Ewura yashitukia mradi wa mabilioni ya fedha wa Songas | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ewura yashitukia mradi wa mabilioni ya fedha wa Songas

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Farmer, Feb 28, 2009.

 1. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,582
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Date::2/28/2009
  Ewura yashitukia mradi wa mabilioni ya fedha wa Songas
  Na Ramadhan Semtawa

  MAMLAKA ya usimamizi wa Huduma za Maji na Nishati (Ewura), imeshitukia na kukataa gharama kubwa za kuandaa na kupanua wigo wa miundombinu ya kusambazia gesi ya Kampuni ya Songas.

  Gharama hizo zimefikia Sh 66 bilioni (dola 65.7milioni) lakini badala yake, Uwera imelekeza iwe Sh 55 bilioni (dola 54.5 milioni).

  Uamuazi huo ambao ulifikiwa katika mkutano wa Bodi ya mamlaka hiyo uliofanyika Februari 24 mwaka huu, umekuja wakati Songas ikiwa inatekeleza mradi wa kutafuta gesi katika eneo la Songosongo, wilayani Kilwa.

  Akitangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, alisema pamoja na kukataa gharama hizo kubwa, mamlaka pia imeitaka Songas kutoingia mikataba mipya inayoingiliana na shughuli za udhibiti, bila idhini yake.

  "Kimsingi, mradi wa Songas ni mzuri na mamlaka inaukubali, hilo liko wazi, lakini kuna maeneo ambayo mamlaka imeona ni vema gharama zake, zikashuka ili kulinda maslahi ya taifa na mtumiaji, yapo ambayo imekubaliana na Songas," alifafanua Masebu.

  Akifafanua sababu za kukataa gharama hizo za mradi, Masubu alisema zinatokana na utafiti wa kitaalamu na uliozingatia maslahi ya taifa, mlaji na mwekezaji.

  Kwa mujibu wa Masebu, utafiti wa kitaalamu wa mamlaka uliozingatia miradi mikubwa ya kimataifa kama huo, umeonyesha kuwa kiasi kilichopendekezwa na Songas ni kikubwa na kitawaumiza watumiaji wa huduma.

  Alisema mamlaka yake pia imekataa na kutoa maelekezo ya gharama za uendeshaji na huduma kutoka dola 4, 132,000 ( zaidi ya sh 400 milioni) hadi kufikia dola 238,000 (zaidi ya sh 238 milioni).

  Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, alisema , mamlaka katika mradi huo wa miaka 14, pia imepunguza asilimia moja kutoka asilimia 16 hadi 15 ya gharama zilizopendekezwa na Songas, katika mchanganuo wa kazi za jumla.

  Alisema hatua hiyo ya kuondoa asilimia moja, ni sawa na kupunguza dola 19 milioni (takribani sh 20 bilioni).

  Hali kadhalika alisema mamlaka imekataa ombi la kutaka kampuni hiyo, iendelee kulipwa riba katika kipindi cha miezi sita zaidi, baada ya kuanza kazi na badala yake itaishia pale kazi itakapoanza rasmi.

  Kwa mujibu wa Masebu, kama Songas itaendelea kulipwa riba katika kipindi cha miezi sita baada ya kuanza, mtaji utakuwa ni sawa na kutoa faida juu ya faida.

  Alisema kwa mujibu wa sheria, Ewura ina mamlaka ya kuangalia mikataba yote katika sekta zilizoanishwa ili kuona kama inazingatia maslahi ya taifa.

  Katika hatua nyingine, Bodi ya Ewura, imesitisha mchakato wa kutathimini ombi la Pan African Energy Tanzania Limited (PAT) baada ya kampuni hiyo na Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), kushindwa kuwasilisha takwimu na taarifa za uhakika za kuiwezesha mamlaka, kukokotoa faida inayostahili katika mtaji wa uwekezaji wa mradi wa kukuza soko la gesi asilia.

  Mamlaka katika kuonyesha meno, imetangaza kwamba pasipo kuathiri maamuzi ya sheria, kuanzia Aprili mosi, mwaka huu tozo kwa huduma ya kusambaza gesi asilia (DT2), itakuwa senti 52 za Marekani kwa kila ujazo wa Giga Joule hadi mamlaka itakapotoa uamuzi mwingine, kufuatia PAT na TPDC kuwasilisha ombi jipya.

  Ewura pia imezitaka TPDC na PAT kuwasilisha uthibitisho wa bei za gesi asilia kwa ajili ya wateja wa viwandani ifikapo Machi 31 mwaka huu.


  source : Mwananchi
   
Loading...