Exchange rate ikoje hapo dsm leo

Dec 1, 2010
68
4
Nasafirisha kiasi kikubwa cha US$ kuja hapo Dar ili kukwepa gharama za Western Union (wao wanatugonga 1US$ = Tshs 1,475.00) Mlioko Dar, bei ikoje mtaani leo?
 
Nenda kwenye website na uangalie. Ila kwa uelewa wangu kama ni USD basi NBC ndio wazuri.
 
Jamani, kama unataka kusaidia mtu, mpe data kamili (website ipi etc).
Mbona kila kitu kiko wazi. Aangalie websites za mabenki. Mara nyingi wao bei zao huwa nzuri kuliko za madukani. Nikaeleza kama ni USD, kwa uelewa wangu NBC bank ni miongoni mwa mabenki yanayo offer rate nzuri.
 
Kwa uzoefu wangu - mtu kama ana dola na anataka dafu, ni bora kuingia mtaani (call it black market if you like) kuliko kwenda bank, huko kuna offer nzuri zaidi.

Bureau de change nyingi huwa zinacheck status ipoje mtandaoni kabla ya kupanga bei zao (www.xe.com) etc)
 
Unajua kwa benki, exchange rates si core business kwahiyo profit motive inaweza isiwe kubwa kama mtaani. Pia risk nyingine ya mtaani ni kupewa fedha fake. Wapo watu wameshapewa fedha fake huko. Lingine ni kwamba black market kwa Tanzania kuna utapeli wa hali ya juu, of all the stuff namshauri mtu ajitahidi kuepuka awezavyo soko hili, yapo watu yameshawahi kuwakuta pale posta. Pia website uliyoweka ni indicative tu. Tofauti na nchini kwetu na nchi za jirani, nchini nyingine haiwezi kukubali kutrade TShs maana si liquid. Mtu atahitaji TSh afanyie nini? Kwahiyo ni web za nyumbani ndio viable au zile unazotumia kufanya transfer.
 
Unajua kwa benki, exchange rates si core business kwahiyo profit motive inaweza isiwe kubwa kama mtaani. Pia risk nyingine ya mtaani ni kupewa fedha fake. Wapo watu wameshapewa fedha fake huko.

Right!
 
Mimi kwa uzoefu, Huwa natumia hii web ni za uhakika ya uhakika 100%. ukienda bongo utakuwa na idea ya bei za mitaani

Currency Converter | OANDA
Hizo quote unazosema wewe ni average huwezi kuona bid-ask (buying-selling), ni bora uangalie kwenye benki zetu siku hizi wanajitahidi na wapo active. Au njia rahisi nenda kwenye website ya BOT then weka + or - (Tsh70 mpaka 100; bid-ask) utapata idea ya retail exchange rates.
 
Nashawishika kuamini kuwa wote mliochangia hii mada hakuna hata mmoja anayeishi DSM au vingine mna uelewa mdogo wa kujibu maswali. Huyu ndugu kauliza, exchange rate ikoje mtaani hapo DSM? Sasa mambo ya aangalie website, sijui nenda CRDB, siyo jibu. Najua na yeye mambo ya website hayampigi chenga, anajua kuliko hata ninyi mliompa website za BOT.
Bosi ,exchange rate iliyooneshwa hapa Samora Avenue mkabala na Extelecom House jioni hii ni: Buying: 1US$ = Tshs 1,497.13 na selling ni Tshs1,512,40.
Mlioona sehemu nyingine mpeni ili atuletee hizo dollar.isi
 
Us $ 1= Tsh 1550.00 lakini kwa jinsi hela yetu ya madafu inavyoporomoka si ajabu utasikia kesho imekuwa Tsh 1600 kwa dolali moja
 
Nashawishika kuamini kuwa wote mliochangia hii mada hakuna hata mmoja anayeishi DSM au vingine mna uelewa mdogo wa kujibu maswali. Huyu ndugu kauliza, exchange rate ikoje mtaani hapo DSM? Sasa mambo ya aangalie website, sijui nenda CRDB, siyo jibu. Najua na yeye mambo ya website hayampigi chenga, anajua kuliko hata ninyi mliompa website za BOT.
Bosi ,exchange rate iliyooneshwa hapa Samora Avenue mkabala na Extelecom House jioni hii ni: Buying: 1US$ = Tshs 1,497.13 na selling ni Tshs1,512,40.
Mlioona sehemu nyingine mpeni ili atuletee hizo dollar.isi
Tunauelewa mdogo enh! Yaani wewe unatatua tatizo kwa siku moja. Halafu exchange rates za mtaani mara nyingi sio the best. Pia wewe unaelewa nini kwamba anafaham juu ya uwepo wa hizo rates huko BOT? By the way BOT ni indicative kwa wholeselling.
 
tsh usd 1,485.94 1,487.16 1,487.55 gbp 2,316.28 2,320.86 2,320.43 eur 1,933.95 1,948.63 1,964.31 zar 208.95 211.05 215.12 dkk 259.41 261.39 263.46 sek 211.73 212.88 215.10 chf 1,483.12 1,479.03 1,495.78 mwk 16.70 16.71 16.71 zkw 0.30 0.30 0.30 k.sh 18.33 18.36 18.50 yen 17.80 17.68 17.77 bot leo
 
INVISIBLE, Ebu tuwekee link binafsi kwa ajili ya Update ya Exchange rate mtani ili itusaidie kusevu kuibiwa na Western Union, Iwepo link inayojitegemea kama ilivyo hii ya Siasa, Uchaguzi mkuu, ili tuendelee kuhabarishana kuhusu mambo ya pesa na interest rate. TAFADHALI.
 
Back
Top Bottom