Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,260
Tanesco wamepeleka maombi Ewura ya kutaka kufuta makato ya5520 ya huduma au service charge ambayo hutozwa kila mwezi mteja anaponunua umeme. Vile vile wanataka kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1 na wameshafikisha maombi yao Ewura. Sasa cha ajabu mamlaka hii ambayo haichelewi kupandisha bei ya mafuta yanapopanda inaburuza miguu kutoa ruhusa kwa Tanesco kushusha bei ya umeme. Sioni kuna haja gani ya kuchelewesha kutoa ruhusa kwa Tanesco kupunguza bei na kuondoa tozo ya huduma ya kila mwezi. Ewura achani kuvuta vuta miguu wananchi tunaumia. Na mwisho wa siku tunataka na makato ya Ewura kwenye bill nayo yakome kwani mamlaka hiyo inahudumiwa na serikali chini ya wizara hakuna haja kutesa wananchi kwa kulipia uendeshaji wa ewura. Tozo pekee inayotakiwa kubaki ni VAT tu nayo pia ishushwe watu tupikie umeme mkaa una maliza misitu!