EWURA: Tunaomba tuvumiliane muda huu, hali halisi kwenye soko la dunia ni ngumu sana

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Leo Ewura, pamoja na mambo mengine wamezungumzia kupanda kwa bei za gesi ya kwenye mitungi zinazotumika zaidi majumbani pia wamezungumzia mradi wao wa gesi asilia zinazosambazwa majumbani(CNG) kwenye kipindi cha 'Morning Trumphet' kinachorushwa na kituo cha Azam TV.

Mtangazaji: Baada ya kusitisha bei za kupanda gesi, mmetuambia kama watawasilisha hoja zenye mashiko huenda zikarejea. Mchakato wa mazungumzo umeshaanza na maamuzi yatatoka lini?

Titus Kaguo(Mawasialiano, Ewura): Ambacho tumewaambia walete hizo hoja mapema ili tufanye review tuone tunaendaje. Tofauti na LPG, natural gas tunaipangia bei.

LPG haijaanza kuja kwa mfumo wa pamoja(Bulk system) pia storage facility bado ni ndogo hivyo tukaacha waendelee kupanga wao ili kulihamasiha na soko. Ewura ana-monitor kuona bei inaenda kama inavyotakiwa.

Wakileta mapema justification zao, zitajadiliwa mapema na zitatoka mapema kwasababu hatuko hapa kuwakamata watu ili wasiendelee na biashara

GESI-MAGARI
Titus: Ili kuendana na upandaji wa bei ya mafuta, EWURA imeshaanza kutoa leseni kwa watu wanaotaka kujenga vituo vya gesi asili kwenye magari. Tumeanza kupokea kwahivyo tunahamasisha watu walete maombi wengi.

Kutoa Dar mpaka Dodoma unaweza kutumia 50,000 au 60,000. Tukiwa na vituo vingi vya gesi na gesi tunayo inaweza kutusaidia kuachana na hii hali ya kutegemea soko la dunia tunavyofanya kazi.

BEI ZA MAFUTA NA GESI MAJUMBANI
Titus Kaguo:
EWURA ipo na ilianzishwa ili isaidie watanzania, bei za mafuta zilizopo ni hali halisi iliyopo duniani lakini tunachohakikisha ni kuhakikisha haiongezeki hata senti katika bei halisi ambayo inakuwa imetolewa.

Pia ni Ewura huyuhuyu, kuna wakati bei zilishuka mpaka wakashangilia. Tunachofanya, pale bei zinaposhuka tunawaletea kwamba bei zimeshuka, zinapopanda tutawaambia bei zimepanda. Tunaomba tuvumiliane muda huu, hali halisi kwenye soko la dunia ni ngumu sana

GESI ASILIA MAJUMBANI
Mita zetu za gesi ni pre-paid kama TANESCO, unaweza kununua hata gesi ya 2,000 kwa ajili ya matumizi, gesi yetu ni rahisi sana kuanzia 1,000. Gesi ya magari inauzwa 1,550 kwa kilo moja na matumizi yake ni mara moja na nusu ya lita moja ya petroli. Kwasasa tuna wateja wengi sana wa uber
 
Nyinyi Ewura toka Magufuli amefariki mnatoa vibali vya ujenzi wa Petrol station mtaa mmoja hata sheli tano kweli huu ni uchafuzi wa mazingira hebu tumbueni aliyepo anayetoa vibali vya sheli maana mnatuharibia mji sasa.

Mfano halisi kuna barabara ya Africana mbezibeach mpaka kawe roundabout kuna kibali mmetoa pale karibu na juliana eneo linalomilikiwa na Mama rwakatare, pale Shabaha long range ya jeshi tayari kuna sheli inaitwa Darpco, mbele karibu na shule ya msingi mbezibeach kuna sheli ya oryx, mbele rainbow kuna oilcom na GBP hivi huu si uchafuzi wa mazingira hata kama ni njaa ya pesa ya vibali kweli mtaa mmoja una sheli zaidi ya nne. Na njia ya tegeta kwenda bunju ndio kuna utitiri wa sheli hivi huwa hamuendi hata kenya mkaona mfano.

Sheli sio vitu vya kujazwa hovyohovyo mtaa mmoja.
 
Tangu JPM aondoke EWURA wameachana na mlaji wa mwisho (Final Consumer) a.k.a Mnyonge.

Wao sasa wanapangiana bei na matajiri tu. Kila siku vitu vinapanda bei.
 
Angalieni na uchumi wa nchi yetu hata MTU mmoja mnatakiwa mpambane kushusha bei ninyi mnapandisha au tuhame hii Tanzania
 
Blabla tu ,wao waseme tu tumeamua kuwakamua hohehahe ili wazinduke ,waache kushangilia hovyo chama
 
Back
Top Bottom