Ex- DC Mnali for PRESIDENT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ex- DC Mnali for PRESIDENT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sikonge, Feb 18, 2009.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Chadema,

  Nafikiri kuna haja ya kumchukua huyu jamaa na kuwa mgombea ubunge wilaya za Mbeya au hata huko Bukoba au kwao (sijui anatoka wapi). Na kama ikiwezekana basi apelekwe shule na kumuandaa kwa mwaka 2015 kuwa mgombea Urais. Maana watu wakorofi kama hawa wanaweza kuishia kuwa akina Idd Amin kama hawatakuwa na shule. Ila kwa kuanzia angelifaa sana kuwa walau Waziri Mkuu.
  Nina imani kokote atakapogombea na kushinda ubunge, basi uzembe mdogomdogo utaisha. Huyu jamaa utamlaani weee, ila mwisho wa siku unakuwa unakubali kuwa "walau huyu kaamua kufanya kitu positive". Kawa na uchungu na nchi yake. Wengine si tu kuwa hawana uchungu na nchi yao ila wao "wananyonya damu za Watz hadi matone ya mwisho".
  Yes, MNALI FOR PRESIDENT!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Date::2/16/2009 ( Mwananchi Read News )
  Bukoba: DC aungwa mkono kwa walimu kuchapwa viboko
  *Polisi wazima mpango wa waalim kuandamana kulaani adhabu hiyo

  Na Lilian Lugakingira

  Walimu mkoani hapa walikuwa wamepanga kuandamana jana lakini maandamano hayo hayakufanyika kutokana na kutopata kibali cha Jeshi la Polisi, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Chama cha Walimu cha Kagera, Dauda Bilikesi.


  Bilikesi alisema kuwa walimu walikuwa wamepanga kufanya maandamano ya amani kulaani kitendo cha mkuu huyo wa wilaya ya Bukoba cha kuwachapa walimu viboko, na kuwa kunyimwa kibali cha kufanya hivyo ni kunyimwa haki yao ya kujieleza na kutoa hisia zao.


  Taarifa kutoka ndani ya jeshi la polisi zimesema kuwa, walimu hao walinyimwa kibali kutokana na kuhofia kuvunjika kwa amani. Hata hivyo, kamanda wa polisi mkoani hapa, Henry Salewi hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo.


  Wakati walimu wakishindwa kuandamana, wakazi wa wilaya ya Bukoba wanamuona DC Mnali kuwa alifanya kitendo sahihi cha kuchapa walimu viboko, wakidai kuwa utoro, uchelewaji na uzembe umezidi.

  Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti, wakazi hao walisema kuwa adhabu aliyoitoa rais kwa mkuu huyo haistahili, wakisema kuwa walimu hao walistahili adhabu hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya utovu wa nidhamu.
  Wakazi hao waliitupia lawama serikali iliyopitisha utaratibu wa walimu kupewa mikopo ambao wamesema umechangia kwa asilimia kubwa walimu kukiuka maadili ya kazi yao, ikiwemo kufanya biashara saa za kazi na kushindwa kufundisha.


  Helleni Lianda, mkazi wa kata Kashai katika manispaa ya Bukoba, alisema kuwa wapo baadhi ya walimu ambao wanafanya kazi zao kwa kufuata misingi na taratibu za kazi, lakini walimu walio wengi wamejiingiza katika biashara na kuwa wanapaswa kuchagua moja, kama kuingia madarasani kufundisha au kufanya biashara.


  "Ni haki yao kupigwa viboko; wanafanya biashara saa za kufundisha; wanafika kazini wakiwa wamechelewa; wanapiga soga kazini badala ya kufundisha. Mimi sioni sababu ya kumwadhibu DC eti kwa sababu kawapiga walimu, ni haki yao," alisema Lianda.


  Naye Beatrice Mshumbusi, mkazi wa kata Hamugembe, alisema walimu walistahili kuchapwa viboko, akidai kuwa wamekuwa kero hasa kutokana na vitendo vyao vya kulewa saa za kazi, hali inayosababisha wengi wao kuwa wachafu kupindukia.
  Mbali na asilimia kubwa ya watu waliohojiwa kuonekana kumuunga mkono mkuu huyo wa wilaya, wapo baadhi ambao wamesema kitendo cha kuwachapa viboko walimu sio cha kiungwana maana zipo taratibu za kumwajibisha mtumishi wa serikali anayeenda kinyume na taratibu za kazi, sio kumchapa viboko.

  Baadhi ya wazazi walisema wanaandaa maandamano kupinga kitendo cha kumwajibisha mkuu wa wilaya ya Bukoba kwa sababu ya kuwapiga walimu viboko.Mzazi mmoja wa Hamugembe aliyejitambulisha kwa jina la Athuman alisema kuwa endapo Jeshi la Polisi litatoa kibali kwa walimu hao kuandamana kuunga mkono uamuzi wa Rais Kikwete, na wazazi wataandamana kupinga hatua hiyo.


  Tuma maoni kwa Mhariri
   
 3. Sabasaba

  Sabasaba Member

  #3
  Feb 18, 2009
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Nafikiri kuna haja ya kumchukua huyu jamaa na kuwa mgombea ubunge wilaya za Mbeya au hata huko Bukoba au kwao (sijui anatoka wapi). Na kama ikiwezekana basi apelekwe shule na kumuandaa kwa mwaka 2015 kuwa mgombea Urais. Maana watu wakorofi kama hawa wanaweza kuishia kuwa akina Idd Amin kama hawatakuwa na shule. Ila kwa kuanzia angelifaa sana kuwa walau Waziri Mkuu.

  sidhani huyu Albert Mnali anastahili sifa zote ulizommwagia ana controversial personality mainly on abuse of power akiwa na madaraka yake ya uDC.

  huyu bwana nakumbuka ni mwaka 2006 au kabla yake alipata scandal ya kupigwa na mwananchi mwenye hasira wilayani Geita kwa sababu alimshika shanga mke wa mtu hadharani, kitendo hicho kikaleta kashikashi akapigwa, naye kwa ulevi wa madaraka akaamuru police wamdhalilishe mume wa mtu, bila kuangalia uzito wa kosa alolifanya!

  Ni circumstance zimempa advantage DC wa zamani bw mnali, lakini i mtaalamu mzuri tu wa kuchemsha!
   
 4. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #4
  Feb 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Tz ili inyooke inahitaji mtu kichaa kama huyu!

  Uzembe..basi ni mboko!!!

  Ila cheo cha uraisi hapana...awe chini ya mtu ...may be Waziri Serikali za Mitaa!

  Nchi za Afrika tunahitaji utaratibu wa China!

  Ni dhambi kubwa kulea wizi, ubadhirifu na uzembe!

  Eti mtu kasababisha upotevu wa 200 billions...na ana majumba kibao kila kona ya Dar..alafu unampeleka Kisutu kutumia pesa ya kodi kuangalia kama ana hatia!

  Halafu mtu huyu huyu anahonga zile pesa alizoiba hakimu..halafu anaachiwa..na na anadai fidia kwa kudhalilishwa!

  Nasema...uzembe, wizi, ubadhirifu...mboko kwanza tena mbele ya mke wake!
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sabasaba,
  uko sawa. Ndiyo maana nikasema kuwa anatakiwa kuanzia cheo cha chini huku akipata shule jinsi ya kujiheshimu. Tatizo la Tanzania watu/viongozi wako free sana kufanya watakalo. Na hapo nikasema huyu anaweza kuwa Idd Amin. Sasa kuzuia mnamuanzia kama Mbunge na akiwa poa basi aende PM na ikibidi hata Rais kwa baadaye. Kama atashindwa kuacha ujinga wake basi mnamtema. Unajua binadamu wengi wakiwa na nafasi basi wanamess-up sana. Ila sheria tu zinatuzuia kufanya hivyo.
  Kama ni kushika shanga hilo ni sawa na akina Clinton tu. Ila heri ya mshika shanga kuliko FISADI.
   
 6. s

  skasuku Senior Member

  #6
  Feb 18, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kitu alichofanya huyu DC ni cha aibu na kuna ulazimu wakuchukuliwa hatua. Jamaa amevunja sheria nyingi sana hapa ( wale wanasheria hebu tujulisheni ). Kiongozi huwezi kurupuka na kuanza kuongoza watu kana kwamba ni familia yako. kuna processes ambazo alitakiwa kufuata.

  Tanzania kuna sheri, process, nyingi nzuri, tena ambazo ni za maendeleo, ila viongozi wetu wengi (sio wote) ni mbumbumbu, wamelewa madaraka, na wanadhani nchi ni yao.

  Kwangu mimi ninasema huyu Mnali afunguliwe mashitaka ya kukiuka haki za binadamu, kutumia madaraka vibaya, kuvunjia watu hshima...... funga hii mtu
   
 7. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #7
  Feb 18, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160

  Hao wanaofuata sheria ktk wizi wa EPA? au Richmond?

  Mboko kwanza...halafu sheria baadae! sasa kama waalimu hawafundishi je wabembelezwe wakati wanalipwa mshahara?

  Hii itasaidia Afrika tubadilike!
   
 8. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #8
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Nakumbuka huko nyuma wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere tulikuwa tukichapana mboko, na ilisaidia sana kwa maana hakuna mwanakijiji (kijijini kwetu) ambaye hakuwa na chakula angalau cha kumtosha yeye na familia yake kwa mwaka mzima; lakini leo hii kwa kisingizio cha "haki za binadamu" tunalea uzembe hadi kuna watu eti wanalia njaa na wakati hakujakuwa na ukame wa kutisha wala nini!!

  I support Mnali!!
   
 9. e

  eddy JF-Expert Member

  #9
  Feb 18, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,383
  Likes Received: 3,775
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa mjadala wa DC waunahoja kwani alishafutwa kazi, sasa tuwajadili walimu ambao mpaka sasa hawajachukuliwa hatua yeyote, tatizo hasa ni nini?

  Walimu wengi wa vijijini waliyapapatikia mahela ya wajasiriamali, mabank hasa CRDB na NMB yaliwajaza mapesa kwa kuona tayari wako organised na ni rahisi kuwabana kulipa. Wengi wa walimu wameanzisha biashara za pikipiki maarufu kama bodaboda, basi siku nzima wako na pikipiki.

  Tatizo sio kubwa mijini kwani tayari walishapata uzoefu kutoka Pride na Finca hivyo hawakuyakimbilia. waliochukua walizitumia kumalizia vibanda vyao na kuendelea kufundisha kama kawaida.
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Duh! na nyie Chadema kwa mazagazaga hamjambo!
   
 11. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2009
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  Kwa hali ilivyo tanzania tunahitaji that kind of leadership. As far as asiwe fisadi basi thats what we want. remember Moringe?? remember naibu waziri mkuu na waziri wa mambo ya ndani Lyatonga? even Keenja Dar. They managed kwani uswahiliswahili ni mwingi.
   
Loading...