Exclusive: Hivi Mwanamke kuolewa ili kuondoa nuksi/ ili kupata zawadi ni akili au matope??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Exclusive: Hivi Mwanamke kuolewa ili kuondoa nuksi/ ili kupata zawadi ni akili au matope???

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Matola, Jan 3, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Wana MMU hii sio tamthilia ya kusadikika bali ni hali halisi iliyopo mtaani kwangu ambayo nadhani si sahihi na tuendako hili laweza kuwa janga kubwa.
  Mimi naishi uswahilini na mtaani kwangu kuna kundi la wadada wasiopungua 20 hawa ni daily members ambao lazima wawe pamoja wakati wa jioni na some time full day, lakini kwa ujumla wao hawa hawapungui 50. sasa basi mimi sina tatizo lolote na wao kuwa na kundi lao la kujiwezesha kwenye sherehe na misiba nawaunga mkono kwenye hilo, lakini tatizo langu kubwa ni hawa dada zangu wa kitaa kugeuza ndoa kuwa kama swala la mzaa!! kwa nini? nitaeleza:

  Katika kundi hili kuna kinara wao huyu Dada hapungui umri wa 50 na hajaolewa ila amefanikiwa kumbaka rafiki yetu mmoja na kuzaa nae mtoto mmoja wa kike baada ya kupata mtoto akamuanzishia visa rafiki yetu na sasa hawaishi pamoja, huyu mdada ana nguvu kubwa za kiuchumi.

  sasa basi umezuka mtindo wa harusi zisizokuwa na kichwa wala miguu kisa mdada mwingine anaona amechangia sana wenzake lakini yeye hajui ataolewa lini na anatamani ile mizawadi wanayozawadianaga, basi hapo ataingizwa mkenge pimbi yeyote na mtasikia mnatangaziwa harusi na kadi za michango lakini baada ya mwaka hakuna ndoa! na binafsi nimeshadecrare hapa mtaani kwamba siko tayari tena kuwachangia hawa wadada, wote hawa ni pepo ya shetani.

  Haya kuna wengine kwenye kundi hili ambao ni waumini wa kiislamu, tene hawa ndio hawana shida maana wako tayri kuolewa na mume wa mtu huku wakijuwa kwenye uislamu talaka haitakuwa tabu baada ya kutimiza malengo yao ya kutoa nuksi!
  Nina mengi kuhusu kundi hili lakini sipendi thread iwe ndefu najuwa wavivu wa kusoma ni wengi, je kwa hali hii ni wapi tunakwenda?

  Hitimisho: kwa sababu huyu dada kinara wa hili kundi ana grocery ya pombe na ina mvuto hapa mtaani kwetu, basi imekuwa ni kivutio vijana wengi kupenda kufika hapo jioni ili kusuuza koo, lakini kama una mke na yeye si mwenyeji wa mtaa huu afikapo hapo uvutiwa na kundi hilo na kesho si lazima uende nae wewe mumewe na huenda yeye mwenyewe kujiunga na uanachama na papo hapo ndio uhesabu ndoa yako sasa itakuwa ni ndoano rasmi.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wakalishe chini uwaambie hufurahishwi na tabia yao maana kusema hapa bila kuwaambia hakuwezi kuwasaidia.

  Hata hivyo hilo sio jambo jipya kiviiiile. Wengi siku hizi wanaingia kwenye ndoa kupata michango, sifa, heshima ya kulazimisha, security na mengine ambayo yanafanya baada ya muda wachokane humo ndani.
   
 3. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kila mtu na akili yake,hao wanao fanya upupu huo hawana ajira, wangekua nazo wasinge kua na mda huo wala kufikiri kuolewa kwenye usawa kama huu eti kisa vyombo au umechangia mtu kwa mda mrefu...
   
 4. M

  Miriamemmanuel Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku hizi wanawake wengi wamepunguza mapenzi kwa wanaume sababu ya tabia zao. Inawezekana ni kweli wanafunga ndoa kwasababu ya kupata vitu au wanapokuwa ndani ya ndoa maisha yanabadilika yanakuwa tofauti na mwanzo wa mapenzi yao hapo ndipo utakuta ndoa inakuwa ndoano.

  Nahao wanawake wanapo waletea card za mchango muongee nao na kuwapa ushauri kabla ya kuingia kwenye ndoa kwani ndoa sio lelemama.
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  whatever is excelency
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nishawahi gusia kua taasisi ya ndoa inabidi ifafanuliwe upya... Ile belief ambayo ilikua Universal to all kua ni kitu ambacho kimetukuka, cha stahili heshima ya hali ya juu na kuboreshwa kwa kuzingatia wanaooana (yaani mwanaume na mwanamke) yamebadilika sasa.... Sad.

  Hata hivo kweli kabisa mwanaume anataka kuoa mwanamke wa moja kwa moja.... Awe mke na mama wa watoto wake inabidi awe makini saana katika kuchagua mke. Kama mwanaume ni yule valu valu tu na hajali wala hana focus na ndoa then sawa. But kweli kabisa yupo serious na ataka mke wa haja... Huwezi ukaenda oa mwanamke ambae kijiwe chake ni grocery na ukategemea kua mambo yatakua mtelezo..... Ni nadra na kwa bahati saaana. For kijiwe cha grocery wahusika na interest zao ni tofauti kabisa na vitu ambavo ni msingi kwa kua katika ndoa na kuidumisha.
   
 8. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kuna wanawake matope kichwani mwao hadi balaa.
  tena wako weeengi kweli siku izzz.
  wanajua kujipodoa hao mmh kama unaoa reception kaka litakula kwako.
  kweli muwe makini kwel ktk kuchagua life partiners wenu, omba mungu akupe wa kufanana na ww daima , ukikurupuka mmh utajuta ndugu mmh.
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Ukiona mkeo anayumbishwa na mwenye grocery
  Jua huna mke.

  Hivi jamani hivi visa mnaviona wapi?
  Au mie naishi dunia ya sita?
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Wewe utakuwa unaishi appartments za Sleep way Masaki, visa utakavyoviona wewe ni mbwa kufanyiwa medical Examination kila mwezi kuliko binadamu anaeishi uswahilini na ana bajeti ya chakula kwa mwezi kuliko Wema Sepetu.
   
 11. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Akili zinatofautiana kaka.
   
 12. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Nadhani unachanganya mada kama umenisoma vizuri hapo wapo mchanganyiko kuna wenye Biashara zao tena wanakwenda Dubai na China.

  Na huyu Mwanamke mwenye hichi kijiwe hapa mtaani peke yake anamiliki nyumba 5 za uhakika na za kisasa ambazo amezipangisha, huyu mimi ndio namuona kama muhimili wa uovu na ambaye amebahatika kuwa na ushawishi mkubwa kwa hawa wa dada, na nilipowafanyia utafiti wa kina nikaona kuna vitafrija mbuzi ambavyo huwa aviishi kila mwezi ndivyo vinawatia wazimu hawa wadada mapepo, na kwa bahati nzuri mimi nimekuwa nikiignore karibu Invitation zao zote hasabhizi Birthday party zisizoisha. ( Note: na mimi nina kaujiko kangu mtaani sio kwamba najipamba )
   
Loading...