EWURA, SUMATRA na wamiliki wa vyombo vya Usafiri hii inawahusu

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,744
21,189
Amani kwako.
Maisha ni gurudumu ambalo lazima likanyage mzunguko wote ili kufikia hatua inayotakiwa.

Mfanyabiashara yeyote hana undugu na mteja hii inatokana na mfumo wa biashara kama kuepuka hasara na mambo mengine.

MADA:
Bei ya mafuta imeshuka maradufu na ndani ya wiki tatu imeshuka tena, hii ni furaha kwa mfanyabiashara yeyote anayetegemea biadhaa ya mafuta ilo kuendesha biashara yake.

Katika hatua mojawapo ambayo tunaishuhudia kila leo ni ile ya kutangazwa kupanda bei ya mafuta alafu kesho yake wadau wa usafirishaji wanatoa tamko la kupandisha nauli kisa mafuta kupanda bei.

Leo tunashuhudia mafuta yaliyokuwa yakiuzwa bei mpaka 2750/= kushuka kwa kiasi kikubwa na hakuna mfanyabiashra anayetaka kutoa tamko la kushusha labda nauli au bidhaa.

Wasimamizi niliowataja pale juu wa sekta hii mnaona, mnasikia na mnatafakari ila hatujui mlilo nalo huko maofisini kwenu.

Mwananchi anaona, anasikia na ANAJUA kila kinachoendelea ila kukaa kimya siyo sababu kuwa hana uwezo wa kudai haki yake, pamoja na kujua kuna chama cha kutetea haki za watumiaji au wasafiri hila hawa wapo kwa faida zao siyo za mwananchi.

EWURA, SUMATRA Chukueni hatua ili Mwananchi ajue hadha ya corona kwenye soko la mafuta duniani imeleta neema, hafueni na upande mwingine majanga pia.

Nawasilisha.
 
Jbu la wafanyabiashara wa vyombo vya moto ni hili 'mafuta yameshuka bei ni kweli lkn Oil&Spare parts zimepanda sana sababu ya Corona'
 
Back
Top Bottom