EWURA yafuta makampuni manne kwa kushindwa kuuza mafuta jumla

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imezifutia leseni za biashara kampuni nne za uuzaji wa mafuta baada ya kampuni hizo kushindwa kufanya biashara ya mafuta kwa jumla kulingana na sheria na taratibu za kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na EWURA na kusambazwa katika vyombo mbalimbali vya habari, imezitaja kampuni hizo kuwa ni Alser Limited lenye leseni No PWL-2017-001, Enoc Africa Limited , Express Oil Limited pamoja na Apex Energy Limited zote za jijini Dar es Salaam.

“Maamuzi ya kuzifungia kampuni hizo yalifikiwa baada ya Bodi kujirishidha kuwa makampuni hayo yote yameshindwa kutekeleza kifungu cha 143(1)(a) cha sheria ya Mafuta sura ya 392 na kanuni ya 16(3) ya kanuni za Petroleum ,toleo la gazeti la Serikali Na.380 la 2018" ilisema taarifa hiyo kupitia kwa Mkurugenzi wake Godfrey Chibulunje.

Aidha Ewura imezitaka kampuni ambazo hazijaridhika na maamuzi hayo ya bodi ya wakurugenzi kukata rufaa katika baraza la ushindani kwa mujibu wa sheria ya Ewura sura ya 414 na sheria ya ushindani sura ya 285.

Hata hatua ya Ewura ya kuzifutia leseni kampuni hizo imekuja ikiwa ni baada ya siku chache tangu Mamlaka hiyo iwatangazie wafanyabiashara hao kufuata sheria za uendeshaji wa biashara hiyo na kusisitiza kuwa kinyume na hivyo ingewafutia leseni.
 
Back
Top Bottom