu ambao wananifufua sasa hivi ni mo blog. Kwa kweli amina alifanya mambo mengi sana nasikitika kuyaona kwamba hayaendelei ila mimi nimerudi kuyaendeleza na nimesema 2010 hii ni wakati wangu wa kuwatumikia vijana ipasavyo na kuyaendeleza yale yaliyoachwa na amina kwa vitendo na si kwa maneno.

Swali: Unazungumziaje jumuiya ya umoja wa vijana ukiwa kama ndio zao lako lililokufanya kuwa mjumbe wa nec, mwaka huu mmeongezewa nafasi za ubunge na tumesikia hivi sasa kumekuwa na mizengwe, kukashifiana kwa baadhi ya wagombea na kwa nguvu uliyokuwa nayo inaonekana watu wanakuogopa?

Violeth: Binafsi mimi ni zao la vijana ni kweli kwa sababu wakati nagombea halmashauri kuu ya taifa nilikuwa mwenyekiti wa shina,nikachaguliwa kuwa mjumbe wa baraza na chama chetu kina nafasi 15 vijana makundi 5 vijana, uwt 20 ,kuna viti 20 bara na zanzibar viti 20 ukitoa zile nafasi za kila mkoa kwenye ngazi ya taifa ambazo wanachukuwa fomu za nec na wenyekiti na makatibu ambao wao wanaingia na nafasi zao, mimi niligombea uwenyekiti wa halmashauri ya taifa kwa sababu kwanza umri wangu ulikuwa unaruhusu mimi bado kijana sana, ukiwa wewe ni kijana ambaye una uwezo wa kutetea sera zetu za chama za jumuiya yetu unajua majukumu yako miiko na maadili na kweli unatambua kabisa unakuwepo kwenye hiyo jumuiya kwa sababu zipi hauna tatizo na ndio maana sasa hivi wanatuingiza kwenye matatizo. Wakati ule wa enzi za kina marehemu amina chifupa nafasi za kugombea ubunge katika jumuiya yetu zilikuwa ni mbili tu lakini sasa hivi nafasi zimeongezeka zimekuwa 11 kutoka 2 kwa hiyo sasa hivi wametokea mabinti mbali mbali kila mmoja na nafasi yake, kila mmoja na anajua alikotoka yani ni tafurani tupu lakini ni tafurani sababu ni wakati wao nafasi ni zao na zetu sisi sababu na sisi pia ni vijana lakini unakuta panapokuwa na uchaguzi kuna mitikisiko mbwembwe nyingi, shutuma hazikosi, vurugu lakini mwisho wa siku tunachosema ni kwamba je umeifanyia nini jumuiya yetu, wewe ni nani mimi leo ukiniuliza nagombea ubunge wa vijana nitakwambia ni mwenyekiti wa shina najua shina, nilikuwa mjumbe wa tawi ofisi ndogo ya makao makuu ya chama, mjumbe wa baraza la vijana mkoa wa dar-es-salaam hatimaye nimekuja kuwa mjumbe wa nec halmashauri kuu ya taifa kuu ya taifa na niko katika idara ya itikadi na uenezi kwa hiyo historia yangu ndani ya chama na ndani ya jumuiya yangu inajidhihirisha na kwamba huyu mtu ni wa aina gani lakini niwaombe tu hao wagombea wanaokuja sasa hivi wasifanye jumuiya ya umoja wa vijana kama ni ngazi ya kuwa mheshimiwa tu tuchuje tujipime kwa sababu unapoenda bungeni wewe unawakilisha vijana deliverance yako wewe inatakiwa ionekana kama kijana hatukatai watu wamesoma tunawasomi kibao lakini kuna wasomi wengine hawajawahi hata kuzungumza ndani ya bunge mpaka wamemaliza miaka yao mitano kwa hiyo tuangalie kwamba sawa tunahitaji mtu aliyesoma, tunahitaji mtu mwenye kutisha ana uwezo wa kusimama kuna mtu yuko form 4 lakini akisimama pale bungeni wewe mwenyewe unasema ala kweli, marehemu amina hakuwa na elimu ya kutosha hakufika kwenye elimu ya chuo kikuu lakini alikuwa ana uwezo kushawishi bungeni akizungumza unasema kweli huyu mtoto amesema wakati mwingine watu wanabeza lakini wanakuja wanakubali alichokisema huyu binti ni sahihi, mimi nasema kwa hawa wanaogombea nafasi za vijana mimi nasema watanisamehe na sintosita kuwaambia ukweli kwamba ndugu yangu huko ulikotokea kwa sababu tunahitaji mbunge akikaa tukimtizama mle ndani kweli niseme hapa kura yangu sikukosea kwa hiyo tusifanye kwamba tunacheza rede na ninawaambia viongozi wenzangu kama watu watachaguliwa wajumbe wa mabaraza kama kutakuwa na mabadiliko lakini kwa kweli tusifanye makosa kuingiza wabunge ambao hawana uchungu na jumuiya yetu, wabunge ambao tumewapandikiza wenyewe kwa sababu ya maslahi yetu sisi binafsi ya baadaye tutakuwa tunauwa jumuiya ya umoja wa vijana ya chama chetu watu wanachaguana. Nasema mabinti wenzangu nawaunga mkono kwa asilimia elfu ishirini lakini nataka yule ambae namuona kabisa kwamba huyu ataenda kuniwakilisha vizuri mimi hapa binafsi naamini uwakilishi wangu kama mjumbe wa nec unakwenda vizuri lakini sijifagilii lakini alhamdulilahi na ndio maana hata viongozi wanakuona wanasema hebu tukaondoe haka tukaweke kidogo huku kwenye chama kaendelee kupata uzoefu kwenye chama.

sister-v-pic-2-722082.jpg


sister v akiwa katika pozi nyumbani kwake.

swali: Tunaingia katika kipindi cha uchaguzi wa wabunge na maraisi, je umefikiria kugombea nafasi ubunge?

Violeth: Kabla sijajibu swali lako ambalo unahamu nikujibu kweli kweli kama nagombea au sigombei niwasihi sana wagombea wote wa nafasi za ubunge nafasi za udiwani ila uraisi najua moja kw moja mh. Jakaya kikwete ndio raisi wetu hizi mbio nyingine za sakafuni zitaishia tu ukingoni watusindikize, wale ni wachangamshaji kwa hiyo wacha wachangamshe kidogo nchi. Ngoja hizi burudani zipite sisi tutamalizia kazi yetu lakini mh.raisi bado atakuwa ni jk miaka mitano yake swafi atamaliza baba kazi yake tuliyompa wengine wasubiri huko mwaka 2015 mungu akitupa uhai kwa wagombea wa udiwani na ubunge. Maadamu tumewapa wananchi ridhaa yao wenyewe wachague kwa kura za maoni tunaamini wabunge watakaotuchagulia ndio wanaokubalika ndani ya chama chetu kwa hiyo kama kutatokea na lolote tusiwe sisi ndio wa kwanza kushadadia na kugombana kwa sababu aliyekuchagua ni mwananchi. Mimi binafsi katika sekta ya kugombea nafasi ya ubunge bado sijaamua na sababu kubwa ya kutokuwa sijaamua, nafsi ikiamua basi itakuwa ni faraja kubwa sana kwangu na wale wengi wote wataona kweli huyu mtu ameamu na ana nia na uwezo. Muda ukifika ndugu mwandishi utaona wewe mwenyewe tena wala usije kuniuliza nitakutumia tu message baba ndege inapaa sasa naenda kwanza kufanya kazi yangu ya chama niliyopewa.

Swali: Wewe kama wewe unaionaje siasa kiujumla kwa tanzania?


Violeth: Siasa kiujumla ni nzuri kama wewe ni mwanasiasa, siasa ni mbaya kama wewe sio mwanasiasa kwa sababu ukijikwaa kidogo tu utaanguka utaamka utajipukuta vumbi utaendelea lakini ukiwa sio mwanasiasa utaanza,unaona wameshaanza na hizi imani zetu potofu wameshanipiga juju hapa hamna swala la juju siasa ni mpangilio siasa ni nzuri, siasa ni tamu yani kwangu mimi naiyona burudani shadidi najisikia raha sana sikujilazimisha nimeipenda mwenyewe kwa hiyo mimi nasema siasa ni tamu na nzuri kama unajua kujipanga na iko kwenye damu basi mambo murua kabisa.

Swali: Kwa nini vijana hawana wito wa kujitokeza kwenye siasa?

Violeth: Kama kuna mwaka ambao vijana watajitokeza kugombea na wameshaanza kujitokeza na kuwasumbua na watu ni huu mwaka 2010 vijana watajitokeza kwa wingi sana wasiwasi wangu ni mdogo tu ambao nataka tu kuwaasa vijana wenzangu tuwe tayari kuwatumikia wananchi tusiwe tayari kugombea kwa ajili ya kumtoa fulani unajua wakati mwengine unaweza kugombea nafasi kwa sababu ya kumkomoa fulani unasema mimi nataka nimwonyeshe mimi si kijana bwana nataka nimwonyeshe kwamba tumepewa nafasi sasa ukishamng'oa yule mtu matokeo yake kwa kuwa hujajianda we kazi yako ilikuwa ni kumng'oa fulani unaposhika yale madaraka baadaye yatakushinda yakikushinda watasema mnaona hawa vijana mliowapa kipaumbele miaka mitano hiyo hamna kitu kwa hiyo niwasihi wenzangu wagombee lakini wajue kwamba wanagomea kwa sabababu wanaenda kuwa wawakilishi wa vijana katika bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania kwa hiyo tusimuangushe mh.raisi ambaye ametupa nafasi hii kubwa kwa kweli ametusaidia sana hata ukiangalia kwenye wizara zake vijana wapo wanashaini kabisa.

Swali: Kuna uvumi kwamba mh.mzindakaya yuko mbioni kukupigiadebeiliuweze kuwa mrithi wa kiti hckae cha ubunge katika jimbo lake,kuna ukweli wowote juu ya hili?

Violeth: Hakuna jimbo ambalo mtu atasema amelirithi kwa sababu majimbo yote ni ya wananchi,mzee mzindakaya alipoaaga hakutaja jina la mwanaye hata mmoja kwamba atagombea, violeth kama violeth akija naye atakuja kivyake kwanza hakuna watu wanaopata shida kama sisi watoto wa viongozi kwa sababu wazazi huogopa kupata aibu iwapo tutashindwa,mzee mzindakaya wala hausiki na kunipigia debe naomba niwatoe watumashaka juu ya hili.

Swali: Nini matarajio yako ya baadaye?


Violeth: Matarajio yangu ya baadaye ni kwenda kusoma nipate masters yangu na phd katika masuala ya uongoziili niweze kuitumikia nchi yangu ili nije kulitumikia taifa langu katika nafasi yoyote ile.

Swali: Unamzungumziaje mh.mohammed dewji au mo?


Violeth: Mo ni mtu wa watu,watu wanamjali na kumpenda kwa hiyo aendelee kuwatumika wananchi wake kama anaona bado muda unamruhusu kwa sababu bado kijana na watu bado wanamuhitaji,keep it up brother.

Swali: Nani role model wako?

Violeth: Ni mh.jakaya mrisho kikwete na analitambua hilo.

Swali: Mwisho una ujumbe gani kwa watanzania?

Violeth: Tunaelekea kipindi cha uchaguzi kwa hiyo nawaomba vijana wenzangu,ndugu zangu,baba zangu,mama zangu,wananchi wenzangu tusifanye makosa raisi bora ni jk amalize miaka yake mitano akapumzike aliyoyaanzisha tuyaendeleze ahsanteni.

Special thanks to mama the woman i love the most,papa for supporting,edward mpogolo my x-husband kwa mengi sitomsahau na ayoub and harrison my big boys kwa maswali wasiliana name kwa number 0717-390353
Source: http://www.mohammeddewji.com/blog/
 
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
Huyu ni Violet Mzindakaya aka Sister V!Naona Mchuzi anatumia blogu yake kupromote watu hawa ,ambao they have got nothing ,just because their dads were in position.

Binti wa Makamba na kaka yake January kila mara habari zao ziko kwenye blogu!
Naona huyu anataka kuwa somebody,anyway tuko fools wengi Tanzania.ana shati la kijani ,ni mwana SISIEMU mzuri.
 
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Messages
408
Likes
4
Points
35
Soulbrother

Soulbrother

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2009
408 4 35
we all promote something swali ni je,what price do we pay? isije ikawa tunajishusha hadhi by doing that
 
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
huyu amepewa mahojiano na Michuzi kwenye blogu yake.Unajiuliza je ana nini cha maana kwa watanzania.I guess kuna Watz wa muhimu zaidi ,madoctor,nurses,policemen etc ambao wanaweza kupewa nafasi kuliko huyu nonsense.

watu wanaweza kuwa na dataz zake,so kujiweka hewani hivi,you get what you want!Publicity for nothing
 
Obi

Obi

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2009
Messages
376
Likes
5
Points
35
Obi

Obi

JF-Expert Member
Joined Jul 6, 2009
376 5 35
Ndio tatizo kubwa sana tulilonalo kwa sasa. Inabidi kutafuta namna ya kuondoa mfumo huu wa watoto wa vigogo kupandikizwa katika nadhifa mbalimbali
 
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Messages
7,494
Likes
104
Points
160
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2008
7,494 104 160
Mzee Mzindakaya ametangaza kustaafu Ubunge kule kwao. Binti anaweza kumrithi babaye. Hatutashangaa. Wazee wengi wa CCM ndio wako kwenye mchakato huo.
 
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Likes
3
Points
35
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 3 35
Washindwe kwa jina la Bwana!
 
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
Tupeni CV yake huyu binti.ukitaka publicity ,ukubali chochote
 
Kibunango

Kibunango

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2006
Messages
7,712
Likes
259
Points
180
Kibunango

Kibunango

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2006
7,712 259 180
Huyu ni Violet Mzindakaya aka Sister V!Naona Mchuzi anatumia blogu yake kupromote watu hawa ,ambao they have got nothing ,just because their dads were in position.

Binti wa Makamba na kaka yake January kila mara habari zao ziko kwenye blogu!
Naona huyu anataka kuwa somebody,anyway tuko fools wengi Tanzania.ana shati la kijani ,ni mwana SISIEMU mzuri.
fail.jpg

 
M

Marigwe

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2009
Messages
227
Likes
5
Points
35
M

Marigwe

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2009
227 5 35
Mmakonde kwa nini umekerwa na mahojiano ya Violet na Michuzi? Kwa kuwa ni mtoto wa Mzindakaya? Au? Mimi sioni tatizo la hiyo interview. Kwani wewe ambaye siyo mtoto wa wakubwa umezuiwa kujitangaza? Wewe una tatizo la inferiority complex kutokana na malezi na kwa vile wazazi wako si wakubwa. Ungekuwa mtoto wa mkubwa ungefanya anachofanya si Violet tu. Chukulia akina Mwamvita Makamba, Nape Nnauye, Ridhwani Kikwete, Vita Kawawa, Zebine Mhita (binti wa Alhaji Omari Muhaji ambaye alikuwa mwanasiasa mashuhuri enzi ya Nyerere) na wengine wengi tu akina Nchimbi. Hawa wazazi wao waliwajenga wajiamini. Na huo ndiyo ukweli wenyewe. Hawa watakuja kuwa viongozi kwa sababu wazazi wao wanatokana na uongozi. JK baba yake alikuwa DC baada ya nchi yetu kupata uhuru wakati Babu yake alikuwa Chifu wa Wakwere. Haikwepeki. Kwa nini kwa sababu ya Universal Law of Attraction. Hiyo ni sayansi kubwa. Haisaidii kuipinga haipingiki ndugu yangu Mmakonde. Hawa waliumbwa ili watawale na watatawala. Hata Freeman Mbowe baba yake alikuwa mwanaharakati maarufu ambaye alimsaidia sana Mzee Nyerere. Someni historia jamani na muache ushabiki wa Kiyanga na Simba kwenye mambo ya maana.
 
Gelange Vidunda

Gelange Vidunda

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2008
Messages
312
Likes
4
Points
35
Gelange Vidunda

Gelange Vidunda

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2008
312 4 35
Acheni hizo! Blogu ya jamii ile, watu wanamtumia na yeye anaziangalia kama zipo poa na anapost/upload kwenye blogu yake. I don't think its a matter of him doing the publicity.

Vilevile, hivi ukienda jimboni au sehemu yeyote yenye demokrasia si utachagiliwa kwa kupigiwa kura? Sasa tatizo lipo wapikama mtu baba yake alikuwa akichaguliwa kwa kura naye akajitosa kujaribu kuchaguliwa? Sidhani kama ni jambo lu "kurithi". Besides, nani aliyesema watotot wa viongozi wasigombee kuchaguliwa?

Some pipo bwana!!!!
 
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Messages
7,494
Likes
104
Points
160
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2008
7,494 104 160
Katika umri mdogo tu wa miaka isiyozidi 23 tayari ana X husband! Kaachika?!
 
Ambassador

Ambassador

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2008
Messages
934
Likes
17
Points
35
Ambassador

Ambassador

JF-Expert Member
Joined Jun 2, 2008
934 17 35
Hivi watoto wa wanasiasa nao lazima wawe wanasiasa by default? Hii ndo inaleteleza wanasiasa wasiokuwa commited au wasiokuwa na uchungu na nchi yao kwani walikuwa wanasiasa kwa sababu wazazi wao wamewaconvince. I like Madaraka Nyerere kwani hajihusishi na siasa na ameweka kwazi kwamba hiyo ilikuwa dream ya mzee lakini yeye ana derams zake nyingine!
 
Balantanda

Balantanda

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2008
Messages
12,389
Likes
1,170
Points
280
Balantanda

Balantanda

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2008
12,389 1,170 280
Katika umri mdogo tu wa miaka isiyozidi 23 tayari ana X husband! Kaachika?!
Kazaliwa mwaka 1977,iweje useme ana umri mdogo usiozidi miaka 23??/,soma mahojiano vizuri mkuu
 
A

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Messages
1,504
Likes
35
Points
145
A

Akili Kichwani

JF-Expert Member
Joined Jan 7, 2010
1,504 35 145
siasa za kimbari zimeingia bongo!!!!!!!!!!!!!!
 
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Likes
30
Points
135
MwanaFalsafa1

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 30 135
Katika umri mdogo tu wa miaka isiyozidi 23 tayari ana X husband! Kaachika?!
Violeth:naitwa violeth mzindakaya nimezaliwa tarehe 29/9/1977

Piga mahesabu vizuri mkuu.
 
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2009
Messages
12,287
Likes
64
Points
145
Teamo

Teamo

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2009
12,287 64 145
huyu dem ni mtangazaji wa clouds fm?
 

Forum statistics

Threads 1,238,317
Members 475,877
Posts 29,315,605