EWURA: Bei ya mafuta ya Petroli yashuka

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,746
11,876
Bei za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam, zitakazoanza kutumika kesho Tar.2/2/2022 zimepungua kwa sh.21/lita (petroli), na sh.44/lita (Taa), wakati bei ya dizeli imeongezeka kwa sh.13/lita.

Bei za rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) zimepungua kwa Sh.123/lita (petroli) na shilingi 92/lita (dizeli)

Kwa mikoa ya kusini (Mtwara, Lindi na Ruvuma) zitaendelea kuwa zile zilizotangazwa katika toleo la Tarehe 5 Januari 2022, kwasababu hakuna shehena ya mafuta iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara.

Taarifa hii imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Mha. Godfrey Chibulunje, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari, katika ofisi za EWURA Makao Makuu jijini Dodoma Tar.1.2.2022

Kujua bei ya mafuta katika eneo lako bonyeza *152*00# kisha fuata maelekezo

----
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA NCHINI

Ndugu waandishi wa Habari,

Bei za mafuta hukokotolewa kwa kutumia Kanuni za Ukokotoaji wa Bei za Bidhaa za Mafuta - EWURA (Petroleum Products Prices Setting) Rules of 2022, na uundwaji wa kanuni hizi ulizingatia maoni ya wadau mbalimbali kabla ya kuchapishwa katika Gazeti la Serikali Na. 2A na 57 ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022.

Kanuni hizo zimeainisha gharama mbalimbali za lazima katika biashara ya mafuta. Gharama hizo ni pamoja na gharama za mafuta (FOB prices); gharama za uagizaji (Premium); gharama za uendeshaji wa biashara kwa jumla na rejareja (Wholesale and Retail Margins); tozo na ada za taasisi mbalimbali za Serikali, kodi na gharama za usafirishaji.

BEI ZA MAFUTA KWA MWEZI FEBRUARI 2022

BEI za rejareja za mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es Salaam zimepungua kwa shilingi 21/Lita (petroli) na shilingi 44/Lita (Taa), wakati bei ya dizeli imeongezeka kwa shilingi 13/Lita.

Bei za bei za rejareja kwa mafuta ya petroli na dizeli kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) zimepungua kwa shilingi 123/lita (petroli) na shilingi 92/lita kwa dizeli mtawalia. Hata hivyo kutokana na kumalizika kwa mafuta ya taa kwenye maghala ya
kuhifadhia yaliyopo Tanga, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kaskazini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

Bei za rejareja za mafuta ya petroli na dizeli kwa Mikoa ya Kusini (Mtwara, Lindi, and Ruvuma) zitaendelea kuwa zile zilizotangazwa katika toleo la tarehe 5 Januari 2022. Hii ni kwa sababu, kwa mwezi Januari 2022 hakuna shehena ya Mafuta iliyopokelewa kupitia bandari ya Mtwara. Pia Kwa kuwa hakuna maghala ya kuhifadhi mafuta ya taa katika bandari ya Mtwara, waendeshaji wa vituo vya mafuta kwenye mikoa ya Kusini wanashauriwa kuchukua mafuta ya taa kutoka katika bandari ya Dar es Salaam na hivyo bei za rejareja za mafuta ya taa katika mikoa hiyo itakuwa kulingana na gharama za kupokelea mafuta ya taa kupitia Bandari ya Dar es Salaam na gharama za usafirishaji mpaka mikoa husika.

UANZISHWAJI WA BEI KIKOMO NA BEI YA CHINI

Katika kuhakikisha kunakuwa na ushindani sawa (fair competition) katika bei zinazoanza kutumika kesho tarehe 2 February 2022, ununuaji wa mafuta kutoka kwenye maghala (wholesales) sasa kutakuwa na bei mbili, bei kikomo ambayo muuzaji hatatakiwa kuzidisha na bei ya chini ambayo vile vile muuzaji hatakiwi kushuka zaidi.

Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa kutumia fomula na Kanuni za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Magazeti ya Serikali Na. 2A na 57 ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022.

JEDWALI LINALOONESHA BEI ZA JUMLA BEI KIKOMO NA BEI YA CHINI

1.JPG

MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KWA MWEZI MACHI NA APRILI

Katika kufuatilia mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia, kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa bei za mafuta kwa mwezi Machi na Aprili 2022.

Hata hivyo, EWURA itaendelea kufuatilia mwenendo huo kwa karibu ili kuishauri Serikali hatua za kuchukua katika harakati za kupunguza makali ya bei za mafuta.

Lifuatalo ni Jedwali linaloonesha bei za rejareja kwa mafuta ya petroli, dizeli na taa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

JEDWALI LINALOONESHA BEI ZA REJAREJA ZA PETROLI, DIZELI NA TAA HAPA NCHINI (SHILINGI/LITA) KUANZIA TAREHE 2 FEBRUARI 2022

1.JPG
2.JPG
3.JPG
4.JPG
5.JPG
6.JPG
7.JPG

IMETOLEWA NA
Mha. GODFREY H. CHIBULUNJE
KAIMU MKURUGENZI MKUU
EWURA
01.02.2022​
 
View attachment 2104979

View attachment 2105006View attachment 2105007View attachment 2105008View attachment 2105009View attachment 2105010View attachment 2105011View attachment 2105012

IMETOLEWA NA
Mha. GODFREY H. CHIBULUNJE
KAIMU MKURUGENZI MKUU
EWURA
01.02.2022​

EWURA , ni Lini mtaita kwa ajili ya Interview, watu walioomba kazi kupitia Tangazo la August 2021?​

GBP na vituo vingi vidogo vilikuwa vinauza 2,480/- kabla ya hii bei mpya.
 
Ina maana ukijaza lita mia unaokoa 2100 tu,
Aisee bora ingebaki pale pale tu
Mfanya biashara ndo anafurahia hii kushuka kwa bei.

Mtu ana malorry kama 500 na kila lorry linajaza lita 400 kila siku. Unadhani anaokoa kiasi gani kwa mwezi mzima?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom