EWURA waridhia kupandisha bei mafuta, bei mpya hizi hapa!

Status
Not open for further replies.
Ningepata hii news mapema ningejaza full tank kabisa.. Hawa watu wa Ewura ndio wanaotuchanganya serikali imewasakizia wenyewe wametulia fresh na bajeti kubwa mno kwani watazitia ndimu tu hawawajawahi kuacha iba hata mwaka mmoja. 2015 watazitema hizi mambo ya sheria ya kulindana ili watuibie hatutaikubali tutawatia vitanzi hadharani
 
jamani kwa staili hii ya watu wazima kufanywa kama machizi!naenda zangu afganistani potelea mbali.
 
Poleni sana watz. Wahenga walisema Amani haipatikani ila kwa ncha ya......
 
"Zimebaki story" tutafanyasiasa zisizokuwa na tija mifano ipo lakini waTZ Tumelala. Jamani, hivi tutaamka lini?
 
Nasubiri kwa hamu 2015... hivi tuje tuwafanye nini wale wanaodanganyika kwa kupewa kanga>..??? alafu wanachagua ccm tena?! hawa ndio wasiliti wa nchi
 
Hivi wakuu kuna anayekumbuka zile bei kabla ya kushusha?tukizipata hizo ndio hao wanaojiita EWURA tutaujua usanii wao!kama kuna mwenye bei hebu azitundike hapa!walitusumbua bure!!!!!!!kumbe wana lao jambo!leo nimepita petrol station alfajiri hakuna muuzaji!wanasubiri wabadilishaj wa pump price wafike!wizi mtupu!
 
Nilishajua tu bei itarudi palepale tena na zaidi!

Hivi visingizio vya shilingi kushuka thamani kwani vimeanza leo? Mbona hata kabla ya bei elekezi ya majuma mawili yaliyopita!na sasa tusubiri kwa bei kupaa zaidi kwani hatuna dalili ya kushusha thamani ya dola!

Kulikuwa na haja gani ya kupandisha bei kwa haraka kiasi hicho na kutusababishia usumbufu kiasi hichi,watu wametembea kwa miguu kisa hakuna mafuta!na hawa wenye mafuta tuone kama watauza kwa bei ya 2004 au 2104 hii mpya kwasababu bakaa waliyonayo ni ile ya bei ya mwanzo kabla ya kupanda kwa mafuta.

Wizi mtupu
 
Ninyi mnamuweka mrundi kuwaongozea taasisi muhimu kama EWURA tunategemea nini?
 
[h=3]TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI ELEKEZI/KIKOMO ZA MAFUTA AINA YA PETROLI KUANZIA TAREHE 15 AGOSTI 2011[/h]

Kama ilivyo ada, na kulingana na Kanuni ya Kukokotoa bei za
bidhaa za mafuta ya petroli bei zimekuwa zikikokotolewa na kutangazwa na
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kila baada ya wiki mbili.
EWURA inatangaza bei elekezi/kikomo za mafuta ya petroli nchini zitakazoanza kutumika
kuanzia Jumatatu, Tarehe 15 Agosti 2011. Bei hizi zimekokotolewa kwa kuzingatia kanuni mpya
iliyoanza kutumika mwanzoni mwa mwezi huu. Pamoja na kutambua bei elekezi/kikomo za bidhaa
mbalimbali za petroli nchi nzima, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:


(a) Bei za jumla na rejareja kwa aina zote za mafuta zimepanda ikilinganishwa na bei zilizokokotolewa kwa ajili ya kuanza kutumika tarehe 1 Agosti 2011 ambazo zilitangazwa tarehe 3 Agosti 2011. Katika toleo hili bei zimepanda kama ifuatavyo: Petroli TZS 100.34 sawa na asilimia 5.51, Dizeli TZS 120.47, sawa na asilimia 6.30 na Mafuta ya taa TZS 100.87, sawa na asilimia 5.30. Mabadiliko haya ya bei za mafuta nchini yametokana na kupanda sana kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuendelea kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na dola ya Marekani (sarafu ambayo hutumika katika manunuzi ya bidhaa za mafuta kwenye soko la dunia).

Kwa mfano, kwa viwango vya bei zilizotumika katika chapisho hili, bei katika soko la dunia zimepanda kwa wastani wa asilimia 5.42 na thamani ya shillingi ya Tanzania imeshuka kwa shilingi 47.12 (asilimia 2.96) kwa dola moja ya Marekani. Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepanda kama ifuatavyo: Petroli TZS 110.34 sawa na asilimia 5.70; Dizeli TZS 120.47 sawa na asilimia 6.54; na Mafuta ya Taa TZS 100.87 sawa na asilimia 5.49.


(b) Bei za rejareja na za jumla zingepanda zaidi endapo formula ya zamani ingeendelea kutumika. Kwa kulinganisha vigezo vilivyo katika fomula ya zamani na fomula mpya, bei za mafuta zingekuwa kama ifuatavyo:

Aina ya Mafuta
Bei za Rejareja (TZS/L)
Bei za Jumla (TZS/L)
Kwa Formula ya zamani
Kwa Formula Mpya
Kwa Formula ya zamani
Kwa Formula Mpya
Petroli
2,298.33
2,114.12
2,230.07
2,046.62
Dizeli
2,213.36
2,031.31
2,140.80
1,963.81
Mafuta ya Taa
2,188.89
2,005.40
2,116.33
1,937.90

Kama inavyoonyesha kwenye jedwali hapo juu, formula mpya inaendelea kutoa unafuu kwa watumiaji ukilinganishwa na kama fomula ya zamani ingetumika. Ni dhahiri kuwa vigezo viwili vikubwa vinavyochochea kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta nchini ni kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ukilinganisha na dola ya Marekani, sarafu ambayo inatumika kuagizia mafuta hayo.



(c) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.



(d) Kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei kikomo (price cap) kama ilivyokokotolewa na fomula iliyopitishwa na EWURA na ambayo ilichapwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 5 la tarehe 9 Januari 2009 na marekebisho yaliyofanywa mwezi Julai 2011.



(e) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika.



(f) Wanunuzi wanashauriwa kuhakikisha kuwa wanapata stakabadhi ya malipo inayoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hiyo ya malipo itatumika kama kidhibiti cha mnunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo; ama endapo utakuwa umeuziwa mafuta yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

A: BEI ZA REJAREJA

Bei Elekezi
Mji
Petroli
Mafuta ya Taa
Dizeli
(TZS/LT)
(TZS/LT)
(TZS/LT)
Dar es Salaam
2,114
2,005
2031
Arusha
2,198
2,089
2115
Arumeru
2,198
2,089
2115
Karatu
2,216
2,108
2133
Monduli
2,203
2,095
2121
Ngorongoro (Loliondo)
2,275
2,166
2192
Kibaha
2,119
2,010
2036
Bagamoyo
2,125
2,016
2042
Kisarawe
2,121
2,013
2038
Mkuranga
2,124
2,015
2041
Rufiji
2,142
2,033
2059
Dodoma
2,173
2,064
2090
Kondoa
2,205
2,096
2122
Kongwa
2,170
2,061
2087
Mpwapwa
2,174
2,065
2091
Iringa
2,178
2,069
2095
Kilolo
2,183
2,074
2100
Ludewa
2,244
2,135
2161
Makete
2,237
2,128
2154
Mufindi
2,188
2,079
2105
Njombe
2,206
2,098
2124
Bukoba
2,329
2,220
2246
Biharamulo
2,303
2,194
2220
Karagwe
2,345
2,236
2262
Muleba
2,320
2,211
 
Naungana na didas masaburi kwa ule useme wake.
mkuu hata ukisema hivyo hapa jamaa wametupiga changa la macho wamerudisha bei ya zamani halafu wakawa wanasema kila baada ya wiki 2 bei ina badilika kwa baada ya leo bei itakuwa petroli ni 2300 na dizeli ni 2204 na mafuta ya taa ni 2196 kwa dar tu..
 
mkuu huyu mleta maada ninavyoona ni kam vile anafikiria kwa kutumia masaburi. Yaani haelewi ila anakurupuka tu, sijui kalewa mbege? Aggghhhh!!! nashindwa hata kumjaji.
hivi mmemuelewa mtoa mada? au unabisha bisha, Ewura wali2mia formula iliyokuwa ikitumika hapo zamani kabla ya mgomo, na hiyo ni baada ya kugundua kuwa formula mpya imekosewa kitaalamu,.
 
mkuu hata ukisema hivyo hapa jamaa wametupiga changa la macho wamerudisha bei ya zamani halafu wakawa wanasema kila baada ya wiki 2 bei ina badilika kwa baada ya leo bei itakuwa petroli ni 2300 na dizeli ni 2204 na mafuta ya taa ni 2196 kwa dar tu..

tutafanyaje sasa.......asubuhi hii nimeona bei ni 2198 kwa petrol.......kama vipi wafanye 2500 kabisa ili tujue moja
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom