Ewura yashtua wabunge kwa kuwa na matumizi makubwa


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,988
Likes
5,382
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,988 5,382 280
KAMATI ya Bunge ya Mashirika ya Umma,imeshtushwa na matumizi makubwa yanayofanywa na Mamlaka ya Udhibiti Nishati na Maji(EWURA) kwa wafanyakazi wake.
Gharama hizo ni pamoja na zile zinazotumika kwa ajili ya matibabu ambapo kwa mwaka zinafika milioni 150,vikao vya bodi milioni 225,mafuta milioni 90 kwa ajili ya magari yao.

Wakati gharama kwa ajili ya mawasilinao ni shilingi milioni 66 kwa mwaka ambapo kila mfanyakazi huwekewa muda wa maongezi kutokana na Idara anayoifanyia kazi ikifika.

Wakitoa maoni yao kwa nyakati tofauti mara baada ya kupokea taarifa ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali(CIG),wabunge hao walisema gharama hizo ni kubwa sana ukilinganisha na uchanga wa Mamlaka hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo,Halima Mdee,alisema kitendo cha Mamlaka hiyo kugharamia matibabu ya mfanyakazi mmoja mmoja kuna hatari kubwa ya kughushiwa kwa risiti kwa matibabau ambayo mfanyakazi hajayapata jambo amablo litaitia Mamlaka hasara.

“Mimi kwa ningeshauri katika hili ili kupunguza gharama hizi ni vyema Ewura mkajinga na Mfuko wa Bima ya Afya,ambapo mfuko huo una uwezo wa kugharamia matibabu ndani na nje ya nchi kwa magonjwa takribani 999 bila kujali kiwango cha mshahara anachopata mfanayakazi.

“Kwa staili mnayoitumia kutoa fedha za matibabu ipo siku atakuja Mkurugenzi yoyte katika Mamlaka hiyo,asiyekuwa na huruma na fedha za walipa kodi,kwenda kutibiwa mafua nje kwa sababu tu fedha hizo zinatolewa na ofisi,”alitahadharisha Mdee.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Kabwe Zitto,alisema haoni haja ya wafanyakazi kuwekewa muda wa maongezi kwenye simu zao na badala yake wanagetumia ‘rediocal’ ili kupunguza gharama zisizo za lazima.

“Katika taarifa yenu inaonyesha kwamba kwa mwaka kiasi cha shilingi milioni 66 zinatumika kwa ajili ya kuwekea wafanyakazi muda wa maongezi,hii ni pesa nyingi sana inatumika,na mna uhakika gani kama muda huo wa maongezi unatumiwa kwa ajili ya shughuli za kazini tu na si vinginevyo,?”alihoji Zitto.

Akijibu hoja hizo,Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka hiyo,Simon Sayore,alisema sula la mafuta walipendekeza kutoa mkopo wa magari kwa wafanyakazi na kuwakata kidogokidogo kwenye mishahara yao baada ya kuona endapo wangetumia magari ya ofisi gharama ingekuwa kubwa zaidi ya ilivyo sasa.

Wakati kuwawekea muda wa maongezi,Sayore alisema kunatokana na aina za kazi ambazo wamekuwa wakifanya kwa masaa kwamba sio kazi za kukaa ofisini bali ni kazi za kwenda mitaani.

Akifafanua zaidi alisema kwa upande wao utumiaji wa ,redio call’ wanaona sio mawasiliano salama kwao ukilinganisha na kazi ambazo wanazifanya.

Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo,Huruna Masebu alisema suala la kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya watakutana na kulijadili kwa unadani ili kuona ni jinsi gani wataweza kujiunga.


http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2156470&&Cat=3
 

Forum statistics

Threads 1,251,538
Members 481,766
Posts 29,775,489