Ex-GF kajitangaza anao, napata kero vibaya

Asanteni wakuu wote mlionishauri. Nimepima ijumaa tarehe 27 Nov, na jibu ni hili: NEGATIVE

Ingawa nilitumia ndomu siku zote, bado nilikuwa na hofu ya kufa mtu! Lakini wameniambia bado nahitaji kupima tena (sijui ndio wananivutia muda wanijie na bad news kabisa?)

Kwa hiyo next appointment ni miezi 3 ijayo, siku ya alhamisi tarehe 19 February 2010, saa 3 asubuhi. Nimenunua diary mpya na kuweka alama tayari, wish me well wakuu zangu.
 
Dah hongera sana mkuu,hiyo miezi 3 wamekupa incase kama una maambukizi mapya umepata hivi karibuni.Lakini kama uliacha yale mambo kitambo sidhani kama una haja ya kuwa na hofu.
Once again HONGERA! na ujitunze>
 
hongera sana mtu B kwa ujasiri wa hali ya juu uliouonyesha naamini utaendelea kuwa makini katika pitapita zako
huo ni mwanzo mzuri kwako
nilikuwa navuta muda tu nije kukuuliza
 
huwezi kuamini dadangu tangu hili sakata limeanza hata kiungo husika kimekufa ganzi kabisa, kama vile sinacho tena! Hata hapa JF nilikuwa nakuja nasoma thread hii tu naondoka!
 
Dah hongera sana mkuu,hiyo miezi 3 wamekupa incase kama una maambukizi mapya umepata hivi karibuni.Lakini kama uliacha yale mambo kitambo sidhani kama una haja ya kuwa na hofu.
Once again HONGERA! na ujitunze>

Nakushukuru dadangu. Yule counselor alitaka nimpe historia kama mara ya mwisho nimefanya lini, tukaangalia hesabu yake ikaonekana ni kama mwezi 1 kabla ya hiyo tarehe 27. Akaniambia ingawa jibu ni NEGATIVE bado kuna risk kwa hilo tukio la mwisho. Lakini kote nimetumia mpira hata hiyo ya mwisho. Akaniambia nikitaka uhakika sasa niache kabisa nirudi tena after 3 months. Kusema kweli niliogopa upya nikadhani ananificha kwanza nijiandae tena aje anipasulie bomu kabisa! Lakini alinihakikishia kuwa hiyo ndiyo procedure, na tena wengi wanaorudi huwa wanapata jibu hilohilo la negative, ingawa pia wapo ambao linabadilika!

Ingawa naonekana strong machoni mwa watu na hapa ofisini na mtaani hakuna anayejua nimeshachukua hatua gani, ukweli ni kwamba nimeteseka. Sasa mateso yamepungua by 50%, nasubiri hiyo ya next year lakini na ujasiri pia umeongezeka.
 
huwezi kuamini dadangu tangu hili sakata limeanza hata kiungo husika kimekufa ganzi kabisa, kama vile sinacho tena! Hata hapa JF nilikuwa nakuja nasoma thread hii tu naondoka!

Mtu B..kwanza wacha nicheke kidogo...eti kiungo husika kilikufa gansi kabisa yaani hii mwisho usije ukakikata kama mganda fulani alisema kama hiki ndicho kitaniletea balaa ka ngoma wacha nikiondoe kabisa!

halafu hongera kwa ujasiri wako kwenda kupima na kuwa upo negative, mshukuru mungu wako anakupenda sana.... sasa hiyo ni wake up call kwako na kwa wote wenye kuhanya hanya bila mpango!!!!

Take care of ya'self!
 
Pole sana mtu B, nadhani ulikuwa kwenye situation ambayo ni ngumu kuieleza, hapo kama nimekusoma Tatizo alikuwa sana kuwa na ngoma au la, bali Tatizo ni hukumu ambayo umeshapewa
na sio siri utabaki kuwa reference kwa baadhi ya watu kwa maisha yao yote, kwamba jamaa ni "keria ana ngoma zaidi ya miaka kumi lakini bado anadunda tu"

Naomba kuuliza jamani hivi Tanzania hakuna hizo KIT za kupimia ngoma, zile kama pregnant test
maana kama una KIT unaweza kwenda kwenye hivi vidispensary na ukawaomba wakutoe damu na kisha ukajifungia chumbani kwako na HIV test KIT yako na kujipima mwenyewe, sometimes haya mambo yanahitaji privace hata kama una ngoma lakini ukiwa the first to know kwa mtazamo wangu inasound vizuri
 
Mtu B, japo ulisema kule mwanzoni huna nia ya kujitangaza lakini ikiwezekana hebu jitolee kidogo ufanye kazi ya uhamasishaji kwa wengine. Hili ni fundisho kubwa sana ndugu yangu wapo wengi bado hawataki kutumia kinga. Ex-Girl friend na wewe mnaweza kutusaidia wengi tu kulielewa hili zaidi! Ni wazo tu
 
Kuna demu alikuwa girlfriend wangu zamani, majuzi kaonekana kitaa anahamasisha masuala ya UKIMWI na amejitangaza laivu kuwa na yeye pia anayo ngoma. Washkaji kibao wanaelewa nilikuwa namega. Lakini mie siku zote nimetumia kondomu. Sasa tangu amejitangaza huyo demu napigiwa simu na sms kibao za kunipa pole kama vile nami pia nina ngoma! Kwa kadri ninavyojua ngoma inaenea kwa kufanya ngono zembe, na mimi sikufanya hivyo hata siku moja.

Najua hata nikitangaza redioni kuwa mi sina ngoma watu hawataniamini, na sasa naona hata mchumba nitakosa, maana hii habari ni mbaya kinoma!

Nishaurini wakubwa. Naomba msinishutumu mnaposhauri, sikupanga yatokee kama yalivyotokea. Nifanyeje niaminike? Tabia flani mbaya nilizokuwa nazo zamani zote nimeacha, lakini naona hii ya huyu demu kujitangaza itatibua kila kitu!

Fyatuka kimbia kapime ngoma! Ila mzee unalo hilo sijui kama utakamata demu kwenye mtaa wako hahaha! Pole sana
 
Pole sana mtu B, nadhani ulikuwa kwenye situation ambayo ni ngumu kuieleza, hapo kama nimekusoma Tatizo alikuwa sana kuwa na ngoma au la, bali Tatizo ni hukumu ambayo umeshapewa
na sio siri utabaki kuwa reference kwa baadhi ya watu kwa maisha yao yote, kwamba jamaa ni "keria ana ngoma zaidi ya miaka kumi lakini bado anadunda tu"

Naomba kuuliza jamani hivi Tanzania hakuna hizo KIT za kupimia ngoma, zile kama pregnant test
maana kama una KIT unaweza kwenda kwenye hivi vidispensary na ukawaomba wakutoe damu na kisha ukajifungia chumbani kwako na HIV test KIT yako na kujipima mwenyewe, sometimes haya mambo yanahitaji privace hata kama una ngoma lakini ukiwa the first to know kwa mtazamo wangu inasound vizuri

Ni kweli hukumu ndiyo ilikuwa inanitesa. Sasa hivi hata wakisema vipi sijali tena chochote maana majibu yangu ninayo, ingawa of course bado test moja hapo february kumalizia. Atakapotokea mchumba nitaenda naye kupima nikiwa najiamini kabisa, na ndiye atakayekuwa shuhuda wangu wa ndani na wa ukweli.
 
Mtu B, japo ulisema kule mwanzoni huna nia ya kujitangaza lakini ikiwezekana hebu jitolee kidogo ufanye kazi ya uhamasishaji kwa wengine. Hili ni fundisho kubwa sana ndugu yangu wapo wengi bado hawataki kutumia kinga. Ex-Girl friend na wewe mnaweza kutusaidia wengi tu kulielewa hili zaidi! Ni wazo tu

Nautafakari ushauri wako naona kama ni mzuri. Naomba unipe muda angalao nipate ile confirmation kabisa waliyoniambia ni baada ya miezi mitatu, na tayari walinipa appoitment ya February next year. Nikishapata jibu hilo ndipo nitakuwa na nguvu hasa za kufanya uhamasishaji kama huo, na hata kutoa ushuhuda wangu ili wengine pia wajifunze.
 
Wakubwa jana ndio ilikuwa siku ya appointment yangu ya confirmation test, na niliiwahi vizuri. Nashukuru tena nimepata jibu lilelile, kwamba sijaambukizwa. Nina furaha kupita kiasi. Na sasa sijali lolote atakalosema mtu yeyote, majibu yangu yameniridhisha kabisa na kuniondolea hofu. Na sitaki tena demu. Kama mke, sawa, lakini kipimo mbele kama tai!
 
Kuna demu alikuwa girlfriend wangu zamani, majuzi kaonekana kitaa anahamasisha masuala ya UKIMWI na amejitangaza laivu kuwa na yeye pia anayo ngoma. Washkaji kibao wanaelewa nilikuwa namega. Lakini mie siku zote nimetumia kondomu. Sasa tangu amejitangaza huyo demu napigiwa simu na sms kibao za kunipa pole kama vile nami pia nina ngoma! Kwa kadri ninavyojua ngoma inaenea kwa kufanya ngono zembe, na mimi sikufanya hivyo hata siku moja.

Najua hata nikitangaza redioni kuwa mi sina ngoma watu hawataniamini, na sasa naona hata mchumba nitakosa, maana hii habari ni mbaya kinoma!

Nishaurini wakubwa. Naomba msinishutumu mnaposhauri, sikupanga yatokee kama yalivyotokea. Nifanyeje niaminike? Tabia flani mbaya nilizokuwa nazo zamani zote nimeacha, lakini naona hii ya huyu demu kujitangaza itatibua kila kitu!

Pole sana ndgu yangu, lakini fanya maamuzi ukapime. Mara nyingi waliotulia huletewa huyu mgeni nyumbani... remember your past as well, judge her not.

Ukimwi sio death sentence lkn ugonjwa unatesa...jamani inabidi wote tuungane kupiga vita ugonjwa huu and it starts at JF. Unajali?
 
Natamani ingekuwa kweli yuko kikazi au kisanii, lakini kwa jinsi ninavyomfahamu personality yake yule hawezi kucheza maigizo ya hivyo, itakuwa ni kweli ngoma!

Kupima niko tayari na jibu la positive siliogopi, lakini kinachoniumiza zaidi ni haya matangazo, maana mimi siko tayari kujitangaza. Lakini kwa kujitangaza kwake ni kama keshanitangaza na mimi tayari hata kama jibu langu litakuwa negative.

Mkuu wewe cha kufanya ni kupima kama ulikuwa hujafanya hivyo, na kama ni negative basi nawe jitangaze kwamba afya yako iko njema kabisa, hujagusa mawayawaya na hata mchumba unaweza kabisa kupata hata kama anajua ulikuwa unamega huyo muathirika maana unaweza kumdhihirishia kwamba mambo yako ni safi kwa kupima pamoja naye.
 
Mkuu kama umefuatilia hii thread tangu ilivyoanza utagundua kuwa nimeshapima, na tena nimerudia kipimo baada ya miezi 3 kama nilivyoshauriwa, sikuchelewa appointment yangu hata dakika moja! Na majibu yake ni kama nilivyoyaposti hapa kuwa kwa bahati yangu tu na hasa msaada wa Mungu wa mababu na nyanya zangu nimetoka salama kwenye mdomo wa mamba bila mkwaruzo wowote! Na masuala ya milupo nk nimestaafu rasmi hata kabla ya sakata hili kuanza, lakini sasa nimepigilia muhuri kabisa, utulivu 100%
 
Back
Top Bottom