Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,806
- 11,968
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji hapa nchini EWURA imesema imebaini baadhi ya mamlaka za maji kukiuka sheria zinazosimamia mamlaka hizo katika kutoa huduma kwa wananchi ikiwamo kutoza bei ambazo hazijapitishwa na EWURA na ubambikiziwaji wa bili za maji.
Hayo yamebainishwa leo Mei 8,2021 jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Mhandisi Godfrey Chibulunje wakati akizungumza na wanahabari amesema baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wateja waliamua kufanya ukaguzi katika mamlaka 24 kati ya 94 zilizopo.