Exclusive: Haya Ndiyo Matukio Makubwa Yaliyopelekea Mauaji Ya Bosi Wa Iebc Musando Huko Kenya

Hivi anayeondolewa na bado anapumua na tunakula nae ' bata ' Kitaa na Yule anayeondolewa kwa ' Kuuwawa ' na anaenda kula ' Bata ' Kaburini nani ana afadhali?
Mkuu, toka jamaa ameondolewa tume ya uchaguzi umewahi kusikia habari zake? Unajuaje kama yuko hai? Au kwa kuwa familia yake haijajitokeza kumtafuta? Matukio hayo ya Kenya hata hapa Bongo yapo sana tu.
 
We can't say for certain the Government is involved or not. Anybody could have planned this incidents.The question is why and who is to benefit?
 
Baada ya taarifa ya Kifo cha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IECB Bwana Chris Musando kutokea jana niliweza kujiridhisha ' Kitaarifa ' zaidi kutoka kwa ' Wadau ' mbalimbali wa Kenya ambao baadhi yao wanahusika moja kwa moja ya masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao huku wengine wakiwa ni ' Wabobezi ' wa Investigative Journalism huko Kenya ambapo kwa pamoja walinithibitishia mambo makubwa saba ( 7 ) yaliyopelekea Kifo hiko cha ' Kikatili ' kabisa.

Yafuatayo ni matukio ambayo Marehemu aliyafanya siku nne ( 4 ) tu zilizopita kabla ya hayo ' Mauaji ' yake ya ' Kikatili ' kutokea hivyo nitayaweka hapa kwenu ili kila mmoja ayaangalie na ayafanyie ' tathmini ' mwenyewe ' Kimoyomoyo ' kisha mwishoni wote tutajua ni nani ' Kamuua ' Marehemu Chris Msando.

Tukio #1.
Kwa niaba ya Tume nzima ya IECB Marehemu alipeleka ombi Serikalini la kupewa Ulinzi wa Yeye na wenzake wote lakini hadi mauti yanamkuta hakujibiwa wakati alipopeleka maombi ya mengine yahusuyo ufanikishaji wa ' Oparesheni ' za IECB alijibiwa na kupewa ' Ushirikiano haraka sana.

Tukio #2.
Siku tatu kabla ya Kifo chake Marehemu alikwenda Police kupeleka taarifa za Yeye ' Kutishiwa ' maisha na Watu asiowajua lakini hakuna ' Ulinzi ' aliopewa hadi Umauti yanamkuta hiyo jana.

Tukio #3.
Marehemu huko nyuma alishapewa ' Onyo ' kali la kutozungumza na Chombo chochote cha Habari nchini Kenya na ' Mamlaka ' na kuambiwa kwamba Mtu pekee ambaye angetakiwa kuzungumza na Media basi ni Waziri tu husika wa Habari na Mawasiliano.

Tukio #4.
Siku mbili tu kabla ya Kifo chake Marehemu Msando ' alikaidi ' hiyo amri kutoka katika ' Mamlaka ' ambapo alikubali mualiko wa kwenda kufanya interview na Kituo Kimoja cha Television nchini Kenya ambapo aliyoyasema huko inasemekana kuwa ndiyo yaliharakisha ' mauaji ' yake.

Tukio #5.
Wakati akiwa ' mubashara ' kabisa akizungumza katika hicho Chombo cha Habari Marehemu alisikika ' akiwahakikishia ' Wakenya wote kuwa kwa jinsi alivyotengeneza ' Mfumo ' wa Kimawasiliano wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya ya IECB hakuna Mtu yeyote yule atakayeweza ' Kuudukua ' hata iweje na akaenda mbele kusema kwamba Mtu akitaka ku ' hack ' taarifa zozote za Tume ya Uchaguzi IECB basi labda akatwe ' Kiganja ' chake kwani ili upate taarifa zao ni mpaka Yeye ( Marehemu ) atumie ' Kiganja ' chake cha Mkono ndipo Mtu mwingine apate taarifa za Tume.

Tukio #6.
Marehemu bila kujua mbinu za ' Kimafia ' na labda pengine alijisahau kuwa siku zote ukitaka tu ' Kuuawa ' Kimafia basi Mtu wako wa Karibu sana ama Nduguyo au Mpenzi wako au Rafiki yako tu wa karibu ndiyo hutumika sana kukumaliza. Marehemu usiku kabla hajafariki alifuatwa na ' Mwanamke ' ambaye inasemekana anamuamini sana ndipo huyo ' Mwanamke ' kwakuwa tayari alishapewa maagizo yote ya ' Kimafia ' ndipo akamtega Marehemu kuwa wapite barabara fulani ambapo kumbe huko mbele ' Wauaji ' wake wale ' Mafia ' walikuwepo.

Tukio #7.
Ili kuonyesha kuwa ama hakika ' Wauaji ' wake wa ' Kimafia ' walichukizwa na Kitendo cha Marehemu kwenda mbele ya Media na kusema kwamba safari hii katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya hakuna ' Udukuzi 'wowote utatokea kama ilivyokuwa Uchaguzi uliopita labda akatwe Kiganja ' chake ndipo hata katika ' mauaji ' yake ya juzi ' Kiganja ' chake cha Mkono ndiyo kilikatwa na kuondoka / kuchukuliwa na hao ' Wauaji ' na kuuacha mwili wake ukiwa na majeraha mengine shingoni, machoni na tumboni.

Na kama zilivyo Kanuni Kuu za Kimafia dunia nzima ni kwamba Yule ambaye atakuwa kafanikisha ' mauaji ' ya Mtu fulani aliyelengwa basi ni lazima nae pia mwishoni auawe ili kufuta ama kuondoa kabisa ushahidi wote kitu ambacho ' Wauaji ' hawa walikifanya kwa ' Kumuua ' na Yule Dada ( Mwanamke ) pamoja na Marehemu na hatimaye mwishoni ikawa ' Mission Accomplished '.

Soma tu kimoyomoyo na ukishamjua ' Muuaji ' Mkuu wa Marehemu Chris Musando basi baki nalo pia moyoni. Mwishoni jiulize tu swali kwamba ni kwanini Marehemu alipoomba msaada wa Police hakupata ushirikiano ila baada ya kufariki jana Police wa Kenya wameonyesha ' Ushirikiano ' mkubwa Kwake ( Maiti ) huku wakiwazuia hadi Watu wengine sasa kwenda kuuangalia mwili wa Msando na kukataa kufanyike independent post-mortem ambapo hata Balozi wa Marekani nchini Kenya alikuwa tayari kuigharamia kutokana na kwamba hata wao Wamarekani ' wamechoka ' na haya mauaji ya ghafla na ya kusikitisha yanayotokea nchini Kenya kila uchao halafu Serikali haichukui hatua yoyote ile kuyakabili / kuyadhibiti.

Nawasilisha.
Kweli wahenga walishasemaga kizuri hakidumu
Pumzka kwa amani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata upande wa pili pia wako tayari kufanya chochote ili kiu yao ya miaka kadhaa tangu enzi za Mwai Kibaki ya kuingia Ikulu itimie. Kwa kifupi siasa ni ka ugonjwa kabaya sana usiombe kakuingie.... Usimuamini mwanasiasa yyt, utakuwa disappointed. Uchunguzi pekee ndio unaweza kutoa majibu 'kama utafanyika kwa uwazi na haki'.
Waliotenda ndio wachunguzaji unategemea nini Ben mpaka sasa kapotea na hakuna majibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini Msando sikuona sababu ya yeye kusema wazi kwenye media kuwa hakuna atakaye ingilia mfumo wa matokeo labda akatwe kiganja....Kwangu mimi niliona kama alikuwa amewapa mbinu wauwaji kabisa na zile zilikuwa tambo zisizo na msingi na hapa kusema kweli kabisa ndipo niliamini hakuna kitu kinaitwa Tume huru...
Kama mtu alipata wasaha kutazama mahojiano ya Msando atagundua kabisa kuwa alikuwa na upande wake na ndio maana alikuwa anaweka tambo na katika maongezi yake alionesha wazi kabisa uchaguzi uliopita uliingiliwa na wazi alikuwa ana watuhumu Jubilee...
Kwa hiyo Msando angeliweza kuhakikisha hakuna anaye ingilia mfumo wa matokeo kwa kuonesha vitendo na sio lazima kuweka tambo na kuonesha jinsi ambavyo wanaweza kuingilia matokeo...hilo ni kosa alilo lifanya pale kwenye usaili wake.

Halafu Kifo chake kina utata sana maana upande wa pili ule unaweza kuwa umetekeleza hii mission ili kuonesha kuwa wahusika ni watu fulani na kuhalalisha kuwa kura zimeibiwa na kabla ya kifo chake NASA walisema wamegundua kuna mpango wa wizi wa kura sasa najiuliza kwanini wasiwe NASA wame usika kwenye hili jambo ili kuthibitisha madai yao kuwa kuna mpango wa wizi wa Kura?
Halafu ni jana tuu NASA wamehoji usalama wa Kura zao baada Msando kuuwawa...
Bado naamini kuna mengi sana nyuma ya kifo cha Msando.
Rutta: afrika hakuna tume huru za uchaguzi jamaa kauawa ili wafanikishe kurudi madarakani kwa mlango wa nyuma, kwani naibu waziri wa mambo ya ndani wa kenye naye yuko upande fulani hata wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa waziri wa wizara hiyo last month aliwataka wakenya kupiga kura na kurudi nyumbani na akaahidi kumwaga askari wengi siku hiyo. No democracy in kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nyie rukeni rukeni ila nawaakikishia uhuru anashinda
huyo odinga arudi shambani tuu

ila kenya raisi hana say kwa polisi au huljui hili?
hiyo tume ni huru pia that means wanaeza kujiamulia mambo yao kwa mwajibu wa kanuni zao!!
this ain't nothing to me than bullshit propaganda
ya wa kenya waachieni wenyewe!!!

soon magufuli ataaibika na hizi damu za wakenya hazito muacha salama
alieomba msaada kwa nchi jirani na aloombwa msaada wote ziro
 
Kwa nini kura zote zisiesabiwe kituo cha kupigia kura na kubandikwa hapo hapo? Ili makao makuu wafanyekujumlisha tu. Maana kila kituo idadi ya wapiga kura ipo kwenye daftari hivyo ni rahisi kujua kama idadi ya wapiga kura imezidi idadi ya waliojiandikisha. Hivi Vigo usababishwa na ulevi wa madaraka haswa huku kwetu afrika turudishe migumo yetu ya machifu/wafalme/malkia kuokoa vifo vya watu
 
Baada ya taarifa ya Kifo cha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya IECB Bwana Chris Musando kutokea jana niliweza kujiridhisha ' Kitaarifa ' zaidi kutoka kwa ' Wadau ' mbalimbali wa Kenya ambao baadhi yao wanahusika moja kwa moja ya masuala ya Uchaguzi Mkuu ujao huku wengine wakiwa ni ' Wabobezi ' wa Investigative Journalism huko Kenya ambapo kwa pamoja walinithibitishia mambo makubwa saba ( 7 ) yaliyopelekea Kifo hiko cha ' Kikatili ' kabisa.

Yafuatayo ni matukio ambayo Marehemu aliyafanya siku nne ( 4 ) tu zilizopita kabla ya hayo ' Mauaji ' yake ya ' Kikatili ' kutokea hivyo nitayaweka hapa kwenu ili kila mmoja ayaangalie na ayafanyie ' tathmini ' mwenyewe ' Kimoyomoyo ' kisha mwishoni wote tutajua ni nani ' Kamuua ' Marehemu Chris Msando.

Tukio #1.
Kwa niaba ya Tume nzima ya IECB Marehemu alipeleka ombi Serikalini la kupewa Ulinzi wa Yeye na wenzake wote lakini hadi mauti yanamkuta hakujibiwa wakati alipopeleka maombi ya mengine yahusuyo ufanikishaji wa ' Oparesheni ' za IECB alijibiwa na kupewa ' Ushirikiano haraka sana.

Tukio #2.
Siku tatu kabla ya Kifo chake Marehemu alikwenda Police kupeleka taarifa za Yeye ' Kutishiwa ' maisha na Watu asiowajua lakini hakuna ' Ulinzi ' aliopewa hadi Umauti yanamkuta hiyo jana.

Tukio #3.
Marehemu huko nyuma alishapewa ' Onyo ' kali la kutozungumza na Chombo chochote cha Habari nchini Kenya na ' Mamlaka ' na kuambiwa kwamba Mtu pekee ambaye angetakiwa kuzungumza na Media basi ni Waziri tu husika wa Habari na Mawasiliano.

Tukio #4.
Siku mbili tu kabla ya Kifo chake Marehemu Msando ' alikaidi ' hiyo amri kutoka katika ' Mamlaka ' ambapo alikubali mualiko wa kwenda kufanya interview na Kituo Kimoja cha Television nchini Kenya ambapo aliyoyasema huko inasemekana kuwa ndiyo yaliharakisha ' mauaji ' yake.

Tukio #5.
Wakati akiwa ' mubashara ' kabisa akizungumza katika hicho Chombo cha Habari Marehemu alisikika ' akiwahakikishia ' Wakenya wote kuwa kwa jinsi alivyotengeneza ' Mfumo ' wa Kimawasiliano wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya ya IECB hakuna Mtu yeyote yule atakayeweza ' Kuudukua ' hata iweje na akaenda mbele kusema kwamba Mtu akitaka ku ' hack ' taarifa zozote za Tume ya Uchaguzi IECB basi labda akatwe ' Kiganja ' chake kwani ili upate taarifa zao ni mpaka Yeye ( Marehemu ) atumie ' Kiganja ' chake cha Mkono ndipo Mtu mwingine apate taarifa za Tume.

Tukio #6.
Marehemu bila kujua mbinu za ' Kimafia ' na labda pengine alijisahau kuwa siku zote ukitaka tu ' Kuuawa ' Kimafia basi Mtu wako wa Karibu sana ama Nduguyo au Mpenzi wako au Rafiki yako tu wa karibu ndiyo hutumika sana kukumaliza. Marehemu usiku kabla hajafariki alifuatwa na ' Mwanamke ' ambaye inasemekana anamuamini sana ndipo huyo ' Mwanamke ' kwakuwa tayari alishapewa maagizo yote ya ' Kimafia ' ndipo akamtega Marehemu kuwa wapite barabara fulani ambapo kumbe huko mbele ' Wauaji ' wake wale ' Mafia ' walikuwepo.

Tukio #7.
Ili kuonyesha kuwa ama hakika ' Wauaji ' wake wa ' Kimafia ' walichukizwa na Kitendo cha Marehemu kwenda mbele ya Media na kusema kwamba safari hii katika Uchaguzi Mkuu wa Kenya hakuna ' Udukuzi 'wowote utatokea kama ilivyokuwa Uchaguzi uliopita labda akatwe Kiganja ' chake ndipo hata katika ' mauaji ' yake ya juzi ' Kiganja ' chake cha Mkono ndiyo kilikatwa na kuondoka / kuchukuliwa na hao ' Wauaji ' na kuuacha mwili wake ukiwa na majeraha mengine shingoni, machoni na tumboni.

Na kama zilivyo Kanuni Kuu za Kimafia dunia nzima ni kwamba Yule ambaye atakuwa kafanikisha ' mauaji ' ya Mtu fulani aliyelengwa basi ni lazima nae pia mwishoni auawe ili kufuta ama kuondoa kabisa ushahidi wote kitu ambacho ' Wauaji ' hawa walikifanya kwa ' Kumuua ' na Yule Dada ( Mwanamke ) pamoja na Marehemu na hatimaye mwishoni ikawa ' Mission Accomplished '.

Soma tu kimoyomoyo na ukishamjua ' Muuaji ' Mkuu wa Marehemu Chris Musando basi baki nalo pia moyoni. Mwishoni jiulize tu swali kwamba ni kwanini Marehemu alipoomba msaada wa Police hakupata ushirikiano ila baada ya kufariki jana Police wa Kenya wameonyesha ' Ushirikiano ' mkubwa Kwake ( Maiti ) huku wakiwazuia hadi Watu wengine sasa kwenda kuuangalia mwili wa Msando na kukataa kufanyike independent post-mortem ambapo hata Balozi wa Marekani nchini Kenya alikuwa tayari kuigharamia kutokana na kwamba hata wao Wamarekani ' wamechoka ' na haya mauaji ya ghafla na ya kusikitisha yanayotokea nchini Kenya kila uchao halafu Serikali haichukui hatua yoyote ile kuyakabili / kuyadhibiti.

Nawasilisha.
Aisee; umeitendea haki makala yako.Angalia usihusishwe kwenye huo msafara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom