EWURA, Vipimo na SUMATRA walifika siku moja kabla ya Waziri Mkuu

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Imefahamika kabla kuwa viongozi wa EWURA,Vipimo na SUMATRA walifika siku moja kandari ya Dar es Salaam na kuweka azimio la kuwasha mita ili kumpiga changa la macho Waziri Mkuu kuwa Flor Meter zinafanya kazi.

Na hii ilisaidiwa na wafanyabiashara wenye mtandao kuwa waziri mkuu asingeweza kujua Flow Meter ziliwashwa lini, lakini tofauti na matarajio waziri aling'amua ingawa sio mtaalam wa mafuta na Flow meter.
 
Kuna mkuu mmoja humu ndani jina lake ni "kikulachochako"..... kimsingi kuna mchwa wanakula ila mbele ya Raisi na waziri mkuu ni watakatifu...... movie ndo imeanza....
 
HAWA EWURA,VIPIMO NADHANI NI MAJIPU BY 100% KWANINI WALIDHAMIRIA KUMPIGA CHANGA LA MACHO W/ MKUU?.
**ILI IWAJE?
**WAFICHE NINI?
**ILI KUMSAIDIA NANI?
**NI NANI YUPO NYUMA YAO?
HALELUJAH.
 
Aliyevujisha siri ya ziara ya waziri mkuu..ni hao hao anaowatumia kujua kinachoendelea huko..bongo ngumu sana..watu tunafurahia uozo na ujinga wetu.
 
ndani ya serekali ya magufuli Kuna baadhi ya mawaziri ni wasaliti na mchwa wanaoshirikiana kundi kubwa la wahujumu uchumi. Nina wasi wasi uadilifu wa muhongo,mwakembe,marope na waziri wa uchukuzi wa sasa mmoja wao anaweza kuwa msaliti na anaeshirikiana na wahujumu uchumi. Ndio maana tunasema ccm ni tatizo kwa ustawi wa Tanzania. Na sidhani kama magufuli atawaweza hawa wanakinga nzito Sana kwenye chama.
 
Sasa hapa ndio tutapata Link ya Muhongo na huyo Mama aliyemtumia SMS ,kumbe kuna watu zaidi ya Muhongo walijua PM ataenda Kukagua hapo bandari ??
 
IMEFAHAMIKA KABLA KUWA VIONGOZI WA EWURA , VIPIMO NA SUMTRA WALIFIKA SIKU MOJA BANDARI YA DAR ES SALAAM. NA KUWEKA AZIMIO LA KUWASHA MITA ILI KUMPIGA CHANGA LA MACHO WAZIRI MKUU- KUWA FLOW METER ZINAFANYA KAZI.

NA HII ILISAIDIWA NA WAFANYABIASHARA WENYE MTANDAO KUWA; WAZIRI MKUU ASINGEWEZA JUA FLOW METER ZILIWASHWA LINI; LAKINI TOFAUTI NA MATARAJIO WAZIRI ALING'AMUA INGAWAA SIO MTAALAM WA MAFUTA NA FLOW METER

Si suala la kung'amua baada ya kufika pale, bali alishakua na full information ya kwamba flow metres hazifanyi kazi na ana data zote kuhusu kilichopo bandarini.

Kilichomshangaza na kumshitua ni kukuta kuna metre zinatembea akajua kuna jambo limefanyika na katika kuuliza maswali, mama akajichanganya na kukuta inambidi aseme ukweli kua ngazi za juu zimemtext ahakikishe metre zinatembea. Hapo mambo ndipo yalipowaharibikia.

Inawezekana angekuta zimesimama na kupewa maelezo kua ni mbovu, angetoa amri kali ya kuhakikisha metre zote zinafanyiwa marekebisho na kutembea. Sasa tatizo kama hazikua mbovu maana huenda hata hilo analo in advance maana tumeona baadhi ya correspondences kutoka TPA kwenda TRA zinazoomba ruhusa ya kubypass flow metres. Tuiachie serikali ifanye kazi yake, mwisho wake tutauona tu.
 
HAWA EWURA,VIPIMO NADHANI NI MAJIPU BY 100% KWANINI WALIDHAMIRIA KUMPIGA CHANGA LA MACHO W/ MKUU?.
ILI IWAJE?
WAFICHE NINI?
ILI KUMSAIDIA NANI?
NI NANI YUPO NYUMA YAO?
HALELUJAH.
Ndio maana tunasema kazi ya kuyatunbua majipu inaikwazo vingi sana
 
Waliosema kikulacho kinguoni mwako hawakukosea. ..

Hapa walio karibu na Uongozi mkuu ndio wanaotoa taarifa ili kuficha madhambi yao...Magufuli na Team yake wana kazi mno. Ila mafanikio yatatokea wakiwa na uvumimilivu.
 
Hapa kumeonekana udhaifu mkubwa Toka TPA,VIPIMO,EWURA NA TRA. Watumishi wote wenye.portfolio za kuwajibika wawajibishwe na kama MH. JPM alivyosema kwemye sherehe za mahakama juzijuzi. Takukuru wasipoteze muda kwa semian elekezi za kufundishana kutafuta ushahidi. Ushahidi hapo ni wajibu ama job descriptions za wahusika wote. Wamekwenda kinyume na.mikataba.yao ya ajira. Hatua stahiki zifuatwe. #HAPAKAZITU
 
Back
Top Bottom