EWURA: Hifadhi ya Petrol ya iliyopo Tanzania ni ya siku 27, jiandaeni kwa bei mpya Jumanne Aprili 5, 2022

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Watanzania wametakiwa kukubaliana na hali halisi kuhusu bei mpya ya nishati ya mafuta ikiwemo Petrol, Diesel, Mafuta ya Taa na Ndege ambayo itatangazwa Jumanne ijayo Aprili 5, 2022

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta si Tanzania pekee bali kote duniani kuna changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa nishati hiyo sababu ya vita ya Urusi na Ukraine.

Akizungumza katika mdahalo wa mafuta jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, Aprili 2, 2022 amesema hadi kufikia leo, nchi ilikuwa na hifadhi ya mafuta ya Petrol ya siku 27.

"Sheria inatutaka tuwe na hifadhi ya mafuta ya kuanzia siku 15. Ina maana hatuko katika hatari japo tunapaswa kuongeza uwezo wetu wa kuhifadhi zaidi," – alisema.

Mhandisi Chibulunje alisema kwa upande wa mafuta ya dizeli yapo ya kutosheleza siku 19, ya taa siku 108 na ya ndege yapo ya siku 35.

Mhandisi Chibulunje alisema kuwa matumizi ya mafuta kwa sasae ni mwezi mmoja na tayari mengine yameshaagizwa huku meli nyingine zikishusha shehena yake.

Aidha, amesema Aprili 24, 2022, kuna meli zitaingiza mafuta nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na nyingine ikitarajiwa kuingizwa nchini mwezi ujao kupitia Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa wote PBPA.

Mhandisi Chibulunje alisema kwa sasa Tanzania ina maghala makubwa matatu yenye uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa siku 122 katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Chanzo: TEF
 
... naona wote wanapita mulemule kwenye kauli ya Rais. Tunawasubiria LATRA nao wapandishe nauli na gharama zote za usafiri and therefore, eventually, kila kitu kitapanda hence, ultimately, maisha yatakuwa juu and, consequently, tutaenda uchumi wa juu kama taifa. CCM! CCM! CCM!
 
Kwani mafuta yanayotumika nchini yanatoka Urusi au katika mataifa ya kiarabu??

Huu usanii utaisha lini mamaeeee
 
Watanzania wametakiwa kukubaliana na hali halisi kuhusu bei mpya ya nishati ya mafuta ikiwemo Petrol, Diesel, Mafuta ya Taa na Ndege ambayo itatangazwa Jumanne ijayo Aprili 5, 2022

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta si Tanzania pekee bali kote duniani kuna changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa nishati hiyo sababu ya vita ya Urusi na Ukraine.

Akizungumza katika mdahalo wa mafuta jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, Aprili 2, 2022 amesema hadi kufikia leo, nchi ilikuwa na hifadhi ya mafuta ya Petrol ya siku 27.

"Sheria inatutaka tuwe na hifadhi ya mafuta ya kuanzia siku 15. Ina maana hatuko katika hatari japo tunapaswa kuongeza uwezo wetu wa kuhifadhi zaidi," – alisema.

Mhandisi Chibulunje alisema kwa upande wa mafuta ya dizeli yapo ya kutosheleza siku 19, ya taa siku 108 na ya ndege yapo ya siku 35.

Mhandisi Chibulunje alisema kuwa matumizi ya mafuta kwa sasae ni mwezi mmoja na tayari mengine yameshaagizwa huku meli nyingine zikishusha shehena yake.

Aidha, amesema Aprili 24, 2022, kuna meli zitaingiza mafuta nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na nyingine ikitarajiwa kuingizwa nchini mwezi ujao kupitia Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa wote PBPA.

Mhandisi Chibulunje alisema kwa sasa Tanzania ina maghala makubwa matatu yenye uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa siku 122 katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Chanzo: TEF
 
Kwani mafuta yanayotumika nchini yanatoka Urusi au katika mataifa ya kiarabu??

Huu usanii utaisha lini mamaeeee
 
Hizi bei zinazoongezeka ni kwa kipato kipi??

Kwanini serikali isiweke pesa kidogo kupunguza makali.

Mizigo yote anabebeshwa mwananchi tu.

Wachumi wetu hawawezi shauri namna serikali inaweza fanya kupunguza mzigo kwa mwananchi??

Gharama za kila kitu zinapanda ila kipato ni kidogo.
 
Kwahiyo Tanzania nayo ilikuwa inanunua mafuta kutoka Urusi ? Samahani wakuu mwenye kufahamu hili ufafanuzi tafadhari!
 
Watanzania wametakiwa kukubaliana na hali halisi kuhusu bei mpya ya nishati ya mafuta ikiwemo Petrol, Diesel, Mafuta ya Taa na Ndege ambayo itatangazwa Jumanne ijayo Aprili 5, 2022

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema kupanda kwa bei ya nishati ya mafuta si Tanzania pekee bali kote duniani kuna changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa nishati hiyo sababu ya vita ya Urusi na Ukraine.

Akizungumza katika mdahalo wa mafuta jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi, Aprili 2, 2022 amesema hadi kufikia leo, nchi ilikuwa na hifadhi ya mafuta ya Petrol ya siku 27.

"Sheria inatutaka tuwe na hifadhi ya mafuta ya kuanzia siku 15. Ina maana hatuko katika hatari japo tunapaswa kuongeza uwezo wetu wa kuhifadhi zaidi," – alisema.

Mhandisi Chibulunje alisema kwa upande wa mafuta ya dizeli yapo ya kutosheleza siku 19, ya taa siku 108 na ya ndege yapo ya siku 35.

Mhandisi Chibulunje alisema kuwa matumizi ya mafuta kwa sasae ni mwezi mmoja na tayari mengine yameshaagizwa huku meli nyingine zikishusha shehena yake.

Aidha, amesema Aprili 24, 2022, kuna meli zitaingiza mafuta nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara na nyingine ikitarajiwa kuingizwa nchini mwezi ujao kupitia Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa wote PBPA.

Mhandisi Chibulunje alisema kwa sasa Tanzania ina maghala makubwa matatu yenye uwezo wa kuhifadhi mafuta kwa siku 122 katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

Chanzo: TEF

Wengine wanaweza je?

IMG_20220402_184504_432.jpg
 
Back
Top Bottom