Ewura: Bei ya gesi ya kupikia imepanda kwa kati ya Tsh 2000 hadi 5000 kutokana na kupanda kwenye soko la dunia

nduza

JF-Expert Member
Feb 7, 2019
1,595
2,497
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) imetangaza kupanda kwa bei ya Gesi ya kupikia kwa kati ya Tsh. 2,000 hadi Tsh. 5,000 kulingana na ujazo wa Mtungi

Mabadiliko ya bei hizo ni kutokana na kupanda kwa bei ya Gesi katika Soko la Dunia. EWURA imesema kampuni za Gesi ndizo zitaamua lini zipandishe bei na kwa kiwango gani

---
Watanzania aliyetuloga sijui ni nani

Hawa jamaa wanaamua kutufanya wanavyotaka na hatuna la kuwafanya

Tozo, mafuta juu, gas juu maji na umeme wa kuungaunga

Machinga ndiyo kama vile wametiwa hasara bila kujali

Kwa kifupi tu gas ya 22000 itauzwa 24000

Na ya 53000 itauzwa 58000

Nadhani hii imeanza leo au itaanza kesho kwa mitungi ya oryx

Wananchi tupo tu tunaona ewala

Kuna wakati najilaumu

Ukitaka kumjua mtanzania vizuri lete habari ya yanga au simba au watu waonewe katika nyanja hiyo ndiyo utajua hujui lakini kwenye habari za msingi zinazohusu maisha moja kwa moja hakuna anayejali
 
Kwa nini unasema vitu vidogo, Kama binadamu anaweza kuuwa binadamu mwezio kwa sababu ya elf 2000 siyo kitu kidogo.
Ukiona mfanyab8ashara amepandisha bei ya kitu na bado watu wananunua tu, ujue watu wanamudu.

Watu wakishindwa kununua kwasababu ya bei maana yake, itabidi wafanyabiashara washushe bei ili mzigo uende.

Hilo ndio soko huria.
 
Ukiona mfanyab8ashara amepandisha bei ya kitu na bado watu wananunua tu, ujue watu wanamudu.

Watu wakishindwa kununua kwasababu ya bei maana yake, itabidi wafanyabiashara washushe bei ili mzigo uende.

Hilo ndio soko huria.
sio kweli..
.
kuna vitu inakulazimu ufanye sio kwa sababu unavimudu bali ni kwa sababu ni basic need yani bila hivo maisha hayaendi.
 
Back
Top Bottom