EWURA: Taarifa lini mnatoa kutokana na maombi ya TANESCO

Ngambako

JF-Expert Member
Dec 27, 2013
315
263
Wanajamvi habari ya mchana

Ikumbukwe kuwa tarehe 27/2/2016 Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) lilipeeleka maombi ya kushushwa kwa gharama za umeme kwa walaji (watumiaji) ikihusisha pia kuondolewa kwa tozo ya kila mwezi ijulikanayo kama (service Charge) ambayo ni zaidi ya Tsh 5200 na wakaiomba EWURA ishushe gharama za umeme kwa asilimia 1.

Kulingana na sheria iliyotungwa na Bunge la JMT, Ewura inatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21 mara baada ya ombi kuwasilishwa; kwa maana hiyo ni kuwa mpaka leo hii tarehe 30/3/2016 zimetimia takribani siku 32 toka ombi hilo kuwasilishwa na Tanesco kwenu.

Mimi kama mlaji wa huduma itolewayo na Tanesco; naomba kufahamishwa ni lini EWURA mtatoa taarifa rasmi juu ya kuondolewa kwa tozo na kushushwa kwa gharama za kununua umeme?
 
Ewura huwa wana spidi kali kutangaza bei kupanda lakini bei kushuka wanakuwa wazito sana sijui kwa nini.
 
Ivi maandamano ya kushawisha ewura watoe tamko ya punguzo ilo yanaruusiwa ua yale magari bado yapo na ubora wake naomba wananchi tufanye maandamano kwa taifa kukumbusha jambo ili muhimu kwa serikali ni kitaifa maana duh kesho mwisho naanza kujipanga service charge inakera kwa mi ninaeunga senti
 
Watanzania hawanaga mpango huo, ingekua South Africa sawa, sisi tulisharogwa....
 
Haya basi wanajamii forum wafunge thread zote tuanze kuandaman kwenye hii app ili kupata sapoti team kubwa wote 2imbe wimbo mmoja wa punguzo
 
Hii ndo Tanzania nchi yangu,,,, miss tanzania by Tholo thang ni wimbo mzuri sana
 
Nimenotice katika token niliyonunulia umeme juzi kwamba service charges zimeondolewa.Sio siri kwamba huu ulikuwa wizi wa wazi.Sijui nani alifaidika na wizi huu, ni vema ikachunguzwa.

Nimalizie kwa kusema kwamba EWURA ni dili la kupiga hela tu,hatuihitaji kabisa.Wanatuongzea tu bei ya umeme,it should go.Kinachotakiwa ni ku-improve management system ya TANESCO tu.
Wanajamvi habari ya mchana

Ikumbukwe kuwa tarehe 27/2/2016 Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) lilipeeleka maombi ya kushushwa kwa gharama za umeme kwa walaji (watumiaji) ikihusisha pia kuondolewa kwa tozo ya kila mwezi ijulikanayo kama (service Charge) ambayo ni zaidi ya Tsh 5200 na wakaiomba EWURA ishushe gharama za umeme kwa asilimia 1.

Kulingana na sheria iliyotungwa na Bunge la JMT, Ewura inatakiwa kutoa taarifa baada ya siku 21 mara baada ya ombi kuwasilishwa; kwa maana hiyo ni kuwa mpaka leo hii tarehe 30/3/2016 zimetimia takribani siku 32 toka ombi hilo kuwasilishwa na Tanesco kwenu.

Mimi kama mlaji wa huduma itolewayo na Tanesco; naomba kufahamishwa ni lini EWURA mtatoa taarifa rasmi juu ya kuondolewa kwa tozo na kushushwa kwa gharama za kununua umeme?
 
Nimenotice katika token niliyonunulia umeme juzi kwamba service charges zimeondolewa.Sio siri kwamba huu ulikuwa wizi wa wazi.Sijui nani alifaidika na wizi huu, ni vema ikachunguzwa.

Nimalizie kwa kusema kwamba EWURA ni dili la kupiga hela tu,hatuihitaji kabisa.Wanatuongzea tu bei ya umeme,it should go.Kinachotakiwa ni ku-improve management system ya TANESCO tu.

Bro are you serious kwamba wametoa hilo litozo lao?
 
Ewura ni moja ya jipu la kutumbuliwa .aifanyikazi ipasavyo .ewura ilitakiwa iwe ya kwanza kuitaka TANESCO ipunguze bei .na sio tanesco au Waziri kama ilivyotokea.hii tuu peke yake inaonyesha ewura ni jipu.ondolea mbali kosa la kukaa na maombi zaidi ya siku 24 za kisheria bila kutoa jibu..ewura ni jipu
 
Back
Top Bottom