EX-BF ananitaka tena na wakati kaoa tayari, nifanyeje?

Pretty! huyo xbf yako muulize maswali yafuatayo:

1. Kama anakupenda kwa dhati na anaona unaumuhimu kwako basi muulize why alioa akakuacha?
2. Je anaweza akaachana kabisa na huyo mkewe then mkafunga ndoa nyote mkaishi pamoja?

Nauhakika atapatwa na kigugumizi hatoweza kutekeleza hayo nawe hapo akili kumkichwa unampiga chini kama yeye alivyokuacha na kuoa mwanamke mwingine.

Usisahau kumwambia hivi ".....We wa nini wenzake wanauliza watakupaa lini...."
Shosti tulia usiwa na BP watakuja wengi tu wakukuliwaza nae utachagua anae kufa...
 
I dont buy that...

una beep au? huenda ni wewe unataka kumjulisha mke wa jamaa kuwa nawe upo kwenye utatu wao.
 
Saa ingine watu wanshabikia tu!

Inategemea ma mazingiza!

Hebu fikiria- wewe ni biniti na ulikuwa na BF na akaoa say 8 years ago! Na wewe umesubiri miaka inaenda sasa ni 35 wala kujapata mtu na unahitaji mtoto! Je utapata bwana wapi wa kuzaa nae hata mtoto mmoja? Kama ulikuwa na BF na mlipendana na nakuambia ni rahisi wewe kama binti kumlilia shida BF wako wa zamani kuliko mtu mwingine tu!

Yote ni maisha tu! Waschana wengine hamkuwahi kuwa na kiu ya kutafuta mtoto wakati umri ndo unaenda!
 
Ungeelezea kwanza sababu za kukuacha wewe na kuoa mwanamke mwingine
 
BABY COME BACK.
Mpe mambo wa usumcheleweshe ana njaa na wewe huyo.

Kandambili usimpotose Prety, kwa ufahamu wangu mtu akishaaoa inamaana amempenda zaidi yule aliyemuoa. kwa hiyo Prety wala usiangaike nae kabisa huyo EX - BF. alikuona wewe sio wa thamani kwake ndio maana aliamua mwanamke/msichana mwingine. lakini naomba nikuulize swali moja;

Kwa nini mliachana?
 
kuna tofauti kubwa kati ya mwanamke wa kuoa na mwanamke wa kustarehe,mwanamme kuoa mtu mwingine na kukuacha wewe haimaanishi hakupendi ila wewe ni mzuri kustarehe kuliko kuolewa.sio kila mwanamke wa kustarehe anafaa kuoa,ndio sababu unaona wanaume wengi wanatafuta mirupo ya kustarehe wkt wana wake zao nyumbani.
 
wana jf nisaidieni


Noma achana naye,Tulia sahihisha makosa yalisababisha asikuoe na songa mbele.Niliwahi kukutana na tatizo kama lako kwa ex -gf wangu ,nilichofanya ni kukaa kimya,let the bygone bygone.
 
Naamini unaye mwingine sasa. Kama hivyo ndivyo, basi mchukue uende naye kwa huyo ex-bf wako muwaombe wawe wasimamizi wa ndoa yenu. Mkewe matron, jamaa bestman!
 
Naamini unaye mwingine sasa. Kama hivyo ndivyo, basi mchukue uende naye kwa huyo ex-bf wako muwaombe wawe wasimamizi wa ndoa yenu. Mkewe matron, jamaa bestman!

Duu hapa patakuwa patamu, mtu aweza zimika akiona busu likiteremka kwenye shavu la bibi harusi kwikwi.. si unajua wivu bwana..
Ila ni dawa safi kabisa. Usikubali kuwa day worker!
 
sasa si bora huyo unayemjua kuliko vicheche wapya? mpe mambo ki pati taimu wakati ukivizia wako wa kudumu!

Hahahaha! hapa sina mbavu uwiiii! PATI TAIMU AKIVIZIA WAKE.

Mi huwa nawashauri watu ukiachana na mtu mliopendana sana akaoa unakata mawasiliano kabisa ikiwezekana unabadilisha namba ya simu kabisa.
 
Nadhani hapo jibu unalo cha muhimu hapo mpe mambo kimya kimya tu lakini mke wake asijue kabisa maana akijua itakuwa so........

N.B nadhani umepotea kuja kuuliza swali kama hili hapa barazani ungeuliza swali lingine lakini kuhusu swala la mapenzi sidhani kama hapa kuna jibu la maana la kuweza kupewa ukapenda unavyotaka maana kwanza utamu wa mapenzi unayajua wewe na yeye jinsi alivyokuwa akikukunja kitandani unafahamu wewe na yeye so hamna mdau wa hapa JF anafahamu so ukiuliza swali kama hilo linakuwa gumu sana kujibu ongea na moyo wako ndio utakujibu zaidi nini ufanye kama unaona bado roho yako ipo pale mpe mambo kama kawaida...........yangu ni hayo tu.
 
Dada sahau yaliyo pita, hata kama ni vigumu. kama angekudhamini angekuoa wewe. Kama mazingira hayakuruhusu kukuoa wewe basi jua Mungu haukupangia huyo kuwa mmeo. Asikudanganye, kuendelea naye mnaanzisha mgogoro ambao wewe na yeye mtakuja kujiraumu baadae.Kuuliza swali hilo maana yake bado mpaka sasa huna BF. vumilia tu hata kama unakosa hiyo huduma mhimu. Utapata 'the right person', time will tell.
 
Mmh Kiteiteu, ushauri wako jamani lol! Pretty mfute kwenye maisha yako, atakupotezea bahati zako bure{ najua ni ngumu maana mnajuwana tayari}
 
Mpaka umeuomba msaada basi unamajibu mengi yaani kuumpa tena au kumnyima! Siwezi kusema humpendi au unampenda bado; lakini kumpa au kumnyima inategemeana na wewe tabia yako, makuzi yako, msimamo wako, imani yako, n.k. Kama ukimpa basi tabia yako machoni pangu ni MBAYA, HUFAI. Kama ukimnyima basi UNAWEZA UKAWA NA TABIA NZURI.
Anakuja mume wa mtu kukutongoza, una ananza kuomba msaada!!! Ishii Wewe vipi????
 
Mmh Kiteiteu, ushauri wako jamani lol! Pretty mfute kwenye maisha yako, atakupotezea bahati zako bure{ najua ni ngumu maana mnajuwana tayari}

Kumbe wewe, VIOLET, mtu unaejuwana nae akikuomba unampa eti unajuwa ni ngumu? Anyway inawezekana ni tabia yako.
 
Mimi ninakupa ushauri wa uhakika

Hakikisha huyo jamaa anakuja ghetto kwako usiku, then muulize saa ngapi atapenda kuondoka, hakikisha dakika 5 - 10 kabla ya muda wa kuondoka unaloweka nguo zake kwenye maji au zifiche kabisa asizione, nadhani hapo utapata jibu la swali lako.
 
Back
Top Bottom