EWURA yatangaza bei mpya za mafuta zitakazoanza kutumika leo

Dazzle 2

Senior Member
Oct 9, 2015
125
225
Leo kama ilivyo ada bei mpya ya mafuta ya petrol, diseli na mafuta ya taa itatangazwa na EWURA. Je ikitokea imepanda na kuathiri maisha ya wanyonge itatumbua mtu ili wanyonge sisi tusipate shida?

======

UPDATE;

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA) imetangaza bei mpya za nishati ya mafuta zitakazoanza kutumika leo Jumatano huku bei ya mafuta ya taa na dizeli ikiwa imeshuka kwa wastani wa shilingi 66 kwa lita.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix Ngamlagosi inaonesha kuwa kwa wastani kumekuwa na ongezeko dogo sana la bei ya mafuta ya petroli ambayo kwa jiji la Dar es Salaam bado itauzwa kwa bei ile ile ilivyokuwa mwezi uliopita.

Hata hivyo, taarifa hiyo imetoa ruhusa kwa wauzaji wa jumla na rejareja wa mafuta nchini kuuza bidhaa hiyo kwa bei ndogo chini ya bei elekezi iliyotangazwa na mamlaka hiyo kama njia ya kuchochea ushindani baina ya wauzaji wa mafuta nchini.
 

Lubebenamawe

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
1,363
2,000
Kwa mkwara ulionyeshwa kwa TANESCO jamaa wa EWURA sasa yuko kikaangoni. Kwa mchecheto anaweza shindwa kutanga bei elekezi ya mafuta.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom