EWURA: Tanzania ni kati ya nchi zenye bei ndogo ya Mafuta

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,355
8,042
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Mhandisi Modeatus Lumato amesema Tanzania ni kati ya nchi zinazouza mafuta kwa bei ya chini kutokana na ruzuku ya Serikali.

Amesema mbali na ruzuku hiyo, hatua ya kuwa wananunua mafuta kwa pamoja imesababisha kushuka kwa bei licha ya kuwepo kwa changamoto zilizosababisha kupanda kwa nishati hiyo kama baa la UVIKO 19 lililoitikisa dunia.

Akizunguka katika Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ewura, Mhandisi Lumato amesema Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi zenye bei ndogo ya mafuta ikilinganishwa na nyingine hasa za Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kulinga na bei ya mafuta ya rejareja ya dizeli iliyotangazwa siku nane zilizopita kwa Dar es Salaam na Tanga kwa Novemba 2022, imepungua kwa Sh31 na Sh34 kwa lita ikilinganishwa na bei hizo kwa mwezi Oktoba mwaka huu.

Pia bei ya rejareja ya mafuta ya petroli kwa Bandari ya Dar es Salaam ingeongezeka kwa Sh110 kwa lita, hata hivyo, Serikali imetoa ruzuku ili bei iliyopo ya Oktoba 2022 isibadilike. “Ruzuku ya Serikali imesababisha kupungua kwa bei hii ndio maana bei yetu ni ndogo ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika,” amesema Lumato.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego alilikumbusha baraza hilo wajibu wake wa kushughulikia maslahi ya wafanyakazi kwa wakati ili kuondoa malalamiko yanayoweza kujitokeza sehemu za kazi. Amesema afya na maendeleo ya wafanyakazi nje na ndani ya eneo la kazi ni wajibu wa viongozi kufuatilia ili kuongeza ufanisi.

“Mfanyakazi akikabiliwa na ukatili wa kijinsia kwa kupigwa na mume au mkewe atafanya kazi vizuri? Si ataathirika? Au akiwa mlevi anatukana na kuzungumza hovyo anapoenda baa, ofisi haiathiriki? Shughulikieni maslahi ya wafanyakazi,” amesema Dendego.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom