EWURA: Bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kuanzia Jumatano, tarehe 3 Agosti 2022

Baada ya ruzuku Dsm itakuwa 3410/= kwa lita moja 10,000/= unapata lita 2.9.

Diesel itakuwa 3322/= kwa lita kwa 10,000/= unapata lita 3.0.

Mungu Mwema.
 
Watu wanawaza mishahara tu, yani wanajiangalia wao tu kwamba yakipanda sio ishu kwakua kuna nyongeza ya mshahara na ambao wamejiajiri je! Hawana haki!! Hii nchi ngumu sana

Sasa mkuu mshahara wenyewe wa 30k Mbona bado ni majanga matupu.... wala usijisikie vbaya hamna cha maana kwenye iyo nyongeza mkuu wangu
 
Haya wakuu mkeka mpya ndio ushatoka. Angalia mkoa wako petrol au diesel imepanda Kwa kiasi gani
#KaziIendelee
Screenshot_20220802-221226.png
Screenshot_20220802-221216.png
Screenshot_20220802-221200.png
 
Mama aigize movie mpya kisha awatafute kina Mwijaku waende Zanzibar kutangaza utalii na kushawishi raia watembelee Serengeti.

Kisha baada ya hapo atembee nchi nyingine walau Ujerumani uko akalale wiki nzima kama alivyolala siku ngapi sijui uko Marekani na wageni wake.

Kisha serikali itunge kamati ya kutunga staili ya kutembea ya Watanzania, kama ambavyo kuna kamati ya kubuni vazi la taifa.

Kazi zipo nyingi tuachane na mambo ya mafuta maana "vitu vitazidi kupanda". Niliwahi dhani tutakuja kugundua Dr. Bashiru Kakurwa ni mjinga, ila sio mjinga sana kama tulivyofikiria
 
Back
Top Bottom