EWURA wafuatilieni wasambazaji wa gesi za kupikia

Usikubali huduma ya kuletewa gas nyumnani kanunue kituo cha mauzo upime kwenye mzani hapohapo ikipungua usichue kwa mfano mtungi wa kg15 ukiwa tupu ,ukijazwa gas mzani unatakiwa usome 30kg
Soma kichwa cha habari shida sio kwanmuuzaji msambazaji ambae hata muuzajinmwenye mzani nae ananunua kwake ukweli jamaa wa MBEZI STOP OVER AITWAE STEVEN AMEHARIBU SNA BIASHARA MBAYA BAADA YA KUKAMATWA SASA ANATUMIA MADEREVA WANAOTOKA VITUO HALALI KAMA KAWE ..SINZA ..NA PALE KINONDONI WAKISHIRIKIANA NA WALE WA MBEZI

KINACHOFANYIKA BAADA YA MADEREVA KUUZA GESI WALIZOTOA DEPO EG SINZA WANAKWENDA KWA HUYU BWANA AMBAE ANA MAGODOWN YANAYOJULIKANA NA POLISI WA MBEZI PIA..

KINACHOFANYIKA WANAJAZA WANAENDELEA KUSAMBAZA KWA WATEJA WAO..WEWEE UTAJUA ZIMETOKA SINZA AMA KAWE AMA KINONDNI VITUO VINAVYOJULIKANA RASMI

SHIDA SIO MUUZAJI MSAMBAZAJI NA HIVI SAS
 
EWURA wako wapi?

Mbona EWURA wako fast kukata % kwenye umeme wa LUKU tu, ila kazi yao haionekani?

Hivi huku EWURA hawasomi maoni ya watu?

Bidhaa mbovu za gesi halafu wapo tu wanakula bata
 
Nilikuwa mteja wa Oryx nikahama baada ya kukutana na sintofahamu matumizi yangu ni fixed nikashangaa gesi imeisha ndani ya robo ya siku ninazozitumia kwa kazi yangu nikagundua kuwa kuna uhuni unafanyika na swala la kupima uzito vituo vingine havina mizani na wanadai wanaletewa mitungi ikiwa sealed.
 
Gesi za kupikia za akina Manjis na Oryx zimechakachuliwa

Gesi wamezidisha liquid na zinaharibu majiko
Kawaida gas ya kupikia ya LPG hukaa kwenye mtungi ktk hali ya kimiminika yaani liquid form na pale unaporuhusu kutoka ndani ya mtungi kupitia ole koki au kwa kizungu regulator kile kimiminjka hubadilika na kuwa gas ambayo hupita kwenye mpira hadi ndani ya jiko lako.Majiko mengi ya gas hasa yale ya mezani watu wengi wanashindwa ku set moto na badala yake kuanza kutoa moto wa njano ambao unatoa moshi.Majiko aina ya Nikai ndio hasa inabidi kuwa nayo makini sana wakati wa kurekebisha moto na ukishindwa basi itatoa moshi mwingi na wewe kudhani ni gas.Wauzaji wote wa hayo majiko watakufumdisha jinsi ya kuset moto ili usipate moshi wakati wa kupika,mtu usidanganyike kabisa kuwa gas inaweza kuongezwa kitu kingine.
 
ndo ushenzi wa wafanya biashara huo na walishaona EWURA hawakogi busy na gas za majumbani hata bei wanajipangiaga tu
 
pia ni ngumu kujua uzito kama ni sahihi,nadhani uwekwe utaratibu wa kumlinda mlaji kwa kuweka mfumo au kifaa cha kupima ujazo,sasa hilo limtungi la chuma,mteja haoni ndani kama liko nusu au robo au robo tatu


Maduka yote ya gesi huwa yana mizani, ukinunua unawaambia wanakupimia. Pia mitungi yote huwa ina seal, kama haipo usinunue. Na wanatakiwa wakupe risiti yaEFD ya TRA
 
Ewura liangalieni hili mnatupa shida sisi wa vipato.vya kubahatisha.
 
Back
Top Bottom