EWURA, yatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini.

Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 7 Novemba 2018. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia
yafuatayo:-

(a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote (Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa)
yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, zimeongezeka ikilinganishwa na toleo
lililopita la tarehe 3 Oktoba 2018. Kwa mwezi Novemba 2018, bei za rejareja za Petroli, Dizeli
na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 29/lita (sawa na asilimia 1.22), Shilingi 81/lita
(sawa na asilimia 3.52) na Shilingi 34/lita (sawa na asilimia 1.50), mtawalia. Vilevile, kwa
kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa
zimeongezeka kwa Shilingi 28.74/lita (sawa na asilimia 1.28), Shilingi 80.90/lita (sawa na
asilimia 3.71) na Shilingi 33.58/lita (sawa na asilimia 1.58), mtawalia. Kwa kiasi kikubwa,
ongezeko la bei za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa kwenye soko la ndani limetokana
na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za
usafirishaji wa mafuta (BPS Premium).

(b) Vilevile, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 3 Oktoba 2018. Bei
za Mafuta ya Taa katika ghala la mafuta mkoani Tanga hazijabadilika kwa sababu hakuna shehena mpya ya Mafuta ya Taa iliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga katika mwezi wa Oktoba 2018. Katika toleo hili, bei za rejareja za Petroli na Dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini
zimeongezeka kwa Shilingi 87/lita (sawa na asilimia 3.72) na Shilingi 111/lita (sawa na asilimia 4.89), mtawalia. Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa Shilingi 87.18/lita (sawa na asilimia 3.92) na Shilingi 110.58/lita (sawa na asilimia 5.15), mtawalia. Ongezeko hili la bei za mafuta katika ghala la mkoani Tanga limetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama
za usafirishaji wa mafuta (BPS Premiums).

(c) Hakuna shehena mpya ya mafuta iliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Mtwara katika mwezi
wa Oktoba 2018. Hivyo, katika mwezi wa Novemba 2018, bei za Petroli na Dizeli mkoani
Mtwara, Lindi na Ruvuma zitaendelea kuwa kama zilivyokuwa mwezi Oktoba 2018. Kwa kuwa
hakuna Mafuta ya Taa yaliyopokelewa katika bandari ya Mtwara, wamiliki wa vituo vya mafuta
katika mikoa tajwa wanashauriwa kununua mafuta hayo kutoka Dar es Salaam na hivyo bei za
rejareja za Mafuta ya Taa kwa mikoa hiyo zinatokana na gharama za mafuta hayo kutokea Dar
es Salaam na kusafirishwa hadi mkoa husika.
 
Hivi anayetakiwa kusimamia mafuta ya taa kufika mikoani au kila sheli ni nani ? Esp sumbawanga ???
 
Baadae kidogo utamsikia mtakwimu mkuu wa serikali akisema inflation imepungua kwa asilimia moja.
 
Hivi kuna tatizo gani na bei ya mafuta?. Kila kukicha kuna nyongeza ya bei. Muda siyo mrefu bei ya petroli kwa lita itafka 3000.
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini.

Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 7 Novemba 2018. Pamoja na kutambua bei kikomo za bidhaa mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia
yafuatayo:-

(a) Bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya aina zote (Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa)
yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, zimeongezeka ikilinganishwa na toleo
lililopita la tarehe 3 Oktoba 2018. Kwa mwezi Novemba 2018, bei za rejareja za Petroli, Dizeli
na Mafuta ya Taa zimeongezeka kwa Shilingi 29/lita (sawa na asilimia 1.22), Shilingi 81/lita
(sawa na asilimia 3.52) na Shilingi 34/lita (sawa na asilimia 1.50), mtawalia. Vilevile, kwa
kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa
zimeongezeka kwa Shilingi 28.74/lita (sawa na asilimia 1.28), Shilingi 80.90/lita (sawa na
asilimia 3.71) na Shilingi 33.58/lita (sawa na asilimia 1.58), mtawalia. Kwa kiasi kikubwa,
ongezeko la bei za mafuta ya Petroli, Dizeli na Mafuta ya Taa kwenye soko la ndani limetokana
na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama za
usafirishaji wa mafuta (BPS Premium).

(b) Vilevile, bei za jumla na rejareja kwa mafuta ya Petroli na Dizeli yaliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la tarehe 3 Oktoba 2018. Bei
za Mafuta ya Taa katika ghala la mafuta mkoani Tanga hazijabadilika kwa sababu hakuna shehena mpya ya Mafuta ya Taa iliyoingizwa nchini kupitia bandari ya Tanga katika mwezi wa Oktoba 2018. Katika toleo hili, bei za rejareja za Petroli na Dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini
zimeongezeka kwa Shilingi 87/lita (sawa na asilimia 3.72) na Shilingi 111/lita (sawa na asilimia 4.89), mtawalia. Aidha, kwa kulinganisha na toleo la mwezi uliopita, bei za jumla za Petroli na Dizeli zimeongezeka kwa Shilingi 87.18/lita (sawa na asilimia 3.92) na Shilingi 110.58/lita (sawa na asilimia 5.15), mtawalia. Ongezeko hili la bei za mafuta katika ghala la mkoani Tanga limetokana na ongezeko la bei za mafuta hayo katika soko la dunia na kuongezeka kwa gharama
za usafirishaji wa mafuta (BPS Premiums).

(c) Hakuna shehena mpya ya mafuta iliyopokelewa nchini kupitia bandari ya Mtwara katika mwezi
wa Oktoba 2018. Hivyo, katika mwezi wa Novemba 2018, bei za Petroli na Dizeli mkoani
Mtwara, Lindi na Ruvuma zitaendelea kuwa kama zilivyokuwa mwezi Oktoba 2018. Kwa kuwa
hakuna Mafuta ya Taa yaliyopokelewa katika bandari ya Mtwara, wamiliki wa vituo vya mafuta
katika mikoa tajwa wanashauriwa kununua mafuta hayo kutoka Dar es Salaam na hivyo bei za
rejareja za Mafuta ya Taa kwa mikoa hiyo zinatokana na gharama za mafuta hayo kutokea Dar
es Salaam na kusafirishwa hadi mkoa husika.
EWURA wanakula njama na WAFANYABIASHARA WA MAFUTA. Sababu wanazotoa wa si za msingi kwa wananchi wa kwaida. Wanaotumia mamlaka ya walionayo kibabe kuwahadaa wananchi.
 
tatizo ni utitiri wa kodi walizoweka utashangaa bei ya mafuta Tanzania ni kubwa ukilinganisha na bei ya Zambia ambao mafuta yao wamepitishia hapa Tanzania.
 
Kodi si tatizo saana mbona zinaeleweka na zinamchanganuo mzuri tu ila hila za wafanya biashara kutaka faida za haraka pasipo kusaidia wananchi. Na EWURA emewekwa kuregurate na kusimmia masirahi ya WAFANYABIASHARA sio wananchi. Watu waliopo EWURA ni kusimmia PERSONAL na PRIVATE interest na sio PUBLIC interest. Serikali ya Wanyonge mbona hamlioni hilo au mpaka watu wagome au waandamane!!?. Mazao ya wakulima yatafikaje sokoni!? Gharama za bidhaa zitashukaje!!!?? Mbona maisha yatakua magumu sana. Korosho mmelivalia njuga na hili jee la usfirishaji limekaaje!!?
 
hao EWURA wenyewe wana petrol station zao wataachaje kushabikia ongezeko la bei za mafuta? halafu cha kushangaza bei ya mafuta katika soko la dunia ikishuka huku bei itaendelea kubaki ile ile.
 
Back
Top Bottom