EWURA inaweza kubana madereva yasema Tatoa


Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Messages
169,612
Likes
620,017
Points
280
Rutashubanyuma

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined Sep 24, 2010
169,612 620,017 280
Wednesday, 01 December 2010
Mwandishi Wetu

CHAMA cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa), kimesema Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), ina uwezo wa kuwabana madereva wa malori yanayosafirisha mafuta, kwa kuwajumuisha katika sheria za usafirishaji wa bidhaa hiyo.

Kwa mujibu Tatoa, kipengele cha 414, sehemu 6(c) ya sheria hiyo, inabainisha kuwa majukumu ya mamlaka hiyo ni pamoja na kulinda matumizi na ubora wa malighafi za mafuta na kwamba madereva wanahusika kwa sababu ndio wanaosafirisha mafuta.

Ilisema kanuni namba 30 pia inawapa Ewura, mamlaka ya kuchagua taasisi ya kutoa mafunzo maalumu kwa madereva wanaosafirisha bidhaa mbalimbali za mafuta.

"Kwa hiyo Tatoa inapendekeza Ewura ifanye marekebisho kwa kuwaingiza madereva," alisema sehemu ya taarifa ya Tatoa.

Sheria na kanuni za usafirishaji mafuta zilizotangazwa na Ewura hivi karibuni, zimekuwa zikiwataja madereva na kuwaonyesha kuwa ni wadau katika biashara hiyo, lakini zimeshindwa kuwajumuisha katika adhabu pale inapobainika kuwa wamebeba mafuta yaliyochakachuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Tatoa iliyosainiwa na Katibu Mkuu, Zacharia Poppe, kwenda Ewura, ikiwa ni mapendekezo rasmi, madereva wa malori wanapaswa kujumuishwa katika sheria ya usafirishaji wa mafuta, ili kukabiliana na tatizo la uchakachuaji.

Lakini wakati Tatoa ikitoa mapendekeza na ya kutaka kodi ya mafuta ya taa ipandishwe, Ewura kwa upande wake inataka upande huo uwajibike kwa madereva hao kwani na kwamba mamlaka hiyo, haiwajibiki moja kwa moja na madereva hao.

Inashangaza kuona sheria hiyo inawaweka pembeni madereva wanaohusika kubeba mafuta hayo hali inayowapa nafasi kubwa ya kufanya uhalifu.
 

Forum statistics

Threads 1,235,142
Members 474,353
Posts 29,213,169