EWURA yaapa kuwashughulikia wanaochakachua mitungi ya Gesi

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mamlaka ya udhibiti wa Nishati, maji na Mafuta (Ewura) mkoa wa Arusha imewataka wafanyabiashara na wakala wa mitungi ya gesi mkoani hapa,kuhakikisha wanatumia mizani katika kuuza bidhaa hiyo na kuepuka udanganyifu ili kulinda maslahi ya mlaji.

Akiongea na wauzaji na masambazaji wa gesi katika semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo, iliyoandaniwa na kampuni ya Taifa Gesi,meneja wa Ewura kanda ya Kaskazini ,mhandisi Lorivii Long'idu,aliwakumbusha wafanyabiashara wajibu wa kutii sheria na kanuni katika kuuza mitungi ya gesi bila kuchakachua.

Alisema ewura imekuwa ikiendesha operesheni kwende maduka ya wafanyabiasha wa gesi za majumbani na kufanikisha kuwakamata wafanyabiashara wawili mkoani Kilimanjaro ambao wamekuwa na tabia ya kuchakachua mitungi ya gesi na kuwauzia wateja ikiwa pungufu.

"Ni kosa kubwa kisheria kuuza gesi bila kuwa na mizani na mwananchi anayenunua mtungi wa gesi ahakikishe mtingi ameupima kupata uzito unaostahili"alisema.

Kwa upande wake meneja wa mauzo Taifa Gesi,Joseph Nzumbi alisema semina hiyo inalenga kuwajengea uwezo wauzaji na mawakala wa gesi ili waweze kuendesha biashara hiyo kwa usahihi zaidi kwa kuwa biashara ya gesi majumbani kwa sasa imekua kwa asilimia 5.

Alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha wananunua mitungi ya gesi yenye uzito sahihi kwa kupima uzito wa mtungi kwenye mizani kabla ya kuinunua.

Naye afisa vipimo mkoa wa Arusha Jasson Theonest ,aliwataka wafanyabiashara wanaouza mitungi ya gesi kuhakikisha wanakuwa na mizani iliyohakikiwa na wakala wa vipimo ili wanapomuuzia mlaji awe na ihakika na ujazo wa bidhaa aliyonunua.

Alisema katika mkoa wa Arusha ,wamekuwa wakifanya ukaguzi wa nara wa mara wa vipimo kwa wafanyabiashara na baadhi yao wametozwa faini kutokana na ukikukwaji wa mizani ya vipimo.

Mmoja ya wauzaji wa mitungi ya gesi,Elizabert Marwa ameipongeza kampuni ya Taifa gesi kwa kuwapatia semina ambayo imewasaidia kuwajengea uelewa zaidi juu ya matumizi ya gesi.

Alisema kuwa yeye kama muuzaji wa gesi eneo la Sanawari jijini Arusha,hajawahi kukumbana na changamoto ya kuchakachuliwa kwa mitungi ya gesi ya kampuni ya Taifa gesi na alitoa wito kwa kampuni zingine za gesi kuzingatia maslahi ya mlaji.

IMG-20220519-WA0209.jpg
 
Back
Top Bottom