Ewura ni mzigo kwa taifa!!!iko kwa faida ya wakubwa na wafanyabiashara wa mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ewura ni mzigo kwa taifa!!!iko kwa faida ya wakubwa na wafanyabiashara wa mafuta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jul 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,449
  Likes Received: 5,700
  Trophy Points: 280
  EWURA naona mamlaka hiyo imeshindwa kazi na sasa utendaji wake hauna tofauti na wafanyabiashara wengine wa mafuta. Kwa ujumla EWURA ni mzigo kwa Taifa na ninaamini mamlaka hii iko kwa faida ya wakubwa wachache na namna wanavyofanya kazi na kukusanya mapato yao ni mzigo kwa raia wa kawaida kwani imekuwa ikiongeza bei kwa bidhaa na huduma zote ambazo ziko kwenye mamlaka yao (umeme, maji, mafuta ...)

  PUMBAFUW WATUPU WAMEKALIA KUSUBIRI SAFARI NA PER DIEM .....WAKIDANGANYANA NA MAKATIBU WA WIZARA HUSIKA AMBAO HUWAJUMUISHA KWENYE SAFARI ZAO...SHAME KIKWETE
   
 2. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Naungana mkono na wewe katika hili, EWURA wangetaka kufanya kazi ni muhimu sana kwa taifa, lakini inaonekana wameshashikwa mikono na makampuni ya mafuta. Juzi kulikuwa na mjadala wa kuwa ili kuweza ku control bei za mafuta na kuwa na uhakika wa hifadhi ya mafuta ni lazima TPDC awezeshwe ili aingize mafuta na kuwauzia hao makampuni at least 50% na remaining 50% inaweza kuingizwa na yeyote. Utafiti umeshafanyika nchi zote Duniani hakuna iliyoachia swala la mafuta kwa private companies. Nchi zote ikiwemo hata Kenya tunayoiona kama nchi ya kibepari inaagiza mafuta kwa bulk through nationa oil company NOK about 60%.

  Baada ya utafiti na report kukamilika serikali ikatangaza through Ngereja kwamba mwaka huu inaanza hilo zoezi. Makampuni ya mafuta kupitia chama chao wakaanza kupinga kwa nguvu zote!! wanasema serikali itapata hasara!!! Ewura baada ya kupewa millions of money zilizochangwa na hayo makampuni wamekubaliana na hayo makampuni ili yaendelee kuwanyonya wananchi!!!. Hivi sasa bei ya mafuta imeshapanda zaidi ya 40% wakati mafuta duniani yamepanda kwa 15% only kwa miezi miwili iliyopita!!?

  Habari za ndani sana zinasema wenye makampuni ya mafuta wamechanga karibu Mil.500 tshs kuhakikisha Wizara ya Nishati na Ewura wanakwamisha huo mpango, na wamefanikiwa hadi jana kwani haijawekwa kwenye budget.

  Lakini je, tutafika kwa kuwa na viongozi wa aina hizo? wasio na uchungu na nchi????
   
Loading...