EWURA watangaza ongezeko la bei ya mafuta karibu maradufu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EWURA watangaza ongezeko la bei ya mafuta karibu maradufu

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by BAK, Jun 15, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,572
  Trophy Points: 280
  Date: 6/15/2009
  EWURA watangaza ongezeko la bei ya mafuta karibu maradufu

  Na Fredy Azzah
  Mwananchi

  WAKATI Mamlaka ya Kitengo cha Taifa cha Takwimu (NBS), kikitangaza kushuka kwa mfumuko wa bei kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta, nauli na bidhaa nyingine, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza kupanda kwa bei za mafuta kwa wastani wa asilimia 46.

  NBS ilitangaza jana kuwa kushuka kwa bei ya mafuta, umeme, maji na nauli kumesababisha mfumuko wa bei kuteremka kutoka asilimia 12 iliyokuwa mwezi Aprili, hadi asilimia 11.3 kwa mwezi Mei.

  "Mfumuko wa bei uko katika mwendo wa asilimia 11.3 kutokana na kushuka kwa bei za bidhaa ambazo si vyakula," Ephraim Kwesigabo, mkurugenzi wa kitengo cha idadi ya watu wa NBS aliieleza Reuters jana.

  Lakini wakati NBS ikitangaza hayo, mkurugenzi wa Ewura, Haruna Masebu alikuwa na mkutano na waandishi wa habari na kutangaza kuwa bei ya petroli imepanda kwa asilimia 46.31, dizeli 11.98 huku mafuta ya taa yakipanda kwa asilimia 13.3.

  Masebu alizitaja sababu zilizosababisha ongezeko hilo kuwa ni pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia pamoja na kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani.

  Alisema kulinganisha bei walizozitangaza Mei 27 mwaka huu, petroli imepanda kwa asilimia 5.47, dizeli kati ya asilimia 2.38 na 2.64 na mafuta ya taa asilimia 3.79.

  Kutokana na ongezeko hilo, bei mpya kwa jiji la Dar es Salaam, petroli itakuwa ni kati ya Sh1,418 hadi 1,524 huku dizeli ikiwa Sh1,338 hadi Sh 1,473 na mafuta ya taa kati ya Sh 860 hadi Sh 924.

  “Kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka huu, bei za mafuta zimekuwa zikipanda japo siyo kwa kiasi kikubwa kama ilivyokuwa mwaka jana. Bei zitaendelea kupanda kutokana na kuimarika kwa uchumi wa dunia na hasa Marekani,” alisema Masebu.

  “Ewura imebaini kuwa bei za mafuta ghafi kwenye soko la dunia imefikia dola 70 za Marekani kwa pipa. Wadadisi wa masuala ya mafuta wanabashiri kuwa huenda bei zikafikia ukomo wa dola 75 za Marekani na hatimaye kushuka kabla ya majira ya baridi Ulaya, Septemba 2009.

  Pamoja na wasiwasi huu, bei za hapa nchini haziwezi kufikia bei za Julai 2008.”

  Hata hivyo, wauzaji wa mafuta wamekuwa wazito kupunguza bei za bidhaa hiyo wakati inaposhuka kwenye soko la dunia, wakisingizia kuwa wanalazimika kuuza kwa bei kubwa kwa sababu bado wanatumia shehena walizoagiza kwa bei kubwa.

  Mapema mwaka huu, bei ya mafuta duniani ilishuka hadi chini ya dola 40 za Marekani kwa pipa, lakini bei iliendelea kupanda hapa nchini kwa kisingizio kuwa meli za mafuta zinashindwa kuvuka pwani ya Somalia kutokana na maharamia kuziteka. Serikali ililazimika kuingilia kati na kuanza kudhibiti bei ya nishati hiyo.

  Kwa mujibu wa Ewura, bei za mafuta katika Mkoa wa Kigoma, dizeli ni Sh1,538 hadi Sh1,688 huku petroli ikiuzwa kwa Sh1,618 hadi Sh1,739.

  Katika Mkoa wa Arusha, petroli itauzwa kwa Sh 1,502 hadi Sh1,614 huku dizeli ikiuzwa kwa Sh1,422 hadi Sh1,528.

  Mwanza petroli itauzwa kwa Sh 1,567 hadi Sh1,685 huku dizeli ikiuzwa kwa Sh1,487 hadi Sh1,634.

  Masebu alisema kituo cha mafuta kitakachobainika kuuza mafuta kwa bei ya juu kuliko iliyotolewa na Ewura kitachukuliwa hatua kali za kisheria.

  Katika hatua nyingine, Masebu alisema mchakato wa kuandaa utaratibu wa kuagiza mafuta kwa pamoja unaendelea na kuwa tayari kampuni ya ushauri wa kitaalamu ya Petrol Development Consultants Ltd ya Uingereza imeshakabidhi rasimu ya pili ya mchakato huo.

  "Kilichobakia ni wadau kuanza kuijadili kwenye mjadala unaotarajiwa kufanyika Juni 23 mwaka huu," alisema.

  Alisema mfumo huo unalenga kupunguza hitilafu zilizobainika kwenye tafiti iliyofanywa Agosti 2007.

  “Utaratibu wa sasa wa kila kampuni kuagiza mafuta yake unasababisha gharama kubwa za usafirishaji, msongamano wa meli bandarini; na hivyo kusababisha ada za ucheleweshwaji wa meli,” alisema Masebu.

   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Kizunguzungu . . . . Ngoja nipate upepo kwanza . . .
   
 3. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Bei kupanda maradufu ni sawa na kusema "bei imepanda kwa asilimia 46"?

  Ingekuwa sawa kama ongezeko la bei ni 94% hivi. (Bei ku-double)
  Au mie ndio nimekosea?
   
 4. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,066
  Trophy Points: 280
  Uchumi wetu hauwezu kuwa stable namna hii, kila mtu anakwenda kivyake! Then 'wajinga' wanasema eti bajeti ya mwaka huu ni babubwa! hivi wanajua hili ongezeko la bei mafuta ya mafuta maana yake nini??!!
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Bei ya mafuta imepanda duniani lakini, so....
   
 6. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,582
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Hii ni kiboko, tutaendesha kweli magari yetu!!!
   
 7. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Wana JF

  Mi naomba kueleshwa jamani....yaani bei ya mafuta kwenye soko la dunia ilishuka leo hii EWURA hapa kwetu wankaa kimyaaaaaaaaaaaaa hawashushi bei ya mafuta kabisaa

  Lakini sasa Bei ikipanda tuuu leo hiii Kesho yake EWURA NA WANAOUUZA mafuta wanapandisha bei haraka sana.

  Sasa mi nashindwa kuelewa hawa EWURA wanafanya kazi gani

  Naombeni mnielewashe naombeni sana
   
 8. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,582
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Kazi yao ni ku-regulate bei inapo panda tu, na sio vinginevyo!!
   
 9. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #9
  Jun 16, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi sipingani nawe kabisaaaaa.....EWURA makini zaidi kupandisha bei kuliko kushusha, i.e hii inatoa mwanya wa kufikiri kuwa nao ni wenye biashara hii either Petrol/Diesel Stations au wanatumika.

  Tembelea website ya OPEC "http://www.opec.org/home/basket.aspx" hapa utaona wazi kuwa bei ya mafuta ghafi imeshuka kuanzia 12 June 2009, na inazidi kushuka lakini EWURA kwa jinsi ambavyo bei ilipopanda tu kuanzia 8th June 2009 kutoka USD 67.02 hadi kufikia USD 70.45 ilipofika 11 June 2009 wao tayari hata haijaisha week tayari wamepandisha bei...na mbona imeanza kushuka kuanzia 12 June 2009 hawakutangaza kushusha bei?.

  Tusitoe visingizio vya kuwa na "stock kubwa" au kushuka kwa thamani ya Tshilling katika hili, hapa ni wizi mtuuuupu wa EWURA na washika pembe wake.

  Jamani, tambueni kuzungumzia kupanda kwa bei ya mafuta hata kwa TShillingi 1(moja) ina madhara makubwa kwa watanzania walio wengi..gharama za maisha zinafanya hata matendo ya uovu(mfano mauaji, wizi, uporaji,ubakaji,ulevi wa bangi n.k) kuongezeka.

  Hii nchi ishauzwa au?....kodi ya pato iko juu kuliko nchi nyingine za bara la Afrika na bado tena mnaleta makamuzi y kimtindo katika mambo ya uhai kama haya?.....du, bora tuhame "TANZANIA tuhamie CHALINZE" labda tutaenda kushangaa njia kuu mbili mbili kwenda Segera, angalau labda utakuwa ni utalii wa ndani utakaopunguza fikra endelevu zinazotuumiza vichwa pindi tunaposhindwa kuzitimiza
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  hivi TSh yetu imekuwa pegged na currency/kitu gani and why........wanaoelewa nisaidieni
   
 11. P

  Preacher JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ha haaaaaaaaaaaa - hiyo imenichekesha sana - afadhali nicheke manake nikiendelea kuwazia haya SUKARI INAPANDA, PRESSURE INAPANDA - inabidi nitafute preacher aniombee.
   
 12. K

  Kasanga Member

  #12
  Jun 16, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili DUDU linaloitwa EWURA limeletwa kuongeza mzigo kwa walala hoi! hebu angalia Ufisadi Huu, Unaponunua umeme kuna pesa unawapa(zinakatwa) hao EWURA! kazi wayofanya ni kulinda maslahi ya wafanabiashara! hakukuwa na umuhimu wa kuwa nachombo ambacho hakiko kwa maslahi ya walalahoi1
   
 13. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #13
  Jun 16, 2009
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Nilishtuka juzi nafika kujaza mafuta kwenye kituo cha Total nakuta bei Tshs 1,495. Kumbe wamebariki bei hizi?

  Mwaka huu kazi ipo na si ndogo...
   
 14. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Tsh nadhani haiko pegged, ni floating currency. So inabadilika na market conditions.
   
Loading...