Ewura yapandisha viwango vya adhabu kwa mafuta

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
EWURA%288%29.jpg

Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura)



Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imepandisha zaidi ya mara mbili viwango cha adhabu kwa wafanyabiashara watakaokutwa na kosa la kuchanganya mafuta ya taa na dizeli.
Hatua hiyo ya Ewura inalenga kukomesha vitendo vya kuchakachukua mafuta vinavyofanywa na wafanyabiashara kwa lengo la kujipatia faida kubwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu, alisema mtu akifanya kosa kwa mara ya kwanza adhabu yake imepanda kutoka Sh. milioni tatu hadi Sh. milioni saba, akirudia mara ya pili atatozwa Sh. milioni 25 badala ya Sh. milioni tano za awali.
Aidha, atakayebainika kufanya kosa hilo kwa mara ya tatu, atanyang'anywa leseni na kufunga kituo chake.
Kwa upande wa wauzaji wa jumla watakaobainika adhabu yake uitakuwa Sh. milioni 10 na kosa la pili imepanda itakuwa Sh. milioni 100 na ikiwa atafanya ksoa hilo kwa mara ya tatu atafungiwa leseni kwa miezi 12 na kulipa Sh. milioni 100.
Alifafanua kuwa upande wa wasafirishaji adhabu yao kwa kosa la kwanza itakuwa Sh. milioni saba kosa la pili Sh. milioni 15 na akirudia mara ya tatu atalipa adhabu ya thamani ya mafuta halisi kwa kiwango atakachokutwa nacho. Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, Masebu alisema lengo la kupandisha adhabu hiyo ni kuweka msisitizo katika kudhibiti vitendo vya kuchakachukua mafuta.
Alitoa mfano kuwa mwaka 2009 Ewura ilifanya ukaguzi kwenye maghala ya kuhifadhia mafuta katika kampuzi za BP (T) Ltd na Orryx Oil (T) Ltd na kubaini kwamba walikuwa wamechakachuwa mafuta yao ambapo walipigwa faini Sh. milioni 10 na kufunga maghala hayo.
Hata hivyo Tume ya Ushindani Nchini FCC ilibatilisha maamuzi hayo ya Ewura na hivyo vituo hivyo vikafunguliwa.
Kwa upande wa kupambana na vituo vinavyouza mafuta bila ya kufuata taratibu, alisema zaidi ya vituo 20 vimefungwa kutokana na kosa hilo baada ya kufanyiwa ukaguzi Aprili mwaka huu.
Wakati huo huo, Masebu alisema uchunguzi umeonyesha kuwa mafuta yaliyojazwa kwenye magari ya Ikulu hayakuwa na ubora unaotakiwa.
Alisema tayari mfanyabishara wa kituo hicho cha mafuta mkoani Kilimanjaro amepigwa faini pamoja na kumfungia biashara yake.
Magari ya Ikulu yalikumbwa na tatizo hilo June 8 mwaka huu ambapo baada ya kuwekewa yalizimika na ksuhindwa kuwaka.



CHANZO: NIPASHE
 
Hii issue ni ngumu kidogo, hawa jamaa wanaouza mafuta wana hela... na wakugunduliwa huwezi amini wanawatuliza hawa jamaa wa EWURA na hakuna kinachofanywa, wanaendelea kuuza mafuta kama kawaida....

Nina mifano hai
 
Matatizo haya hayatakwisha mpaka EWURA yeyenye waache kupokea Rushwa kwa hao Wahalifu wa Mafuta.Ndio matatizo hayo ya kuuza mafuta ovyovyo yatakavyokwisha Viongozi wanaohusika wanayajuwa lakini wameyafumbia macho hayo matatizo. Kazi kweli Waswahili husema MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO.
 
Je yule alieharibiwa gari lake kwa kuwekewa mafuta feki atafidiwa vipi?...dawa hapa ingekuwa ukigundua umewekewa mafuta feki ufidiwe kiasi kadhaa toka kwa aliekuuzia
 
Back
Top Bottom